Neno shemeji halina maana tena

Neno shemeji halina maana tena

JEKI

JF-Expert Member
Joined
Aug 16, 2013
Posts
4,845
Reaction score
2,968
Baada ya kuwaza kwa muda mrefu sasa nasema hadharani neno shemeji halina thamani tena kama ile ilivyotarajiwa, ukiwa kwenye daladala utasikia konda akiomba nauli kwa wadada, hapo shemeji, hivi kweli shemeji yako utamuomba nauli?

Au hata mateja yakiona mdada yanaita shemeji, yaani neno shemeji limekuwa kama mzaha na dhihaka tu, heri tuitane kwa majina tu.
 
Mm nazani makonda wako sahihi kwani wanajua huyo ni mke au mshikaji wa mtu ndi maana konda anamuota shemeji kkama kimiheshimu
 
unapendekeza makonda watuitaje ilhali hawajui majina yetu????
 
Baada ya kuwaza kwa muda mrefu sasa nasema hadharani neno shemeji halina thamani tena kama ile ilivyotarajiwa, ukiwa kwenye daladala utasikia konda akiomba nauli kwa wadada, hapo shemeji, hivi kweli shemeji yako utamuomba nauli?

Au hata mateja yakiona mdada yanaita shemeji, yaani neno shemeji limekuwa kama mzaha na dhihaka tu, heri tuitane kwa majina tu.

Uhalali wa neno shemeji unatoweka sababu hilo neno limetumika na konda au??? Sikuhizi imekuwa kawaida sana...
Maneno kama Kaka, Sista, Mjomba, Ndugu, Faza, Mwana hutumika sana hasa pale ambapo watu hawajuani majina..
 
Hakuna tatizo mkuu ni sawa na kupeana heshima bila ya kujali matabaka kama tunavyoitana hapa kijijini Mkuu au Kiongozi
 
Back
Top Bottom