Neno la leo

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
269,633
697,791
KARIBU TUTAFAKARI PAMOJA NENO HILI

Watu wawili walikuwa wanakunywa pombe baa. Wakati wanakunywa wakaanza kubishana na baadaye ule ubishi ukawa ugomvi. Mmoja akamrukia mwenzake akaanza kumpiga. Baada ya kumpiga kwa muda mrefu akagundua kuwa mwenzake hapumui tena. Kumbe amemwua mwenzie.

Ndipo alipoanza kukimbia huku shati laki likiwa limechafuka sana na damu. Wale waliyokuwa wanauangalia ule ugomvi wakaanza kumfukuza. Huyu mwuaji akakimbilia kwenye nyumba ya mtu mmoja mcha Mungu na akamwomba yule mtu amfiche maana ameua mtu na watu walikuwa wanamfukuza. Yule mcha Mungu akasema nitakuficha wapi wakati mimi nina chumba kimoja tu?

Yule mwuaji akamjibu akamwambia acha kuendelea kupoteza wakati fikiria tu mahali pa kunificha. Yule mcha Mungu akavua shati lake safi akampa yule mwuaji alafu yeye akachukua lile shati la muaji lililojaa damu akalivaa. Akampa sharti yule mwuaji na kumwambia tunza shati langu usilichafue. Yule mcha Mungu alipofungua mlango wa chumba chake wale watu wakamvamia na kumpiga sana wakijua yeye ndo mwuaji huku mwuaji akiondoka salama na kurudi kwake.

Baada ya kumpiga sana yule ndugu akapelekwa polisi na baadaye akapelekwa mahakamani na akahukumiwa kunyongwa kwa kumwua mtu mwingine. Yule mwuaji halisi akiwa kule nyumbani alijisikia vibaya sana akaenda mahakamani akajisalimisha akasema yeye ndiye aliyeua, yule ndugu aachiwe huru. Hakimu akamwambia umechelewa, yule ndugu kesha nyongwa. Alilia sana na kujiambia kuwa yule mtu amekufa kwa kosa ambalo sio lake.

Akakumbuka maneno ya mwisho ya yule ndugu "LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE." Yesu alikufa kwa ajili ya dhambi zako na zangu. Alichukua vazi letu lililochafuliwa na uchafu wa dhambi zetu akatupa vazi Lake takatifu la haki. Yesu aliuawa kwa kosa lako na langu. Akatupa haki Yake na kutuambia tusichafue tena maisha yetu. Kuendelea kutenda dhambi baada ya yale ambayo Yesu ametufanyia ni kuidharau sana kazi ya msalaba na kuikanyagia chini Damu Yake ambayo tumesafishwa kwayo.

Ni kushindwa kuthamini kuwa kuna mtu alishakufa kwa ajili yetu. Ni kushindwa kutambua uthamani wa wokovu ambao tumeupokea. Tutapataje kupona tusipojali wokovu mkuu namna hii.

LITUNZE SHATI LANGU USILICHAFUE.
 
Ukiachana na neno hili zuri na muafaka kwa kipindi hiki cha wenzetu wakristo ambao wanatafakuri mateso ya bwana Yesu kristo na kufunga, Hujawai acha kunishangaza bwana Mshana Jr, Neno unalijua, uchawi na ndumba wazijua... hakika unajua kunichanganya ndugu yangu katika yote..
 
Ukiachana na neno hili zuri na muafaka kwa kipindi hiki cha wenzetu wakristo ambao wanatafakuri mateso ya bwana Yesu kristo na kufunga, Hujawai acha kunishangaza bwana Mshana Jr, Neno unalijua, uchawi na ndumba wazijua... hakika unajua kunichanganya ndugu yangu katika yote..
Mungu wetu ndio mwenye enzi yote na kwake kila goti litapigwa ...hakuna mtu awaye yote aliye mkuu kuliko yeye....
 
Malaika wako husimama mbele kidogo ya ule mstari wako wa kukata tamaa akisubiri uuvuke ili adhihirishe muujiza wa Mungu juu yako. Ukifika ile hatua ya kukata tamaa, usiachie hapo, tembea mbele tena kidogo ,🙏🏿🙏🏿
 
Malaika wako husimama mbele kidogo ya ule mstari wako wa kukata tamaa akisubiri uuvuke ili adhihirishe muujiza wa Mungu juu yako. Ukifika ile hatua ya kukata tamaa, usiachie hapo, tembea mbele tena kidogo ,
Nimebarikiwa na hili neno
 
Uliwah anzisha Uzi wa wanywa pombe na walevi
Nikisoma story yako nafahamu chanzo Cha yote ilitokana na pombe/ ulevi Hadi wakaanza kupigana

Pombe is too bad
Chini ya mbingu ya kaisari tunampa kaisari....Neno linatuasa tuwe na kiasi kwa kila jambo ...kwakuwa kuna matendo ya roho lakini pia kuna matendo ya mwili... Mungu akubariki Moniel
 
Jinsi ya kulitunza hilo shati lisichafuke ni shughuli pevu kwenye hii dunia iliyojaa vidimbwi vya tope na utelezi wa kutosha kazi ipo.
Mwambie huyo.. hapo bado hujakutana na pisi kali mtoto jicho jicho! Bado hujakutana na kale ka balimi a.k.a kaondoa seteresi..! Na dhambi zilivyo huwa zinaalikana ukianza unzinzi itamualika uongo! Ikija pombe itamleta uzinzi n.k..
Vidimbwi vingi sana..🤣
 
Mwambie huyo.. hapo bado hujakutana na pisi kali mtoto jicho jicho! Bado hujakutana na kale ka balimi a.k.a kaondoa seteresi..! Na dhambi zilivyo huwa zinaalikana ukianza unzinzi itamualika uongo! Ikija pombe itamleta uzinzi n.k..
Vidimbwi vingi sana..
Hili pepo ulilonalo likashindwe kwa jina la Yesu
 
Back
Top Bottom