Neno La Leo: Unapotongozwa Na Usiyemdhania, Jitathmini...

Platozoom,
Nakubaliana na mengi uliyoyaandikia, nyongeza hapa ni hii; hapa mtongozwaji kwa mara ya kwanza anakabiliwa na mazingira mapya katika kutongozwa kwake. Zamani aliweza ' kumdengulia' mtongazaji kama hakumpenda,lakini sasa mtongozwaji anaweza kujikuta anakosa mwana na maji ya moto. Na kuna maisha ya kisiasa ambayo mtongozwaji anayahitaji kuyaishi hata baada ya ' Vita ya leo'.
Maggid

Maggid umenichekesha: "kuyaishi maisha mapya"? Mimi nafikiri kwa kujali mustakabali wa yajayo ni vyema mtongozwa akajitathmini kwanza kama hayo maisha anayahitaji kwa ajili ya hatma yake au ni adabcadabra ama upepo tu unapita.

Na hata kama atagundua hayo ndiyo maisha anayohitajika kuyaishi ni vyema baada ya tathmini akayaweka kwenye mizania na mtazamo wake hata kama mwenye "dhana" ni mwingine, ili huko mbele y safari aseme naam nilifanya maamuzi yangu hata kama nimekosea, na najisahihisha (kumbuka mwalimu Nyerere aliandika tujisahihishe)
 
Mkuu yapo mambo mengi sana yamsingi wanayoyafuata wanaotongozwa au wanao tongoza,wapo wanaotongoza si kwakukupenda bali wametamani ulichonacho na kwakuwa hawawezi kusema wamekutamani au wametamani ulichonacho,nilazima waseme wamekupenda.2,wanao tongoza kwakupenda kwa dhati kutoka moyoni wao utanguliza utu na si kitu.Na katika siasa za kibongo wapo wanaokuja kwa sababu wamesikia unatoa kitu mfano pesa,khanga,kofia,wali,mahindi, nk.watakusanyika kwa wingi sana lkn si kwasababu wanakipenda chama chako bali wanafuta kile unacho kitoa.Na kunawengine hawatoi kitu lkn watu wana wapenda walivyo na umasikini wao.kumbuka KUPENDA au KUPENDWA nikipaji kutoka kwa mungu.
 
Platozoom, katika hilo, kuna jamaa yangu aliyekuwa ndani ya kikao cha Baraza la Vijana ( CCM) ameninong'oneza, kuwa Baraza La Vijana, CCM lililokutana Dodoma lilikuwa tulivu kupita yote aliyopata kuyashuhudia.
Riziwan awavuruga UVCCM Dodoma na mamilioni

Mtoto Rais Jakaya Kikwete, Riziwan, ambaye yupo Dodoma kuhudhuria vikao vya Kamati ya utekelezaji na Baraza kuu la vijana huko Dodoma amewavuruga vijana wenzake baada ya kuzidiwa hoja na vijana wengi nchi nzima kwenye vikao hivyo, sasa akaanza kutumia nguvu ya mamlaka/dola na mabilioni ya pesa ambayo amejitengenezea katika kipindi hiki cha Urais wa baba yake.


umesikika.
 
Maggid acha unafiki, tumekuchoka!
Na ukiona wana jf una wabore basi ujue hiyo ni dalili ya wewe kuishiwa na ukiona hatuchangii basi pia ujue hata wale wazamani nao pia wamekuchoka...tafakari na chukua hatua!!
 
Maggid acha unafiki, tumekuchoka!
Na ukiona wana jf una wabore basi ujue hiyo ni dalili ya wewe kuishiwa na ukiona hatuchangii basi pia ujue hata wale wazamani nao pia wamekuchoka...tafakari na chukua hatua!!

Akohi,

Kama umenichoka kwa nini unanifuata, threads ziko nyingi, yangu unaweza kuiacha tu. Ndio, ukiona wa zamani na wapya wanakutongoza, basi ujue umefanikiwa. Wewe hutaki kunikimbia, hunichukii, nami nakupenda pia!
Maggid
 
Siwezi poteza muda wangu kujadili utumbo wa uyu mnafiki...huo muda bora nile viroba nilichangie taifa kodi.

Nadhani pia uwezo wako wa kufikiri unaathiriwa na hivyo viroba-wee endelea kuvibugia tu, tuache tufuatilie mjadala; hata kama ni kimya kimya!
 
Hii nadhani inawahusu wanawake na mashoga, mi mwanaume na mambo ya kutongozwa wapi na wapi bwana Majjid? Aaaah, mi sichangi bana!
 
Akohi,

Kama umenichoka kwa nini unanifuata, threads ziko nyingi, yangu unaweza kuiacha tu. Ndio, ukiona wa zamani na wapya wanakutongoza, basi ujue umefanikiwa. Wewe hutaki kunikimbia, hunichukii, nami nakupenda pia!
Maggid

Hahaha ila jana umenifurahisha na nimeona umeanza kubadilika baada ya kumtembelea mjane, big up!!
 
Back
Top Bottom