Bujibuji Simba Nyamaume
JF-Expert Member
- Feb 4, 2009
- 75,203
- 157,362
Somo: Baadhi ya kauli unazopaswa kuziepuka unapokuwa umeumizwa na kujeruhiwa moyo wako.
1. Usiseme, "sitaoa/kuolewa tena " maana katika maisha ndoa inayo nafasi yake kukusaidia kutimiza ndoto za maisha yako, ndiyo maana mungu akasema "si vyema mtu awe peke yake na wawili ni bora kuliko mmoja "kuoa /kuolewa ni nguzo muhimu inayoshikilia maono yako.
2.Usiseme, "hautamsaidia tena mtu ",kwa sababu uliowasaidia wamekujeruhi. Kwa sababu wapo watu wema na wenye fadhili wanaouhitaji msaada wako ambao Mungu anapitisha maishani mwako uweze kuwafikia huko walipo, kuwafungia mlango ni sawa na kuwafungia mungu mlango.
3. Usiseme , "sitasamehe" maana mbinguni hauwezi kuingia kama haujamsamehe mtu, mbona mungu amekusemehe dhambi zako tena nyekundu sana, na pia kutokusamehe kunakufanya mungu akufungie mlango ya mbinguni.
4.Usiseme, "utakufa/ ueumbiwa mabaya tu " ,hata kama iweje usijitamkie kifo au mambo mabaya, kwa sababu maneno ya kinywa chako yatakufunga na ipo siku yatatimia.
5.Usiseme, "nitalipiza kisasi " kwa sababu kisasi huwa analipa mungu tu, wewe kutaka kulipa kisasi nikumwingilia mungu majukumu yake, mungu akikilipia ndiye atakaye kulipia vizuri a kikamilifu kuliko wewe ukilipa.
6.Usiseme, "namwombea yamkute mabaya", maana imeandikwa msichoke kutenda mema na waombeeni adui zenu, na wewe kama mkristo wa kweli, lazima ujifunze kuishi maisha ya ziada, yatakayo mfanya mkosaji ajue kosa lake na aseme ,hakika una mungu .Ushinde Ubaya kwa kutenda mema.
7.Usiseme, "sitapenda tena ", maana si kila mwanadamu ni mjeruhi /mkatili kama huyo aliye kujeruhi, cha msingi kaa magotini, mungu atakupa atakaye kupenda,na utakaye mpenda kama kristo alivyolipenda kanisa.