laskaboza
Senior Member
- Jun 8, 2020
- 144
- 1,601
Kuna Movie moja hivi ya ki China (nimesahau jina) niliwahi kuangalia zamani kidogo. Kuna mahali kijana mmoja alikua anataka kuoa kwaiyo akamuomba babu yake ampe ushauri kuhusu wanawake. Babu yake akamwambia;Hata siku moja ukiwa kama mwanaume usije kuthubutu ku open up kwa mwanamke na kuonesha your soft side your emotional side, sababu mwanamke akigundua your insecurity akigundua your soft side, umempatia silaha ya kukuumiza nayo maishani atatumia hiyo kuharibu maisha yako, atatumia hiyo kukuangusha, atatumia hiyo kukufanya ujione you are not man enough.
Jambo moja unapaswa kutambua mwanamke anapenda strong man masculine man, lakini wanahitaji soft men kwa ajili ya kuwa control siku zote wanawake wanapenda wanaume ambao ni desirable wanaume hao ni strong man, tatizo la strong man ni wagumu kuwapata na hata ukiwapata ni vigumu kuwa control.
Strong man ni desirable moja ya weekness zao au tabia zao ni kutokuwa controlable, maisha ya mwanamke na strong man, hayana guarantee kabisa, moja ya technique wanazotumia wanawake ni kumtafuta strong man, kisha kumharibu kumtesa ki akili kisha kumtawala, wanafanya hivi hili ku establish koloni lao kuhakikisha kwamba wewe hautoki kamwe na kwamba hautoweza kumuacha.
Kitu kimoja wanawake wanashindwa kuelewa baada ya wao kufanikiwa kumtawala mwanaume wanapoteza ule mvuto ambao mwanzo walimuona nao, hivyo akitokea another strong man mwanamke anavutiwa naye na anahamia kwake na mzunguko huo unaendelea tena.
Ukiwa kama mwanaume na unapatwa na shida na some feelings bora hata upeleke kwa mama yako au ukalilie kwa mwanaume mwenzio, ukijiloga kumchukulia mwanamke kama mfariji wako kama mshauri wako katika maswala ya emotion na feelings unampatia mwanamke mkuki wa kukuchoma nao never show weekness to a woman, she will use it agains you, huu ni moja ya mzigo wanaume wanapaswa kubeba wenyewe.
"Show her you care, but never let her know how much you love her"
Leo nimeona huu uzi nikakumbuka hayo maneno ya kwenye ile Movie (Ilikua na subtitle) .
Mwanaume unatakiwa umjali mwanamke wako, mahitaji yake umtimizie lakini kamwe usije ukamuonesha unampenda kiasi gani! Yeye ndio anatakiwa akukadirie jinsi unavyompenda lakini asiwe na uhakika ni kwa kiasi gani. Namna bora ya kufanya hivi ni kujitahidi sana kuonekana neutral linapotokea jambo lolote linalogusa hisia zako kwa nguvu. Sio kisa tu umemuona dame wako amesimamishwa na mjamaa njiani, unaenda kuleta ugomvi nyumbani bila kujali walikua wanaongea nini. In fact, issue kama hizi unatakiwa kufuta tu mdomo kama haujaona vile, sijui kama unanielewa vizuri...!!
Mwanamke ataku.challenge sana kwenye vitu vingi ili tu akuone unavyo.react achukue point.. lakini wewe unatakiwa kumfanya aone kama kila kitu kwako wewe ni KAWAIDA tu. Akipatwa na tatizo, mfariji na sio kulia lia tena kama yeye. Mshirikishe mambo ambayo unaona anaweza akawa na msaada nayo tu, potezea mambo ambayo unajua hawezi kukusaidia chochote. Na hata akitishia kukuacha au akakuuliza kitu cha kukutega, usi.panick, fanya ajue tu kuwa hakuna kitu kitakachokutokea ambacho utashindwa kukabiliana nacho. Yes, that is a Sign of a Real Strength!
Ukiwa na mindset ya namna hiyo kama mwanaume, mambo mengi sana utayamudu sio tu kwenye mahusiano, lakini hata kwenye nyadhifa mbalimbali katika maisha. Hata ukitaka kuwa mfanyabiashara mzuri au kiongozi mzuri mahali popote pale, jaribu sana kukaa mbali na emotional decisions. Maamuzi ya hisia ni alama ya udhaifu!
La Mwisho, sio kila mwanaume anaweza kumudu changamoto zake zote za maisha peke yake. Na sio kila mwanamke ana tabia ya kutumia matatizo ya mwanaume kama silaha ya kumtawala. Kikubwa ni kujifahamu wewe na wanaokuzunguka. Kama umejaliwa kuwa na watu sahihi wenye msaada na nia njema kwako sio mbaya ukiwashirikisha mambo yaliyokuzidi uwezo wakusaidie hata kama ni wanawake. Just make sure unashare madhaifu yako + feelings zako na watu sahihi : )