Neno La Leo: Unapotongozwa Na Usiyemdhania, Jitathmini... | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Unapotongozwa Na Usiyemdhania, Jitathmini...

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Sep 16, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,

  Maishani wengi wetu tumetongozwa, iwe kwa mwanammke au mwanamme.

  Juzi hapa nikiwa kwa Bi Mkora pale Msamvu, akanilalamikia hili, kuwa siku hizi ameanza kutongozwa na hata ambao hakuwadhania.

  Ama , makubwa hayo. Lakini, akaniomba nimpe tafsiri ya jambo hilo.

  Nikamjibu, kuwa mwanadamu ukianza kuona unatongozwa na wale ambao hukuwadhania, basi, uanze kwanza kujitathmini, maana, kuna mawili;

  Ama, ulivyo sasa na mwenenendo wako, ikiwamo staili yako ya maisha, na hata mavazi yako, yamewafanya wale ambao hukuwadhania , kuanza sasa kukutongoza, au, kwa mabadiliko hayo, wale ambao walikuwa wakikutongoza zamani wameacha sasa kukutongoza, na kuwa sasa unatongozwa na wapya wenye kuvutiwa na mabadiliko hayo yenye kukuhusu wewe.

  Lililo jema kwa mwanadamu, ni kwa wale waliokuwa wakikutongoza zamani kuendelea kukutongoza, na juu ya hapo, ukapata watongozaji wapya. Hivyo, personal transformation ( Mabadiliko binafsi) uliyoyapitia yatakuwa yamefanikiwa.

  Na katika hili unaweza kuzama kifikra. Ukaangalia hata kwenye chama cha siasa. Kama chama cha siasa kitaanza kukimbiwa na wale waliokuwa wakikimbilia zamani, na kupata wakimbiliaji wapya, basi, hapo kuna tafsiri kama ya hapo juu. Nacho kitahitaji kujitathmini.

  Wajumbe nakaribisha hoja zenu...

  Maggid

  Iringa.
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 2. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #2
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,317
  Likes Received: 2,284
  Trophy Points: 280
  Tatizo lako tukianza mjadala hutaki kuchangia hoja...........mijadala mizuri kama hii inahitaji two way traffic
   
 3. King Kong III

  King Kong III JF-Expert Member

  #3
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 15, 2010
  Messages: 25,153
  Likes Received: 2,402
  Trophy Points: 280
  Kwahyo unaiambia nini ccm inavyokimbiwa na wanachama wake?
   
 4. Root

  Root JF-Expert Member

  #4
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 23, 2012
  Messages: 26,250
  Likes Received: 12,974
  Trophy Points: 280
  no comment in this
   
 5. m

  maggid Verified User

  #5
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Platozoom,

  Asante, changia hoja. Na kama kuna hoja ya kuchangia nitachangia, kama ninacho cha kuchangia, na kama sina si busara kuchangia hoja kwa vile tu kuna wengine wanaokutaka kuchangia. Na hoja zingine huchangiwa na wengine na mimi huzisoma na kuelimika nazo kama watembeleaji wengine. Na wakati mwingine ni rahisi kuchangia kama Platozoom maana si wengi wenye kumjua Platozoom ni nani. Hivyo, tofauti na tunaoingia humu na majina yetu halisi, Platozoom huenda usiwajibike kwa unachokiandika humu. Yaweza kuwa ukawa hata jirani yangu hapa Iringa. Ukanitukana humu asubuhi hii na mchana tukawa wote tunaongea kama majirani!
  Nashukuru sana kwa mchango wako.
  Maggid
   
 6. BelindaJacob

  BelindaJacob JF-Expert Member

  #6
  Sep 16, 2012
  Joined: Nov 24, 2008
  Messages: 6,060
  Likes Received: 475
  Trophy Points: 180
  Mweeh! jumapili maridadi kweli hii..
   
 7. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #7
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,317
  Likes Received: 2,284
  Trophy Points: 280
  Ni kweli si lazima kuchangia lakini kuna "circumstances" fulani fulani zinahitaji wewe kuchangia ili mjadala unyooke forgot wanaotukana kwa sababu tunaishi kwenye jamii inayojifunza kusimama. Ndiyo utawajibika kwa lile unaloandika kwani kuna ubaya gani............sidhani kama kuna ubaya kuwajibika kwa hilo labda kama una ajenda iliyojificha lakini kwa akina siye walala hoi ni wajibu kuwajibika kama si hapa basi hata huku uraiani.

  Na mama zetu walitufunza ukiwapikia watu chakula angalau uonje ama ule nao
   
 8. m

  maggid Verified User

  #8
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Platozoom,
  Asante sana. Nakubaliana nawe, kuwa kuna mazingira fulani mjadala unanihitaji nichangie ili unyooke, hata kama kwa kufanya hivyo kuna watakaopambana kuhakikisha unapinda-pinda, lakini, wenye kuelewa wataelewa.

  Nitajitahidi sana kufanya hivyo pale itapohitajika. Asante sana kwa ushauri wako.

  Maggid,
  Iringa.
  0788 111 765
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
 9. h

  hippocratessocrates JF-Expert Member

  #9
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 1, 2012
  Messages: 3,612
  Likes Received: 26
  Trophy Points: 135
  and this is the day we were waiting for, jukwaa la siasa kuvamiwa.
   
 10. AshaDii

  AshaDii Platinum Member

  #10
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 16, 2011
  Messages: 16,247
  Likes Received: 282
  Trophy Points: 180
  Kwa mtazamo wangu Majjid ukiona hata ambao walikuwa hawakutongozi wanakutongoza sio hayo mawili tu ulotaja inaweza kuwa kati ya haya:

  1. Uthamani wako umeonekana wazi kabisa baada ya wewe mwenyewe (ama kwa msaada wa mwengine) kuonesha wazi Uwezo/thamani na Utashu wa yalioyo ndani ya uhitaji na utakwa wa kundi hilo jipya la wakutongozao. Hapo wewe inabidi uchagu nini unataka ukijiuliza:

  - Hapo ulipo ni bora zaidi ama wewe utakua bora zaidi ukiwakubali hao wakutongozao? Kwa misingi ya vilivo msingi katika maisha yako.
  - Hao wanaokutongoza wanakutongoza kwa kuiga ama wanajua kweli kabisa Uwezo/Thamani na Utashu wako? Maana kama watongozaji hawajitambui linaweza kuwa janga kwako.
  - Wataongozaji wanakutaka wewe tu ama jamii yako nzima? Wanajua kupenda ua na boga? Maana unaweza ukatongozweka ukapata vitu flani flani ambavo vikaishia kwako tu, Ikawa haina maana kwa ndugu na jamaa waliokuzunguka. Haina maana.

  2. Inaweza pia kuwa ni sababu tu umeonesha dhahiri kuwa wewe ni fuata upepo. Na yeye niya ni kuonekana na wewe tu hana hasara kabisa kwa lolote litakalo kukuta ili mradi umkubalie takwa lake ambalo litamuunganisha kwa lile ambalo kalenga. Iwe Personally or Impersonally!
   
 11. m

  maggid Verified User

  #11
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Hippo,

  Ni kwa namna gani limevamiwa wakati kuna hoja ya msingi imewasilishwa na yenye kuhitaji mjadala? Au ndio unapiga king'ora cha Mod aifute thread hii na hivyo tunyimwe uhuru wa kujadili siasa hata katika hili!
   
 12. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #12
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,317
  Likes Received: 2,284
  Trophy Points: 280
  Asante.

  Back to the topic. Kwenye dhana ya kutongozwa kwa muktadha wa jamii na siasa zetu haitegemei mtongozwa kuonyesha mabadiliko hasi lakini pia inawezekana mazingira yanayomzunguka mtongoza na mtongozwa yamebadilika sana. Ule woga wa mtongoza umekwisha na sababu ni nyingi huenda ujasiri umempata, na hii inaweza kuwa kwa sababu ya suluba ama neema fulani aliyoipata ambayo kwa fikra zake inaweza kuwa kete muhimu ya mawindo yake.

  Lakini pia inawezekana kabisa mazingira yamembadilisha mtongozwa na kutizama nyuma na kuona pengine ile dhana ya kumkataa mtongoza hapo kabla haikuwa sawa na pengine ilikuwa ni hali ya kutokujua mambo tu.

  Kwa haya yote siye wengine tulio nje ya ulingo hao wawili ndio tunaweza kupima (kwa muono mbali) kama ni sawa movement anayoifanya mtongozwa au amemezwa na "pressure" za mtongoza na kushindwa kujizuia!
   
 13. PMNBuko

  PMNBuko JF-Expert Member

  #13
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 27, 2010
  Messages: 971
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wewe Maggid umeshatongozwa na CCM hadi unashindwa kuandika maovu yake. Ondoka hapa, umeshindwa hata kuweka makala ya kutetea haki za wanahabari?? Hata kile ulichoandika ulikuwa unauma na kupuliza CCM??
   
 14. K

  Keil JF-Expert Member

  #14
  Sep 16, 2012
  Joined: Jul 2, 2007
  Messages: 2,214
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Maggid,

  Kila siku unapoamua kurusha makombora kwa chama chako pendwa, huwa unapenda sana kutumia lugha ya mafumbo ambayo wakati mwingine wahusika huwa hawawezi kuambua kitu.

  Lakini kukiwa na swala ambalo linavihusu vyama fulani, huwa hutumii lugha ya mafumbo, bali huwa unapopoa kwa kutumia mawe ya nguvu na ujumbe huwafikia walengwa pasipo na shaka, yaani "bila chenga".

  Juzi nimesoma makala yako moja kuhusu uliyoyaona na kuyasikia hapo kijijini Nyololo. Mpaka mwisho wa makala ile sikuambua ujumbe wako zaidi ya kusema waandishi wanatakiwa waende hapo ili waweze kutafuta yaliyofichika ndani ya mioyo ya wana Nyololo. Wewe ukiwa mwalimu wa waandishi, ulishindwa nini kufanyia kazi hilo swala?

  Kutokana na makala zako pamoja na post zako hapa JF na kwenye blog yako, unawasaidia sana wale wa vyama fulani ambao huwa unawarushia makombora ya wazi huku ukiendelea kukibomoa chama chako pendwa kwa kuwa mafumbo yako hayakisaidii. Kisaidie chama chako pendwa kwa kukikosoa wazi ili siku moja waje wakukumbuke kwamba Maggid aliwahi kutuambia haya. Lakini kwa kutumia mafumbo yako ya mara mtoto wa Mfalme, mara sijui Ng'ombe kipofu na Ng'ombe kilema, hakuna anayekuelewa. Mkosoaji mzuri ni yule anayekosoa wazi wazi bila chenga.
   
 15. Nzenzu

  Nzenzu JF-Expert Member

  #15
  Sep 16, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 859
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Huyu jamaa kazidi hadithi na masimuliyi kama yale ya BABU KWA MJUKUU. Hii post TOA PELAKA JUKWAA LA MAHUSIANO!
   
 16. m

  maggid Verified User

  #16
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Platozoom, katika hilo, kuna jamaa yangu aliyekuwa ndani ya kikao cha Baraza la Vijana ( CCM) ameninong'oneza, kuwa Baraza La Vijana, CCM lililokutana Dodoma lilikuwa tulivu kupita yote aliyopata kuyashuhudia. Tunakuja kwenye hoja yako ya " Mazingira yanapombadilisha mtongozwa!"

  Mtoa habari wangu ameninong'oneza kuwa yeye kama mjumbe kuna wakati alisimama na kuwapinga wajumbe wawili wenye ushawishi na wenye kutoka kambi mbili tofauti za Urais ambao wote walisimama katika hoja moja na kujaribu kuitetea kikaoni. Jambo hilo hakulidhania kuwa lingetokea. Na hapa kuna nadharia ya familia yenye ugomvi inapomwona ' adui' akijiandaa kuvamia nyumba yao. Kuna mawili ya kuchagua; ama waendelee na ugomvi wao na kumwacha adui aingie , au wasimame pamoja kupambana na adui aliye nje. Na unafanyaje basi kama adui si ' upepo' unaopita tu? Wakati mwingine ni busara kumruhusu adui yako aingie kwenye hema lako na ' haja ndogo' aifanye kwa kutokea ndani ya hema kuelekeza nje ya hema, kuliko kumfanya adui abaki nje na ' kutiririsha' haja ndogo kupitia tundu za hema akiwa nje!
  Maggid
   
 17. D

  DT125 JF-Expert Member

  #17
  Sep 16, 2012
  Joined: Oct 19, 2011
  Messages: 203
  Likes Received: 40
  Trophy Points: 45
  Kukimbiwa kwaweza kusababishwaa na kuibuka kwa washindani wapya wakitumia mbinu mpya kwa kuelewa kwa kina udhaifu wako. Kukimbiwa si lazima kuwepo mabadiliko binafsi kwako.
   
 18. james chapacha

  james chapacha JF-Expert Member

  #18
  Sep 16, 2012
  Joined: Apr 3, 2012
  Messages: 942
  Likes Received: 19
  Trophy Points: 35
  Rudia kusoma utaelewa vizuri tu.
   
 19. platozoom

  platozoom JF-Expert Member

  #19
  Sep 16, 2012
  Joined: Jan 24, 2012
  Messages: 7,317
  Likes Received: 2,284
  Trophy Points: 280
  Nami Maggid niliyapata ya kikaoni kama wewe, ingawa kwangu mimi ilikuwa habari inakuja kwenye kijiwe cha mlalahoi (na hapa unajua huwa inakuja ikiwa mbichi haijatiwa chumvi, kwani mlalahoi ana madhara basi!!) na kwa bahati nzuri pia nipo Dodoma, ni kweli kuna dhana ya uadui iliingia kwenye vikao lakini katika angle tofauti kabisa.

  Labda tutazame hiyo dhana ya uadui (pasipo kutoka nje ya mada )imejengwa juu ya msingi gani: Je ni tofauti ya itikadi, mtazamo au "vuguvugu". Kama hayo ndiyo yaliyoleta changamoto basi ni jambo la kheri. Lakini kwa mtazamo wa haraka sidhani ni kwa ajili hiyo...........kama walipigana vita ni ile ya msimu wa maandalizi ya mavuno na pengine lilioleta mshikemshike ni juu ya mtoto wa bwana mkubwa kutaka kupanga safu.......na kama tunavyojua wakati mwingine watu wanachoka na kuamua liwalo na liwe...........Sasa tuseme hiyo ni hatua ya kupigiwa mfano? Au mtongozaji kachanga karata zake vizuri kugonganisha watu vichwa na mtongozwa kutojua? Tafakari.
   
 20. m

  maggid Verified User

  #20
  Sep 16, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Platozoom,
  Nakubaliana na mengi uliyoyaandikia, nyongeza hapa ni hii; hapa mtongozwaji kwa mara ya kwanza anakabiliwa na mazingira mapya katika kutongozwa kwake. Zamani aliweza ' kumdengulia' mtongazaji kama hakumpenda,lakini sasa mtongozwaji anaweza kujikuta anakosa mwana na maji ya moto. Na kuna maisha ya kisiasa ambayo mtongozwaji anayahitaji kuyaishi hata baada ya ' Vita ya leo'.
  Maggid
   
Loading...