Neno La Leo: Ngeleja's Last Dance!

Neno La Leo: Ngeleja's Last Dance!

maggid

JF-Expert Member
Joined
Dec 3, 2006
Posts
1,084
Reaction score
1,250
Ndugu zangu,

Leo nilipata tabu sana hata kunyanyuka kitini kwenda haja ndogo wakati mjadala wa ripoti ya Kamati Teule ya Nishati na Madini ukiendelea. Niliufuatilia tangu mwanzo hadi mwisho.

Na mchana huu nikawachukua wanangu kwenda kupata mahitaji sokoni. Njiani nilisimama kununua karanga za kukaanga. Mwuuza karanga ni msichana asiyezidi miaka 16. Nilimwona akiwa amekaa juani anauza karanga zake.

Pakiti ya karanga ni shilingi mia. Nikatoa noti ya shilingi mia tano kununua paketi tatu za karanga. Nilimwangalia msichana yule akihangaika na chenji ya shilingi mia mbili.

" Hapana, acha tu!" Nilimwambia.

Mmoja wa watoto wangu akaniambia; " Baba, nina shilingi mia mbili nyingine mfukoni, ngoja nimwongezee."

Msichana yule ikamchanganya. Akachukua karanga nyingine paketi nne anipe. Alidhani, kuwa nimebadili mawazo, kuwa ile mia mbili niliyomwachia na hii ya sasa tunataka karanga nyingine.

Akashangaa na kushukuru alipofahamu kuwa tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.

Niliondoka mahali pale nikitafakari sana juu ya umasikini wa watu wetu huku bado kumbukumbu ya mjadala wa bungeni leo Jumamosi ungali kichwani mwangu.

Nawafikria akina Ngeleja na Malima na ujasiri wao wa kifisadi wa kusaini malipo ya shilingi milioni nne kila mmoja kama ' Posho ya kukarimisha'. Nawafikiria akina Jairo na Luhanjo na ufisadi wa Wizara kuchangisha mamilioni ya shilingi na kupeleka watumishi zaidi ya mia mbili Dodoma kufanikisha uwasilishaji wa bajeti ya Wizara.

Maneno ya Mheshimiwa Lembeli yananijia; " Ndugu yangu Ngeleja jiuzuru!". Na hakika, wabunge wengi niliowasikia leo wamezungumza kwa uchungu juu ya kashfa na aibu hii kwa taifa akina akina Ngeleja na wenzake wametuletea.

Nawapongeza sana wabunge wetu kwa ujasiri waliouonyesha leo. Nami kama raia tu nasema; walichofanya akina Ngeleja na wenzake ni uhalifu na hakuna kingine cha wao kufanya sasa bali kuachia ngazi ili kulinda heshima zao, ya Rais na nchi yetu. Na juu ya hapo wafikishwe mahakamani.

Na kwa mtani wangu Ngeleja kama ni disco leo awe amecheza ' Last Dance!'. Kumwona Ngeleja Bunge lijalo akiwa kama Waziri si kingine bali ni matusi kwa WaTanzania.

Nahitimisha.

Maggid Mjengwa,
Iringa,
 
naona sisi tushazoea "kutukanwa". sitashangaa huyo ngeleja
kutocheza hiyo dansi ya mwisho na hakuna kitakachotekea
zaidi ya kupokea "matusi" mengine. inasikitisha sana. loh!
 
Nchi ya kitu kidogo hii ndugu Mjengwa.

Kushangaa mtashangaa sana lakini Ngeleja ataendelea kuwa waziri wa Nishati na madini.

Hii wizara ilimshinda siku nyingi, hata aliyemteua anajua, lakini kwa kuwa mawaziri wanawekwa strategically, Ngeleja yuko pale kwa sababu maalum anazozijua aliyemteua, angekuwa ni wa kuwajibika leo angetangaza kujiuzulu kwa jinsi wabunge walivyomkomalia.

Hata hivyo nani kasema Kujiuzulu na kufikishana mahakamani ni utamaduni wetu watanzania?
 
Hussein Mwinyi alisema hawezi kujiuzulu na bado hakujiuzulu,ngoja tuendelee kutukanwa Tanzania lakini..
 
Hussein Mwinyi alisema hawezi kujiuzulu na bado hakujiuzulu,ngoja tuendelee kutukanwa Tanzania lakini..

Hata Ngeleja alishakataa kujiuzulu na kudai tatizo la umeme yeye kalikuta na ni la Serikali yote. Na kwa kuwa anafahamu kwamba fisadi Rostam kamkingia kifua na fisadi Rostam kamuweka mfukoni Kikwete basi hana wasiwasi ataendelea kuwepo pale Nishati na Madini hadi 2015 labda kama Kikwete atabwaga manyanga.
 
Mjengwa ni wengi wametaka Ngeleja ajiuzulu lakini hebu ona unafiki wa Shelukindo yeye ndiye aliyewasilisha ile barua halafu leo hii anamkingia kifua asijiuzulu!!!!!
Ni unafiki huu utakampa nguvu Ngeleja asijiuzulu. Sitegemei miujiza mpaka hapa.
 
Nchi ya kitu kidogo hii ndugu Mjengwa.

Kushangaa mtashangaa sana lakini Ngeleja ataendelea kuwa waziri wa Nishati na madini.

Hii wizara ilimshinda siku nyingi, hata aliyemteua anajua, lakini kwa kuwa mawaziri wanawekwa strategically, Ngeleja yuko pale kwa sababu maalum anazozijua aliyemteua, angekuwa ni wa kuwajibika leo angetangaza kujiuzulu kwa jinsi wabunge walivyomkomalia.

Hata hivyo nani kasema Kujiuzulu na kufikishana mahakamani ni utamaduni wetu watanzania?

No one will ever try to resign from this Government! Instead they say they are fighting from within............and the big reason is that political seat in Tanzania is so sweet it comes with goods in handy.....i.e free top range cars, drivers, bodyguards and then for the corrupt minded its an highway to their corrupt practices. So instead of choosing to use his own car, fuel, driver, wear and tear on Tanzanian roads they prefer to hang on and keep complaining through public (media), unnecessary press conferences etc. All this makes them say i better from within........anyway that is our Tanzania, shamba la bibi.
 
Haah! kumbe ni Mggid Mjengwa, napita tu hapa hapanifai. ile bahasha yako waliokupa wakati wa uchaguzi mkuu mwaka jana imekwisha ? naona unaanza kuonea gere ulaji wa wenzako.
 
:eyebrows: mimi nimwanaCCM lakini katika hili kama ngeleja hatajiuzulu,ntaihama hiki chama rasmi na ntamtukana waziwazi.
 
Ndugu yangu Mjengwa, Narudia tena dharau ya ccm na viongozi wake kwa watanzania ni hali ya juu kiasi kwamba hakuna wa kujiuzuru ndugu zangu hawana aibu tena wala nini wao wameamua kula nchi kuponda mali za maskini bila aibu so sitajii yeyote kujiuzuru sana sana natarajia Jairo kurejea ofisini soo.
 
...alipofahamu kuwa tumenunua karanga za shilingi mia tatu na tumemwachia shilingi mia nne abaki nazo.

Maggid Mjengwa,
Iringa,
Novemba 19, 2011
Umemwachia mia nne abaki nazo, na umenunua karanga za mia tatu.

Kwa hiyo umetoa tip ya shilingi mia. Sio mbaya, ubarikiwe. Lakini tip ya shilingi mia sio ya kuianzishia thread!
 
Umemwachia mia nne abaki nazo, na umenunua karanga za mia tatu.

Kwa hiyo umetoa tip ya shilingi mia. Sio mbaya, ubarikiwe. Lakini tip ya shilingi mia sio ya kuianzishia thread!
Nilikuwa nafanya utafiti ni kwa nini division zero zimekuwa nyingi siku hizi, kumbe hata hapa JF wapo zero brain wengi, kwahiyo mia2 + mia2= mia1!?
 
Tanzania yetu amani, hivi vingine vya kujiuzuru siyo desturi yetu.
 
Last dance ya Ngeleja inaletwa na muuza karanga?.
 
Sasa ndo nimejua kuwa wapotoshaji wa umma wako serikalini. Katibu mkuu kiongozi ameupotosha umma.

Control and Auditor General, amechafuka. Wabunge walitakiwa waairishe National Board of Accountants and Auditors (NBAA) Kumchunguza bwana Utoh, kwa kukiuka maadili ya NBAA. Nawakijiridhisha, ni lazima afutiwe usajili wake kwani alichofanya ni ufisadi na amedhalilisha taaluma. Shame on him
 
Umemwachia mia nne abaki nazo, na umenunua karanga za mia tatu.

Kwa hiyo umetoa tip ya shilingi mia. Sio mbaya, ubarikiwe. Lakini tip ya shilingi mia sio ya kuianzishia thread!
embu jaribu ku-spare hata dakika moja kusoma main post kabla ya kukurupuka watu wengine bwana.
 
Last dance ya Ngeleja inaletwa na muuza karanga?.
jamani mtoa thread katoa ujumbe kwa mtiririko wa hadithi ya ukweli aliyoiona ukicompare maisha ya kimaskini ya binti muuza karanga na wa akina Jairo na Kafumu(both under Ngeleja Roof) wanaopokea posho ndefundefu kwa siku
 
Back
Top Bottom