Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 33,742
- 40,872
Wapo ndugu zetu kwa kisingizio cha "ubepari" wanataka tuamini kuwa katika Ubepari wafanyabiashara wana uhuru wa kufanya lolote, popote, vyovyote na bila matokeo yoyote (with impunity). Ndugu zetu hawa wanataka tuamini kuwa kwenye nchi ya kibepari wafanyabiashara kwa sababu ya kutaka faida wanaweza kubania bidhaa ili kusababisha ongezeko la mahitaji (demand) ili waweze kupandisha bei (price). Yaani, wafanyabiashara wazuie ugavi (supply) ili kuliendesha soko badala ya soko lenyewe kuamua nini kinahitajika na kwa bei gani.
Watetezi hawa wa ubepari uchwara wanataka tuamini kuwa kwenye nchi ya kibepari mfanyabiashara mkubwa (wholesaler) anaweza kuamua kununua bidhaa kutoka kwa mtengenezaji (manufacturer) halafu akaificha bidhaa hiyo ili kutokea uhaba (scarcity). Kwamba, kwenye nchi hizo za wenzetu serikali haziwezi kuingilia mipango hiyo kwa sababu ikiingilia hivyo itakuwa ni kama kuifanya serikali iwe ya kijamaa ambayo inasimamia shughuli za uzalishaji mali (means of production).
Ndugu zetu hawa ama hawajui Ubepari halisi ulivyo au hawajawahi kuchukua muda kujifunza nchi za Kibepari (za Kimagharibi) zimewahi kufanya nini katika kusababisha ugawaji wa bidhaa pale inapobidi. Nitatoa mifano michache hapa ili kuzima na kufutilia mbali hoja ya watetezi hawa wa Ubepari uchwara ambao Tanzania haijawahi kuwa mjengaji wake wala mwanafunzi wake mzuri!
1. Mwezi Mei 1942 wakati wa Vita ya Pili ya Dunia Ofisi ya Usimamizi wa Bei (Office of Price Administration) ya Marekani ilisimamisha bei ya karibu vitu vyote kwa sababu ya uhaba uliojitokeza. Vitu vya kwanza kupangiwa bei ilikuwa ni Sukari na Kahawa. Na kutoka hapo karibu vitu vyote vilikuwa vinanunuliwa kwa kiasi kilichopangwa na serikali kwa kila familia. Mtu hata kama alikuwa na uwezo wa kiasi gani hakuweza kununua zaidi ya alivyopangiwa; mafuta ya gari, n.k vyote vilisimamiwa na bodi karibu 8000 zilizoundwa nchi nzima kusimamia utaratibu huu wa ugavi.
Tanzania tulipoingia kwenye ugavi wa aina hii mwanzoni mwa miaka ya themanini tulifuata kwa kiasi kikubwa mfumo ule wa Marekani. Lengo lilikuwa ni lile lile kuwa katika hali hii ya uhaba basi kila mtu apate angalau sawasawa bila watu wenye uwezo sana wapate zaidi kwa sababu ya uwezo wao. Katika mazingira ya kuacha soko lijifanyie wenyewe ambao watadhurika zaidi ni maskini na watu wakipato cha chini kwani wenye uwezo nao wataweza kununua kiasi kikubwa na kuweka kwenye mojawapo ya vyumba vyao kwenye mahekalu yao!
Karatasi la Propaganda toka OPA
2. Waingereza wao walianza kufanya rationing (kusimamia ugavi wa bidhaa mbalimbali) tangu 1940. Wao walianza kusimamia vyakula kwa makundi matatu; kuanzia vile vya lazima - sukari n.k na vya msimu (mboga n.k) na vile ambavyo ni vya ziada. Lengo likiwa ni lile lile. Familia ziligawiwa coupons za kutumia kununua bidhaa mbalimbali. Hukuweza kununua zaidi ya kile ambacho coupon yako inakuruhusu kununua - hata kama unataka sana.
3. Baada ya Nchi za OPEC mwanzoni mwa miaka ya sabini kuweka mgomo wa kuuza mafuta; nchi za Magharibi (mabepari kweli kweli) walijikuta hawana jinsi isipokuwa kuingilia kati ugavi wa mafuta na kuweka utaratibu wa kugawa mafuta (rationing) ili kuhakikisha kuwa kila mtu anapata nafasi ya kupata mafuta kidogo.
Siyo kusudio langu kuzama katika mada hii na kuchambua kila kilichotokea na kama mazingira ya vita yanaendana na mazingira ya sasa au kama uamuzi wa sasa unafaa. Hadi hivi sasa bado serikali haijaanza kugawa au kuweka utaratibu wa kugawa bidhaa - hasa sukari. Kwa kiasi kikubwa hatujafikia huko na sidhani kama tutafikia huko kwani suala hili la kwetu ni suala la ndani (domestic issue) na ambalo haliendani na mambo yanayoendelea kimataifa.
Ukweli ni kuwa hata nchi za kibepari inapofikia wakati wa kulinda maslahi ya wananchi wao wengi wanasahau yote waliyojifunza kutoka kwa Adam Smith na kuwa wajamaa!