Neno La Leo: ' Village Swaraj' | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: ' Village Swaraj'

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jun 6, 2011.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jun 6, 2011
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  “ Ukitaka kujua roho ya nchi, nenda kijijini”- Mahtma Ghandi. Na mwaka 2004 nilipata kumsikia mwandishi mahiri, Ngugi wa Thiong’o akitamka pale Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, kuwa; “ Ukitaka kujua nchi itakuwaje kesho, basi, waangalie vijana wake wa leo”.


  Katika kazi zangu nimepata bahati kubwa ya kutembelea vijiji vingi vya nchi hii. Hata jana jioni nilifika pale kijijini Tosamaganga. Ni umbali wa kilomita 14 hivi kutoka Iringa mjini. Nimeongea na vijana, na wazee pia. Kuna mengi ninayojifunza. Na picha nyingine zinatia huzuni, kama ya mama huyo pichani na mbwa wake. Kuna ombwe- Vacuum. Anasema maisha yamekuwa magumu sana kwake na familia yake.


  Na hakika tunafanya makosa makubwa, kudhani kuwa Watanzania wa vijijini bado wako usingizini. Hapana, Watanzania wameanza kuamka, hata vijijini. Na kama tungekuwa na mipango thabiti ya kuwekeza kwa Watanzania hawa wa vijijini, basi, tungepiga haraka hatua za maendeleo.


  Na waraka wa 23 wa Mtume Yohana una mapungufu, unatutaka tuwekeze kwa watu. Kwamba tupendane, tuheshimiane, tujaliane na mengineyo. Hilo ni jambo jema kwetu wanadamu. Lakini, na tujiulize. Inatosha tu kuwekeza kwa watu?


  Kuna mapungufu. Ni vema pia tukafikiri sasa, umuhimu wa kuwekeza kwenye akili za watu na baadae ikawa vitu. Tuwekeze kwenye exellency za watu wetu. Maana, watawala wetu hawawapendi watu wenye akili. Watu wenye kufikiri kwa bidii na hata kuhoji.


  Na ndio maana wakati mwingine, huwa ni faraja, kwa watawala, kuona watu wa vijijini wanabaki kuwa nyuma katika uelewa wa mambo. Hayo ni makosa makubwa. Tuanze sasa kufkiri katika ’ Village Swaraj’.


  Hii ni falsafa ya Mahtama Ghandi ambayo kimsingi imejikita katika kuwekeza kwenye akili za watu wa vijijini. Maana, vijiji ndio roho ya nchi. Na hilo ni Neno la Leo.
  Maggid,
  Iringa,
  Juni 6, 2011
  MJENGWA - Picha, Habari & Matangazo
   
Loading...