Pascal Mayalla
Platinum Member
- Sep 22, 2008
- 52,692
- 119,327
Wanabodi,
Tumezoa kusikia neno "Matukufu" kila yanapotajwa Mapinduzi ya Zanzibar ya January 1964, Jee neno hili, Matukufu, lilitokea wapi na lina maana gani kwenye Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar, na kama ni kuhusu utukufu wa Mapinduzi hayo, Jee Mapinduzi ya Zanzibar yana utukufu gani hadi kustahili kuitwa Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar?!.
Nakiri kupandisha uzi huu, kufuatia mchango wa mwana jf huyu, Maalim
Mohamed Said kwenye uzi
Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar: Kumbe Waarabu Hawakufukuzwa .
kuhusiana na neno Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar!.
Na nikimsoma Maalim Mohamed Said, amesema kwa mujibu wa Imani ya Dini ya Kiislamu, "Utukufu ni wa Allah pekee!", Jee hili ni kweli kuwa Kiislam neno Utukufu hutumika kwa Allah pekee?!, Jee sasa hawa Waislamu tena Swala tano, tunaowasikia kila siku wakitoa utukufu kwa Mapinduzi, ina maana kila anayeyaita Mapinduzi Matukufu jee anatenda dhambi dhidi ya utukufu wa Allah pekee?!.
Pia kuna maneno Ikulu ni mahali patakatifu!, Bunge Tukufu, hadi Mtukufu rais...inawezekana wote hawa wana kufuru?.
Paskali

Kitu ninachokiona kwa Pasco ni kutokujua ukweli wa mauaji
ya dhulma waliofanyiwa watu Zanzibar katika na baada ya
mapinduzi.
Ana
Yeye hajui anapotumia maneno ''mapinduzi matakatifu,'' nk. nk.
kuna watoto wa waliouliwa na wajukuu zao wanasoma maneno
haya na maini yanawakata.
Nawaomba wajuvi wa mambo ya Zanzibar mtujuze, Jee Mapinduzi ya Zanzibar ni Mapinduzi Matukufu, au ni Mapinduzi tuu?!, kama ni Mapinduzi Matukufu, Jee Mapinduzi yele yana utukufu gani?!.Pasco,
Kuna mtu baada ya kuona hii post yako yako kwa
uchungu anasema huyu ni mtu wa kuapizwa.
Ana maana na wewe auliwe katika wako ujue uchungu wa mwana
kuuliwa kwa mapanga na risasi.
Nimemtuliza.
Nimemwambia haifai.
Nimemwambia kuwa nimekuasa uache
Nimemweleza hafai kuapizwa ila kuombewa dua.
Kanitajia baba yake alivyouliwa kisha akaja mtu akaipiga teke maiti
ya baba yake yeye akiona.
Pasco hili si jambo la ushabiki na kujiona wewe hodari wa lugha kwa
kuandika, ''mapinduzi matakatifu,'' na mengine.
Utukufu ni wa Allah pekee.
Umezungumza kuhusu mapinduzi daima.
Ikiwa ni hivyo iweje sasa Wazanzibari wanaiangusha CCM mfululizo kila
uchaguzi?