Ndugu zangu,
Mwanafalsafa John Rawls anasema; hata kama utakalo ni haki yako ya asili, lakini, kama hilo utakalo halina faida kwa walio wengi, basi, si haki yako kulifanya.
Katika nchi yenye raia wengi wenye kujitambua na kujivunia taifa lao, akitokea mmoja wao, tena mbaya zaidi kiongozi, akasimama hadharani kumdhalilisha kiongozi wao mkuu, tena wa kuchaguliwa, basi, raia hao husikitishwa na hata kufikia kumpuuza raia mwenzao huyo.
Watafanya hivyo kwa vile, hata kama mwenzao huyo alikuwa na haki ya kufanya alilotaka, lakini, kwa raia hao walio wengi, na kwa kuzingatia mila na desturi zao, nao watasikitishwa na kumpuuza mwezao huyo kwa vile takwa la mwenzao huyo halikuwa na faida ya walio wengi, na kwa taifa lao.
Mwanafalsafa mwingine, Benjamin Disraeli, huyu alipata kuwa Waziri Mkuu wa Uingereza, atakumbukwa kwa kauli yake ifuatayo;
" A good leader knows himself and the times". Kwamba kiongozi mzuri hujijua na hujua wakati unaomzunguka.
Na hapa kuna mfano wa kule Marekani, kwenye kuwania Urais kati yake na Obama. John McCain katika moja ya mikutano yake ya kampeni zake aliruhusu maswali kutoka kwa wapiga kura.
Wakatokea watu wawili waliokuwa na mitazamo hasi juu ya Obama.
Mmoja wa wawili wale alimwuliuza McCain kama Obama alikuwa Mwarabu na mwingine akatamka kuwa Obama ni gaidi.
McCain alitumia dakika kadhaa kuwatuliza wapiga kura wale kwa kuwaambia; kuwa Obama ni Mmarekani kama wengine, na kuwa Obama anaishi maisha adilifu ya ndoa na familia yake. McCain akazidi kuongeza, kuwa Obama angeweza kabisa kuwa Rais wa Marekani. Alichofanya McCain ni kumweka mpinzani wake Obama mahali pa salama, kwa maslahi ya Marekani, hata kama watu wale wawili walikuwa na haki ya kufanya walilotaka.
Maneno yale ya McCain yalidhihirisha ni kwa jinsi gain McCain alitanguliza utaifa kwanza na kuacha nyuma maslahi ya kisiasa. McCain aliona hatari iliyokuwepo ya kuruhusu fikra kama zile zenye kuchochea moto wa ubaguzi na kuufanya kupenya na kuota mizizi katika bongo za Wamarekani.
Alisimama pale kumtetea mpinzani wake kwa maana ya Obama, lakini kubwa kabisa, alisimama pale kuitetea misingi ya kidemokrasia ya taifa la Marekani.
Hapo McCain alikuwa ni kiongozi aliyejijua na aliyejua wakati unaomzunguka. Angetetea ujinga ule wa wapiga kura wale, basi, McCain angejivunjia hadhi na heshima yake mbele ya macho ya wengi. Historia ingemkumbuka kwa upuuzi wake huo.
Ndivyo inanavyotakiwa iwe. Na si kwa Marekani tu, hata huku kwetu. Katika nchi zetu hizi tuachane na siasa za misimu na kutanguliza maslahi binafsi na ya vikundi vya wachache.
Ni Neno La Leo.
Maggid Mjengwa.