Neno MAMA LISHE kwa kingereza

Mama Lishe a.k.a Mama Ntilie kwa lugha ya Kiingereza tunaweza kulinganisha na mhudumu wa kantini yaani 'Dinner Lady '.

Mhudumu wa 'kantini' au kibanda cha mama ntilie kwa mazingira ya Ki-Tanzania anaweza kuchukua nafasi zote mbili /tatu anapika, kupakua na kutilia / kugawa.

Hivyo neno la Kiingereza kwa Mama lishe /Mama Ntilie lafaa kuwa Dinner Lady badala ya Food Vendor ambaye anaweza kuwa muuzaji matunda, mboga za majani , mihogo mibichi, samaki wakavu, unga wa sembe n.k
 
Mkuu habari,

Kitaalamu, tunasema lugha ni zao la utamaduni. Kwa hiyo, lugha hutegemea sana utamaduni wa sehemu husika, au kwa kisukuma tunasema, Every language is culture-specific. Kwa hiyo, kabla hujauliza neno 'mama lishe' kwa kiingereza ni nini, ni lazima uongezee swali 'je, lugha zinazotumia kiingereza kama mother tongue, yaani lugha mama, kuna hao kina mama lishe?'. Kama jibu lako ni ndiyo, basi amini kuna neno hilo, lakini kama hapana, basi hakuna neno hilo. Na kama hakuna neno hilo, basi kuna wanaofanana kama mama lishe huko, hivyo wana majina yao. Ukishapata, hiyo itakuwa ni mfananisho tu (equivalent), na si maana sahihi unayoitaka. Nje kidogo na mama lishe, nikupe mfano mmoja wa nahau ya kiingereza na kiswaili ili unielewe nachokisema.

Wazungu wanasema, 'birds of feather flock together' kama nahau kwa maana ya kwamba, wanaofanana akili huungana mkono. Sasa, nahau kama hii, huwezi kuipata kwa maana ya moja kwa moja ya kiswahili, bali utatafuta nahau inayofanana maana na hiyo ili ufidishie. Mara nyingi Kiswahili tunasema, 'waarabu wa pemba hujuana kwa vilemba', na ndiyo maana sawa na birds of feather flock together.

Asante
fact!
 
Back
Top Bottom