Ndugu zangu,
Nimekuwa nikifuatilia hili tatizo la mihadarati kwenye jamii na tuhuma za kuhusika kwa baadhi ya wasanii wetu.
Kiukweli, juhudi za RC wa Dar, Paul Makonda katika kujaribu kupambana na tatizo husika ni za kuungwa mkono.
Ingawa hivyo, kuna changamoto katika vita hii, na andiko hili lichukuliwe kama nasaha kutoka kwa mtu mwenye umri wa kutosha na uzoefu wa kutosha wa masuala ya kijamii kuweza kuwa na maoni binafsi ambayo si lazima yafanane na ya mwenye kuyasoma.
Ndugu zangu,
Nikiwa kama mzazi pia, naguswa sana kila ninapoliona tatizo la matumizi mabaya ya madawa ya kulevya likiongezeka hapa nchini. Idadi ya vijana wetu wanaoangamia kwenye hili inaongezeka.
Jana nilimsikiliza Waziri Nape Nnauye. Kimsingi, naungana na Nape kwenye msogeleo wa tatizo/ Approach. Kwenye matatizo yao, hawa wasanii wetu, kuna umuhimu pia wa kuangalia leo na kesho yao katika kibarua chao kinachowafanya waishi.
Pale wanapotumbikia kwenye shimo la matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, tutafute namna ya kuwatoa shimoni kwa kuwapeleka Rehab, kama alivyoita Waziri Nape. Rehab kifupisho tu cha Rehabilitation kwa maana kupatiwa usaidizi wa kuondokana na tatizo. Hivyo, uwepo wa Rehabilitation Centres.
Anayetumia madawa ya kulevya kimsingi ni mgonjwa. Anahitaji msaada wa jamii atoke kwenye hali hiyo. Serikali nayo ina jukumu la kumsaidia raia kama huyu. Ni rahisi kuwaona baadhi ya wasanii tu kwa vile wana majina makubwa. Lakini, tatizo ni kubwa kwenye miji yetu. Inahitajika jitihada ya pamoja.
Walau, kwa mifano tunaweza kuona jinsi rehab zinavyoweza kuwatoa vijana wetu hawa wakarudi wapya kwenye jamii.
Kwa mfano, nimekuwa mpenzi wa msanii Ray C na tungo zake. Bahati mbaya sijapata kumuona akitumbuiza. Nakumbuka mwaka 2004 nikiwa Moshi Mjini nilisikia kuwa Ray C angetumbuiza kwenye moja ya kumbi maarufu za mji huo.
Nilikwenda ukumbini hapo usiku huo na kukaa mpaka saa saba usiku bila kumwona Ray C, kama ilivyonitokea kwa msaanii mwingine ninayependa tungo zake alipokuja Iringa, Lady Jay Dee.
Niliondoka pale ukumbini Moshi bila kumwona Ray C. Kesho yake nikaambiwa aliingia ukumbini saa nane za usiku. Hilo ni tatizo lingine la wasanii na hapa si mahali pake.
Alhamisi ya Juni 16, 2016, nilisoma gazetini kuwa Ray C alionekana usiku eneo la Manyanya, Kinondoni akiropoka hovyo na kuomba kisu ajiue. Polisi walimkamata na akafikishwa kwenye Rehab Centre.
Nilifarijika, Januari 30, kuona mitandaoni kuwa Ray C ametumbuiza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kule Dodoma.
Niliangalia video ile, yenye kumuonyesha Ray C, sio tu uwezo na kipaji chake cha muziki, bali kutufundisha, kuwa inawezekana kuwasaidia hawa wasanii wetu, kwa kuwapeleka Rehab.
Kisha wakarudi kwenye jamii na kuendelea na kazi yao ya kuwapatia kipato halali cha kuishi.
Imewezekana kwa Ray C, inawezakana kwa wasanii wengine na wanajamii wengine walio kwenye shimo la madawa ya kulevya.
Neno lile la Waziri Nape, ' Rehab', lituongoze pia katika kutafuta jawabu la tatizo husika.
Ukweli, wasanii hawa ni vijana wetu na tunawapenda kwa kazi zao njema.
- Tusiwaache Bila Sababu, Tuwatafutie Matabibu..
Na Video hii ya Ray C ni uthibitisho wa ukweli huu..
Maggid,
Iringa.