Uelewa wangu, Zip (Zone Improvement Plan) , Postcode(Postal code)
ZIP code hili hunichanganya linapotumika. Kuna kitu kinaitwa country code mfano Tanzania ni +255, China ni +86 na Nigeria ni +234. Sasa hizi country code huwa zinatumika kama ZIP code.
Postcode , hii ni postal code hii sasa hutofautisha eneo dogo zaidi ya zip code, hizi hutumika sana na makampuni ya POSTA ya ndani katika kusambazia bidhaa zao. Hizi postcode kwa hapa Tanzania zipo na zinatofautiana kwa kila ward(kitongoji/kijiji) na ward.
Mfano: Postcode ya Dar es Salaam ni 11000, Sasa kama unakaa Sea View utatumia postcode ya Kivukoni ambayo ni 11101 .
Hizi kila nchi wanajua wanavyoweka unaona hapa kwetu tunatumia tarakimu tano (*****) , South Afrika tarakimu nne (****) nk .
Eneo linalowakilishwa na postalcode hizi linahitajika kuwa ndani ya zipcode(Country code) moja.
Panaponichanganya: Je kuna nchi zina-zipcode za ndani au huwa wanasema tu wakiwakilisha postcode. USA ina country code ya +1 ambayo mimi naitambua kama zip code, ila kuna sites zinaoneshaga kuna ZIP codes ndani ya USA, Je majimbo yao yamegawanywa kwa ZIP halafu ndiyo zikaanza postal code au vipi. Kuna nchi zingine pia vivyo hivyo japo country code yao inakuwa inajulikana.
Nimeattach file lina orodha ya postcode za Tanzania , unaweza lidownload (4mb), linapatikana pia kwenye tovuti ya tcra.
Krait,
Mars Rover,
smartfocus,
kukudume2015,
@josephzeclassic92,