Neno la shukrani kwa Watanzania

Neno la shukrani kwa Watanzania

Tatizo wenzetu kifikra mmefikia `point of no return' kwamba hakuna wazo jingine jipya ambalo unaweza ingiza kichwani tofauti na unachokiamini!

Katika kipengere cha maazimio ya baraza kuu la chadema katika uzi wako umeviita `na mengineyo' hivyo ndivyo vilikuweka matatani. kwa sababu umefanya editing ya hayo maazimio basi ukubaliane na mimi kwamba umetambua kosa lako,

vinginevyo kama unamaanisha kile ulichokiandika basi hayo `mengineyo' yataje kama ulivyo yataja mwanzo ili sheria ichukue tena mkondo wake kwa kesi ya `kurudia kosa makusudi'
 
Huwa sionagi effects yako hata kwa sisimizi. Na sioni kama kuna mtu atakutafuta kwa unayofanya zaidi ya kukosea serikali kama vibaka wengine.
 
Utarudia tena kufanya uliyofanya au umekoma hurudii tena ili usisumbue familia yako na Chadema? Utarudia au hurudii?
ahaaaaaa narudi tena kwa kasi ya makinikia😀😀😀😀😀😀😀😀
 
Naungana nawe kulaani huyu MAAGZO TOKA JUU ashindwe na kulegea,

Mungu akulinde na kukupa afya, watz mamilion wanahitaji watu wakiwasemea
 
Vijana wa ccm mnafahamu kuwa kada mwenzenu Bolen Ngeti amekaa selo kwa siku zaidi ya 16 mpaka jana ijumaa alipotoka, kibaya zaidi hana mdaada wa kisheria wala wa chama chenu?

Endeleeni mkidhani ni Chadema tu ndio watakaoumia....
siasa hizi malipo ni hapa hapa duniani.....
 
Vijana wa ccm mnafahamu kuwa kada mwenzenu Bolen Ngeti amekaa selo kwa siku zaidi ya 16 mpaka jana ijumaa alipotoka, kibaya zaidi hana mdaada wa kisheria wala wa chama chenu?

Endeleeni mkidhani ni Chadema tu ndio watakaoumia....
Iache misukule isote na ijisoteshe kwa vile wao ni meno nje tu Nduhu tabbu
 
Ukweli siku zote husimama!!!! Haki hata binadamu akubanie! Mungu atatenda Haki daima
 
5472719_546619752197405218780avatar12342gif6ad642a37725e84edc6f827455c34a21gifacde8cf2e8b4eeea6ecd1a25a490fc67giff1ef2f77b40fa6df9fd4158bd7f00163_gife69cab1818e2d902ffda0835666b20a1
Kweli unene shidaaaa
 
Makamanda, ndugu jamaa na marafiki,

Kwa heshima zote naomba niwashukuru kwa kuwa nami katika kipindi kigumu nilichopitiana ninachoendelea kupitia hadi sasa,

Naishukuru familia yangu na naiomba radhi kwakuipitisha katika bonde hili la uvuli wa mauti, hii ndio njia tuliyopo na nilazima tufike tulipokusudia...

Kwa uzito usioelezeka, namshukuru sana wakili wangu msomi Mh Peter Kibatala na jopo zima la mawakili wenza, Nakishukuru chama changu cha Chadema chini ya Mwanasheria Mkuu ambae pia ni Rais wa TLS wakili msomi Mh Tundu Lissu,

Naishukuru serikali ya Chadema Dar chini ya Meya wa Jiji Mstahiki Isaya Mwita, Nalishukuru jopo la uongozi Chadema Kanda ya Pwani chini ya kamanda Mbusule C. Shillu
Afisa Oganizesheni na Uchaguzi Kanda ya Pwani, Naishukuru Chadema Wilaya ya Kigamboni chini Katibu wa Chama Kamanda Simon Magese, Nawashukuru madiwani wa Chadema Dar wakiongozwa na Mh Selestine Maufi Diwani wa Mjimwema Kigamboni, Diwani wa Mchikichini Ilala, Diwani viti Maalumu Kigamboni Mh Stela, Nawashukuru sana baraza la wazee Mbutu wakiongozwa na Mwenyekiti wa mtaa Mh Jamal Hassan Mfaume, mmekuwa silaha yangu na walezi imara katika kipindi chote.

Na mwisho nalishukuru jeshi la polisi na maafisa usalama wote waliotekeleza wajibu wao kwa mjibu wa sheria na miiko ya kijeshi, NINALAANI kwa nguvu zote MDUDU anayeitwa "MAAGIZO TOKA JUU", Huyu kwahakika anaichafua serikali ya rais wetu mpendwa Daktari John Joseph Pombe Magufuli kwakubaka haki za watu, tunayo sababu ya kumuomba rais wetu amshughulikie....

Nawashukuru watumishi na viongozi wa kiroho ambao kwa kila sekunde mnapaza sauti zenu mbele ya Mungu kuniombea, Lakini kubwa kuliko yote nawashukuru waandishi wa habari na wadau wote katika mitandao ya kijamii, Umoja na mshikamano mlionionyesha nawaomba usiishie kwangu tu, uendelee kwa wadau wote, mechi bado mbichi, imehamia mahakamani rasmi....

Sina neno linalojitosheleza katika shukrani hizi, zaidi ya kusema asanteni sana sana...

Niwahakikishie Mimi nipo imara kuliko nyakati zozote zile, Mimi na wenzangu hatutarudi nyuma katika kupigania mambo ya msingi katika taifa letu,

Tumedhamiria, na hili naomba niweke wazi, Azimio la Baraza Kuu Chadema la 27/5/2017 pale Dodoma lililotangazwa na Mwenyekiti was Chadema Taifa Kamanda wa Anga Mh Freeman Mbowe juu ya madai ya Katiba Mpya, Tume HURU ya Uchaguzi na mengineyo vitasimama kuwa ndio msimamo wangu na sitarudi nyuma kwa hofu ama ghiriba zozote, nitaishinda hofu kwa kuikabili USO kwa macho.

Na Yericko Nyerere
Acha kuandika habari za uongo zinazotokana na mawazo yako yanayo shabihiana na mapenzi yako kwa CDM.
Ieleweke wala huisaidii CDM kuandika habari za UONGO!
 
Back
Top Bottom