Neno la leo

Naona akaunti ya huyu mshikaji imekuwa hacked! Mods liangalieni hili sio kwa mahubiri haya..
 
Naona akaunti ya huyu mshikaji imekuwa hacked! Mods liangalieni hili sio kwa mahubiri haya..
Ikumbuke siku ya Bwana Mungu wako kuitakasa...unajua ni amri ya ngapi hii?
 
🙏
 
Aaah nyingine tunazitakasa wenyewe kuwa siyo dhambi maana ni hitaji la muhimu kabisa.
 
Siamini kabisa km Leo hii Mshana umetoa ujumbe huu,yaani nimesoma mara mbili mbili kuthibitisha km ndio Wewe Kweli?.Aisee Mungu akubariki Sana Mshana Jr.
 
Siamini kabisa km Leo hii Mshana umetoa ujumbe huu,yaani nimesoma mara mbili mbili kuthibitisha km ndio Wewe Kweli?.Aisee Mungu akubariki Sana Mshana Jr.
Ni mimi mwenyewe kabisa...Neno linasema ikumbuke siku ya Bwana Mungu wako UITAKASE... Naheshimu sana neno la Mungu
 
Nimelipenda neno lako na Mungu akubariki. ninasema Amen. Yesu amenichukulia dhambi zangu na sasa ninaimba Halleluya.

Isa 1:18 SUV​

Haya, njoni, tusemezane, asema BWANA. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
 


Sent using Jamii Forums mobile app
 
Sasa si aliuawa na Shetani bro yake!! kwa kuwatumia wanadamu hawahawa!! huyu!! huyu shetani ni ndugu yake waliwahi kuishi wote Mbinguni wakitanua kwenye Milki ya Bwana Mungu, wakati huo shetani akiitwa Lucifa. kawaida shetani anajua sana mitaa ya mbinguni!! !! kulivo!!!! tokea kiti cha enzi kilipo!! kimekaaje!! kuliko mimi na wewe!

Yesu na Shetani wanajuana wanapiga story sana tu!! rejea pale shetani alipo mwambia Yesu amsujudie!!! hata Mungu anapiga story sana na shetani kama pale..

Mungu alimuuliza ''shetani unatoka wapi???
shetani akajibu ''natoka kuzunguka huku na huko Duniani!!....''

Unaona sasa Mungu anaongea na kiumbe chake bila kinyongo!! but hajawahi kuongea na wewe!!

wanadamu mna wivu na chuki na kiumbe chake alikiumba kwa gharama kubwa kuliko nyie miudongo!!! Yesu si alijua atakufa? kwa nini aliuendea Msalaba?? na kuleta taharuki?? ili iweje yaani aliamua kuchezea muda??

km wachawi wanaweza chukua msukule na kuweka limgomba hapo! na watu mkaamini ndugu yenu kafa!! Yesu alishindwa nini kumuwekea shetani limgomba tu! na yey kasepa zake juu!!

Kwa nini Mungu asiseme tu Imekwisha!! na ikawa? km alivoumba mbingu na nchi? kwa jinsi tunavomsikia Mungu wa Ibrahimu!!!! Kashetani hako ni nusu dakika sifuri anakamaliza!! kwa nini Mungu anamuogopa shetani!!

Mna tugeuza juu chini chini juu!! kwa nini Mungu hakutaka tule matunda ya mti wa kujua mema na mabaya? je alikuwa mchoyo wa kutugawia maarifa?? Shetani yeye akatupatia kirahisi tu!! nani mzuri hapo anaekupa Elimu?? au anaekunyima elimu?? uendelee kuwa mjinga??? nani mbaya nani mzuri

Ni kwa vipi unaamini Mungu atamfutilia mbali mwanae mpendwa shetani wakati amemuumba kwa gharama kubwa??? wewe unadhani kwa nini Mungu amemuacha anapeta humu Duniani na huko ahera? ulisha wahi sikia anaumwa huyu shetani?? lkn wewe unakisukari ukizembea dawa wafwa!!

wanadamu wana roho mbaya wanafurahia shetani ateketezwe siku ya mwisho! shetani wa watu kajikalia kimyaaa!! anatafakari msivompenda. Mungu si mwanadamu anaweza msamehe shetani!! sijui mtajisikiaje watu ambao hamkufaudu leo!!

Mlioamini shetani wake ni moto tu!! yaani mnaweza nyie kufa kwa jinsi mlivo na roho zenu!!
 
AYUBU 36:21-22

²¹ Jitunze, usiutazame uovu; Kwani umeuchagua huo zaidi ya taabu.

²² Tazama, Mungu hutenda makuu kwa uweza wake; Ni nani afundishaye kama yeye?

HILO NDILO NENO LA MUNGU
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…