Netanyahu: Israel haiyakubali mapendekezo ya Hamas

The Zanzibar Echo

JF-Expert Member
Joined
Apr 21, 2025
Posts
490
Reaction score
836
Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu amesema Kundi la Wanamgambo wa Kipalestina la Hamas linatafuta mabadiliko "yasiyokubalika" kwa pendekezo jipya la kusitisha mapigano huko Gaza Ukanda.

Netanyahu amenukuliwa na Shirika la Habari la DPA, akisema mabadiliko ambayo Hamas inataka kuyafanya katika pendekezo la Qatar yaliofikishwa kwao usiku wa jana hayakubaliki kwa Israeli. Maafisa wa Hamas waliiambia DPA kuwa bado kuna haja ufafanuzi kuhusu kuendelea kwa usitishaji mapigano baada ya kipindi cha awali cha siku 60, kuondolewa kwa wanajeshi wa Israel Gaza na upatikanaji wa misaada ya kibinadamu katika eneo hilo pasina vikwazo.

Mazungumzo hayo yanayoratibiwa na Qatar, Misri na Marekani yanalenga kufanikisha makubaliano ya kusitisha mapigano kwa siku 60 huko Gaza na kuachiliwa kwa mateka ambao bado wanashikiliwa na Hamas, na baadhi ya wafungwa wa Kipalestina wanaoshikiliwa na Israel.
 
Hamas si walianzisha vita October 7 wenyewe ulitegemea Netanyahuu angefanyaje
Kabla ya hiyo Oktoba 7, unafahamu jela za Israel kitambo tu zimejaa Wapalestina wa kila aina! Kuanzia wanawake, watoto, wazee, vijana, nk. Achilia mbali wale waliouwawa, kuteswa, nk na hao Waizrael!

Binafsi ninachofahamu hao Hamas ni zao la manyanyaso yaliyopitiliza kwa Wapelestina miaka nenda. Kusingekuwepo na uonevu, mateso, mauaji yasiyokwisha, nk. inawezekana kabisa hao Hamas wangekosa watu wa kuwaunga mkono kwenye hizo harakati zao.
 
Unajadiliana na mfia dini tutusa huyo mkuu.
Kila jambo analichukulia kiudini udini mkuu.
 
Netanyau mbona hakung'ang'ania kuendelea na vita kati yake na Irani kama anavyong'ang'ang'a kuendea vita Hamasi?
 
Kwa Iran alilalamika kua wamerusha mabomu kipindi Cha cease fire imeanza 🤣🤣🤣
Hapa kwa gaza hatk cease fire
 
Iran alifikia lengo lake
Kwa makamanda kadhaa na wanasayansi kulamba udongo
 
Kabla ya hiyo Oktoba 7, unafahamu jela za Israel kitambo tu zimejaa Wapalestina wa kila aina! Kuanzia wanawake, watoto, wazee, vijana, nk. Achilia mbali wale waliouwawa, kuteswa, nk na hao Waizrael!

Binafsi ninachofahamu hao Hamas ni zao la manyanyaso yaliyopitiliza kwa Wapelestina miaka nenda. Kusingekuwepo na uonevu, mateso, mauaji yasiyokwisha, nk. inawezekana kabisa hao Hamas wangekosa watu wa kuwaunga mkono kwenye hizo harakati zao.
Hata jela zetu zimejaa lakin
 
Magaidi waanzishe vita Oct 7 halafu unamlaumu kamanda Netanyahu kwa kuipigania nchi yake?!
Kwani mwenye kuleta mapendekezo ninani si uyo uyo Baba wa Israel sasa mlete pendekezo vita isimame kisha analeta na masharti tena ni

Hamas ndio watatoa miongozo iweje iweje uyo Netanyahu m'bana pua tu.
 
Kweli Israel angeikuta Iran ni mnyonge angesitisha vita? jamani tuacheni ushabiki wangekaa sana pale,kumbukeni Israel ni US na pale Irani Kuna mafuta mengi sana na wangekaa sana,hapo inawezekana alipima kina cha maji akaona ni kirefu akasitisha vita
 
Hamas si walianzisha vita October 7 wenyewe ulitegemea Netanyahuu angefanyaje
kwasababu hujui kitu ndo maana unadhani walichofanya HAMAS oct 7 ndo walianzisha,kwamba kabla ya oct 7 israeli na palestina hakuna chochote kilichokuwa kinaendelea...kilichofanywa oct 7 ni kulipa kisasi cha unyama ambao israeli walikuwa wanawafanyia wapalestina kila siku iendayo kwa MUNGU
 
Hivi kuna faida gani kupokea maiti ya mateka?

Yani mnakaa miezi 8 mnajadiliana mpewe mwili, hizo maiti zao zinathamani gani?

Hawa wanaouwawa kwa mabomu kila siku wao hawahesabiki au ndio kuonyesha uwezo?
 
Back
Top Bottom