ngoshwe
JF-Expert Member
- Mar 31, 2009
- 4,141
- 951
=Musoma Mara=
Mimi ni mgeni wa mji huu. Tulipoingia na jamaa yangu kikazi, sikuona haja yakujifungia vyumbani, nilimwomba jamaa tutoke kuzungukia maeneo ya kupumzikia.
Nilichojifunzatukiwa kwenye Baa moja hapa ni jinsi wananchi walivyokuwa wakarimu. Tumeingia tu tumepokelewa na "Karibu kina baa, eeh, karibuni ..." (kwa rafudhi ya kikukra, kijita kizanaki). Ni kundi kubwa la kina Dada, wapata watano wanatukaribisha Baa lakini kila mmojaanaonekana kama ana hadidu za rejea anania ya kuzikamilisha . Tunaulizwa, "eti,mngependa kukaa karibu na wapochoma kuku au hapahapa..? kabla hatujajibu jamaa wa jikoni analeta kuku aliyechinjwa kwenye sinia "Baba kuku wapo, bei poa tu".
Tunaamuakukaa karibu na jiko. Baada ya kuagiza "Pombe", mara kati ya wale akina dada waliotukaribisha, wawili wanakuja kukaa pale tulipokaa… mmoja anauliza "mpo peke yenu" . Namuuluza una maana gani?Anajinu "eh, tusije tukapigwa"…natabasamu. Ghafla wote wawili wamakimbia kufuatawateja wengine….wanawakaribisha na kuturejea..hapo nabaini utaratibu ni huo.
Baada yamuda jamaa yangu ananionyesha mwanamke, amesimama karibu na "Kaunta",kamfungasha sana ..jamaa yangu imemshitua..anaonyesha kuwa na shahuku nae.Amwita "Baa Maid" na kumwomba amwitie. Yule Baa maid anauliza "sasa na sisi?,yaani we umemwaona yule tu..haya ngoja nimwite..". Yule Mwanamke kwanza anakataa, Baada ya muda anakuja lakini akiwa na mwenzie ambae kalewa chakali hatakuongea hawezi vizuri. Wanaketi pamoja nasi. Jamaa yangu anaagiza kinywaji,yule mwanamke anamzuia asiwamgizie mwenzie aliyelewa lakini inaoekana yulealiyelewa anataka kuleta vurugu kwa kutonunuliwa pombe.
Binafsi moyoumekosa furaha kukaa na wale wanawake ila nalazimika tu. Jamaa yangu anaagizakuku mzima, tunakula ..stori zinaendelea. Kwenye meza ya pili kuna wanaumewatatu na mwanamke mmoja. Huyu mwanamke anatutizama sana kila wakati anapinduashingo kutuangalia kule tulikokaa.. Baadae anageuza kitiu chake na anaonyeshaamepoteza hamu na mazungumzo kwenye meza aliyokaa..ananitizama machoni nakutikiza kichwa kama anaesikitikia jambo.
Baada yamuda jamaa yangu anasimama kwenda maliwatoni. Yule Dada wa meza ya pili naanachukua sekunde na kusimama…anakwenda "kaunta"ambayo ipo karibu na njia ya kwenda chooni. Jamaa yangu anapotokea chooni yule Dada anamwita..naona anamnong'oneza jambo huku akionesha kidole kule tulikokaa. Jamaa zake wale wa kiume hawajaona kitu wao wanafuatilia muziki wa kihaya (SAIDA KALOLI) kwenye TV.
Jamaa yangu anaporejea na jaribu kumdadisi yule dada anataka nini na kwanini amno'ngoneze mtu hawafahamiani?, anasema "just wait" (nisubiri). Baada ya muda anawaambia wale kina dadatuliokuwa nao "sasa jamani inatosha, sisi hatuna mpango nanyi". Wale kina dadawanaonyesha hasira kwa nini, kwani wao hawana nini?...Jamaa yangu ana waambiakuna wake zetu wanakuja, wanaogopa na kuhama meza.
Tukiwa hapokitambo, pombe zinapokolea, ile meza yapili wanaoume wawili wanaondoka na kubaki mmoja na yule Dada. Ghafla wanaanza kutuchangamkia, wanavuta viti karibu, yetuDada anauliza "ninyi mnatokea wapi,naona sio wa hapa", mimi natokea Dar, , ila nafanya kazi hapa Musoma…tunazoena ana yule jamaa yake (mwanaume) nae anajitambulisha kuwa yeye ni Mwalimu Mbeya alikuja kumsalimu yule Dada nirafiki yake wa kike. Baada ya kuzoeana yule Dada anatueleza akimtizama jamaayangu: "Kaka samahani sana mimi ni Nesi hapa, nilipowaona na wale kina dada moyouliniuma sana, nimekuwa nikiwasihi muda mrefu wasifanye vile wanavyofanya, waowana kiliniki chini yangu, wanapaswa kujichunga na kuwalinda wengine lakinisiku hizi wameanza tena biashara yakujiuza , hasa kwa watu wangeni hapa Musoma., niliumia sana kuwaona kaka zanguwenye afya njema mkiingia kwenye matatizo , wale wote ni wangonjwa. Yulemwingine aliyefunganisha nyuma alikwisha sana na ukimwaona mchana huwezikumdhania, huwa inasadikika anaweka vigodoro huku nyuma". Akasisistiza, "ogopeni sana hapa, sisi tuliokuwa kule mahospitali tunajua sana, pengine moyo unakuuma ukiona mwenzio ana kwenda kuangamia,..haijalishia hata kama wewe unao lakini ukiona mwingina anataka kuambukiza wenzake kwa makusudi, Mungu anasema mlinde yule asiye na hatia".
Akakazia,:"Mimi mwenyewe na huyu jamaa yangu kila hakija nahakiisha anatumia kinga, simwamini huko hatokako..."
Moyo ulinishtuka… jamaa yangu akasema "Asante, Nesi wa Musoma, duh, tembea uone, hakika umetuokoa!!"
Nilihisimwili kuingia ubaridi, sikuelewa kauli ile ya jamaa yangu "hakika umetuokoa!!",nikajiuluza moyoni' Alitaka kwenda kupiga kavu kavu? Au kama asingeambiwa yule Dadaana matatizo asingemchukua? Au kwa hamu ile aliyokuwa nayo kutokana na kuonamfungasho wa nyuma, Je, moyoni anaweza kuamini tu kuwa yule Dada ni mgonjwa??. Hivikumbe mwanaume hawezi kuvumilia asizini mpaka aambiwe kuwa yule anayetakakuzini nae kaathirika?>>