Neno La Leo: Unayemnyima Kisu, Mpe Banzi!

maggid

JF-Expert Member
Dec 3, 2006
1,084
1,246
Na Maggid Mjengwa,

WAHENGA walinena; ” Unayemnyima kisu, mpe banzi!”. Hizi ni kauli
zinazotutaka tufikiri kwa bidii. Kisu kilichotengenezwa kwa banzi ni mfano
wa kisu, si kisu. Wakati mwingine unafikiri, kuwa kuna Watanzania wanaoishi
mfano wa maisha. Katika maisha yangu ya kazi nimebahatika kutembelea maeneo
mengi ya vijijini. Huko nimeona changamoto za maendeleo. Nakumbuka sana
nilipokuwa kijiji cha Chipogoro, Dodoma. Pale nilimwona mama aliyekaa kwenye
mto uliokauka. Alikaa akichimba chini kutafuta maji.

Pichani ni kijijini Ubena Uzomozi, Pwani. Ni juzi tunilipita mahali hapo.
Picha hiyo inayoonyesha ombwe kuu. Katika nyumba hiyo ya mbavu za mbwa kuna
familia inaishi, japo upande mmoja umeporomoka. Baiskeli hiyo ni muhimu sana
kwa mwenye nayo. Na kuna tairi hapo. Ni kiti hicho, watu hukaa. Naam.
Unayemnyima kisu, mpe banzi! Hilo ni neno la leo.

Kwa kazi zaidi tembelea; http://mjengwa.blogspot.com/
http://www.kwanzajamii.com
 
Na hao ndo mtaji wa ccm kuendelea kutawala. Je kuna haja ya kuwahurumia??
 
Back
Top Bottom