New administration under Samia Suluhu gives hope after 5 years of hopelessness

WAOMBOLEZAJI WAMWAGA CHAKULA MSIBANI HUKO KILEMA MOSHI, WADAI MAREHEMU HAKUWA AKIPEWA CHAKULA ALIPOKUWA HAI

Waendesha bodaboda wa kituo cha Kisangiro kata ya Kilema Kaskazini wilayani Moshi Mkoa wa Kilimanjaro wamevamia msiba wa Lenard Abel (20) na kumwaga chakula na pombe kwa madai kuwa ndugu na majirani wa marehemu wakimtelekeza hawakumsaidia chochote alipokuwa hai hata chakula tu walishindwa kumpa hali iliyolazimu bodaboda hao kupeana zamu za kumpelekea chakula.

Walifika katika msiba huo saa 9 alasiri jana Jumatatu Mei 3, 2021 baada ya mazishi wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula na kumwaga chakula hicho kitendo kilichozua tafrani na waombolezaji kulazimika kutimua mbio.

Shuhuda wa tukio hilo, Lucy Lyimo amesema kundi hilo la vijana lilifika msibani na kuvamia jikoni na kuanza kumwaga chakula na pombe aina ya mbege sambamba na kuvunja viti.

“Wakati mwenyekiti wa ukoo akitoa ratiba ya chakula kulitokea kundi la vijana zaidi ya ishirini wakipiga ukunga na kusema huyu marehemu kipindi akiwa hai alikuwa hapewi chakula iweje leo amekufa chakula kipo na pombe, " amesema Lucy akibainisha wakati wakisema hayo walikuwa wakielekea ilipohifadhiwa pombe na chakula

Amesema walipomwaga chakula na pombe waliwasha mishumaa na kuelekea makaburi yalikofanyika mazishi.

Mwenyekiti wa kijiji cha Kyou, Paul Lyimo amesema wakati vijana wakifanya vurugu za kumwaga chakula na vinywaji Padri wa Parokia ya Kilema aliyeendesha ibada ya mazishi aliwafuata kuwaomba wasifanye vurugu ila hawakusikia.

"Padri aliwapigia hadi magoti kuwaomba wasifanye hivyo lakini waliendelea kumwaga chakula huku wakipiga ukunga na baada ya hapo walienda kuwasha mishumaa kwenye kaburi na kutawanyika," amesema.

_____
NOTE: Kuna haja gani ya kuonesha unafiki wa kufanya mazishi ya kifahari kwa mwendazake marehemu ili hali hatukumjali alipokuwa hai? Kuna faida gani kutumia mamilioni ya shilingi kuonesha ufahari msibani huku baada ya msiba tukizitelekeza familia watoto na hata mjane wa mwendazake?

Ni unafiki na kufuru kunamjali sana marehemu kuliko mgonjwa au mtu alie hai ambaye ulikuwa na nafasi ya kumsaidia lakini ukangoja afe ili jamii ikuone wewe una pesa siku ya mazishi.

Ni unafiki na kufuru kunatumia gharama kubwa za mazishi na tunajitolea sana lakini hatujitolei kuokoa maisha ya mgonjwa.

Ni unafiki kujifanya kuwa upo bize na mambo yako na huna muda wa kwenda kutizama mgonjwa lakini akifa tunapata muda wa kwenda kukesha msibani.

Wengine hawajahi kupata kabisa zawadi za maua lakini wakifariki yatakuja mengi sana juu ya kaburi lake. This is none sense.

Tutapamba kaburi kwa marumaru hata kama nyumba ya marehemu haikuwai kuwekewa marumaru. Je tulimuacha aishi kwa ufikara ili maiti yake ioze kifahari?

Tumekuwa wanafiki kupitiliza wakati mwingine ukifuatilia ripoti ya daktari unaambiwa marehemu alidhoofu kutokana na lishe duni na msongo wa mawazo baada ya kutelekezwa na ndugu, watoto na hata marafiki. Wanafiki hawahawa siku ya mazishi utaona wakiingia na pikapu iliyosheheni vyakula na jeneza la kifahari ambalo nusu ya gharama yake ingetosha kuokoa maisha ya mwendazake kwa kupata tiba na lishe bora....

Lazima tujue thamani ya Maisha kuliko Kifo tuache UNAFIKI!!!
 
FUNZO,,,,KAMA UNAPITIA KIPINDI KIGUMU HII ITAKUSAIDIA
Kila mtu huwa mwenye malengo ambayo huwa anatarajia kuyatimiza na matokeo mabaya huwa yanavunja moyo sana

Kila mtu huwa anaumizwa na matokeo mabaya kwa sababu huwa yanapunguza morali ya kujiwekea malengo mengine makubwa

Ukifanikiwa kwenye malengo huwa unapata nguvu sana ya kujiwekea malengo mengine na huwa unajiamini sana na kujikubali sana na kuona kuwa unaweza

Ikiwa utapata matokeo mabaya huwa unapata hasira na kuanza kutilia shaka uwezo wako

Kitendo cha kujitilia shaka husababisha huzuni, kupoteza morali,kuishiwa mawazo ya kuboresha kazi yako ,hufanya uamini huwezi kufanikiwa tena hivyo hisia za kukata tamaa huanza kuja

Kuna nyakati utaona kama upo kwenye kisiwa cha pekeako ambapo unajiona mpweke sana ,huoni sapoti kutoka kokote,huoni watu uliowazoea,utaanza kujiuliza umewakosea nini walimwengu mpaka wanaokuacha mpweke uteseke

Katika hali ngumu za maisha kama kipindi cha maradhi,kipindi huna pesa,kipindi umeachwa na unaowapenda ,kipindi huna kazi ya kueleweka,kipindi migogoro ni mingi sana maeneo yako ya kazi

Ni kipindi kigumu sana lakini tafsiri unayoweka juu ya ugumu huo huwa inafanya ugumu huo kuonekana mkubwa kuliko kawaida

Unatakiwa utambue kuwa kufeli,kukataliwa,malengo kwenda tofauti,ahadi kuvunjwa ni kawaida

Tambua kuwa haijalishi upo katika hali ngumu kiasi gani kumbuka kuna mtu amepitia hali ngumu kuliko wewe na aliweza kuondokana na hali hiyo

Habari nzuri ni kuwa matatizo huwa hayadumu isipokuwa fikra zako juu ya tataizo ndio huamua ugumu huo uendelee

Unatakiwa utambue kuwa wewe ni binadamu tu hivyo kukosea ni kawaida na kupata matatizo ni kawaida

Wastani wa binadamu kupata matatizo ni miezi 3 hivyo tambua kuwa ndani ya miezi 3 utakuwa na tatizo vilevile unaweza kukumbuka miezi 3 iliyopita kama hukuwa na tatizo lolote la kiafya,kifedha, marafiki, mahusiano na kazini au biashara zako

Hivyo basi tambua kuwa binadamu hujifunza kwenye maumivu na makosa

Bila matatizo maisha hayana maana

Unatakiwa ujifunze kanuni za asili "Law of cause and effect" ni KANUNI ambayo kueleza kuwa kila jambo hutokea kwa sababu na ikiwa hujui sababu bado sababu ipo

Tambua chanzo cha matatizo yako kisha tafuta suluhu yake

Ikiwa unapitia kipindi kigumu jiulize kuwa unaweza kulitatua tatizo lako na ikiwa huwezi basi liache

Kuendelea kung'ang'ania jambo ambalo huwezi kulikabili kutazidisha maumivu na hasira

Kukasirika kwa sababu maisha ni magumu ni kujipa adhabu kwa kosa hujafanya

Kwanza maisha hayawezi kuwa mazuri kwa sababu eti umekasirika au unapitia kwenye maumivu badala yake tafuta ufumbuzi wa ugumu huo

Ikiwa tatizo lako linahitaji kufanyiwa upasuaji maana yake unatakiwa ufanyike upasuaji sio kulia ili watu wakuonee huruma

Ikiwa pesa ndio ngumu maana yake unatakiwa utafute pesa sio kulia ili watu wakuonee huruma

Ikiwa mapenzi ndio tatizo unatakiwa utambue kuwa huwezi kudhibiti tabia za mwengine bali tabia zako tu hivyo kukasirika kwa sababu ya tabia za mwengine ni kujipa adhabu kwa kosa hujafanya

Tabasamu kwa sababu haumiliki matatizo yote ya ulimwengu

Inawezekana hujaoa kwa sababu ya kipato au kuolewa na umri unakwenda kasi lakini hutakiwi kukasirika kwa sababu watu hawafungi ndoa kwa sababu wanajua kukasirika

Kutaka watu wakuonee huruma kutafanya upate maumivu makubwa sana na utazidi kujiona mnyonge sana kiasi cha kuamini hustahili kupata matatizo

Ondoa fikra za kujiweka kwenye unyonge kisa tu maisha ni magumu

Hata kama unalala njaa,hata kama unalala chini,hata kama huna kazi,hata kama huna ajira,hata kama hakuna anaekuamini,hata kama huna kizazi,hata kama upo kwenye kiti cha magurudumu,hata kama upo kitandani hospitalini,hata kama hupewi sapoti sio sababu ya kujiweka kwenye unyonge

Kujiweka kwenye unyonge huzidisha maumivu mpaka utaona kama unaonewa sana kwa maisha magumu unayopitia

Ni kweli hakuna anayependa maisha kuwa magumu lakini hatuwezi kupinga ukweli kuwa maisha hayajawahi kuwa mepesi hata siku moja

Kila mwaka utasikia maisha ni magumu sana maana yake lazima ukubali kuwa hayo ndio maisha sio movie

Kikwazo chochote kilichopo njiani hiyo ndio njia yenyewe ya mafanikio

Tazama tofauti na utaona tofauti.
Kutarajia maisha yako kubadilika wakati wewe hujabadilika ni kuchanganyikiwa

2+2=4 ukitaka upate 5 badilisha namba sio kulia au kutaka watu kukuonea huruma

Kujiweka katika unyonge ni adhabu watu wengi huwa wanajipa

Hata kama dunia nzima wamekata tamaa juu yako kamwe usikate tamaa juu yako

Hata kama hakuna anaekupa faraja sio sababu ya kujichukia

Ondoa fikra kuwa "kwanini mimi " badala yake weka fikra "Nifanye nini sasa"

Jana imepita na haiwezi kurudi na fursa zote za jana haziwezi kurejea

Kesho haijafika na huna sababu ya kuweka hofu kuhusu kesho kwa sababu hofu haiwezi kuifanya kesho iwe tofauti

Maisha yako yanajengwa na leo sio jana au kesho

Hali yako ya sasa ni matokeo ya maamuzi ya siku zilizopita na ikiwa unataka maisha yako kuwa tofauti fikiria kitu tofauti

Kujuta kwa makosa ya zamani ni kupoteza muda

Huwezi kurudi nyuma kurekebisha makosa yako bali unaweza kujifunza kwenye makosa yako

Kila mtu anafanya makosa hivyo kukosea ni kawaida

Kufeli ni kawaida
Tambua kuwa huwezi kuwa mzuri kwa kila mtu na huwezi kuwa mbaya kwa kila mtu

Hakuna mzuri 100% wala mbaya kwa 100%

Adolph Hitler tunajua mabaya yake mengi sana lakini wapo waliokuwa wakimpemda sana

Hivyo haijalishi umefanya kosa kubwa kiasi gani bado wapo watu watakupenda na haijalishi utakuwa na mazuri kiasi gani bado kuna mtu atakuchukia

Binadamu hupokea taarifa kisha huzichuja kwa hisia zake za wakati huo

Endapo atakuwa na furaha hupokea taarifa kwa mazuri yake na akiwa na huzuni hupokea taarifa kwa huzuni

Mtu hawezi kukusema kwa mazuri ikiwa yeye mwenyewe huwa anajisema kwa mabaya muda wote

Kupata kitabu cha
1.FIKRA ZAKO FURAHA YAKO (softcopy)
2TIBA YA MSONGO WA MAWAZO (hardcopy & softcopy)
3.BADILI FIKRA ZAKO BADILI MAISHA YAKO (hardcopy & Softcopy)
4.MALEZI YA UBONGO KISAYANSI( hardcopy & softcopy)
5.TABIA ZA WATU WALIOFANIKIWA (Hardcopy & softcopy)

6 MISINGI 10 YA FURAHA SIKU ZOTE (hardcopy &softcopy)

+255766862579
+255622414991

Imeandikwa na Psychologist
Said Kasege
Temeke,Dar es salaam
 
I believe
1620276873830.jpg
 
Back
Top Bottom