Neno La Leo: Nape, Ray C Na Rehab...

Neno La Leo: Nape, Ray C Na Rehab...

rehab kwa watumiaji wa madawa ni mwafaka ktk jamii yetu. lakini wauzaji, wasafirirhaji na mapapa wafadhili au wamiliki wa biashara hii, mahali pao salama ni jela, tena kifungo maisha.
 
Katika hili, utaona kuna tatizo kubwa sana la namna gani mapambano yanaendeshwa

Nakubaliana na Nape kuhusu tuhuma, sikubaliani na suala la Rehab
Siyo kwamba sikubali rehab, ninachokataa ni kutoa rehab kama kipaumbele

Kipaumbele ni kuhakikisha hakuna supply ya madawa kwanza, halafu walioathirika wafanyiwe rehab. Kwa maneno mengine tunatatua tatizo halafu tunakarabati

Sasa Makonda anakamata watumiaji akidhani anaweza kupambana na 'suppliers'
Hawa ni watu ambao majina yao yalitua Ikulu hakuna kilichofanyika

Kinachoendelea ni kuaminisha umma wasanii ndio tatizo. Hili tu ni tatizo

Vita hii inahitaji akili na maarifa si harakati na stunt. Failure is imminent
 
Ndugu zangu,

Nimekuwa nikifuatilia hili tatizo la mihadarati kwenye jamii na tuhuma za kuhusika kwa baadhi ya wasanii wetu.

Kiukweli, juhudi za RC wa Dar, Paul Makonda katika kujaribu kupambana na tatizo husika ni za kuungwa mkono.

Ingawa hivyo, kuna changamoto katika vita hii, na andiko hili lichukuliwe kama nasaha kutoka kwa mtu mwenye umri wa kutosha na uzoefu wa kutosha wa masuala ya kijamii kuweza kuwa na maoni binafsi ambayo si lazima yafanane na ya mwenye kuyasoma.

Ndugu zangu,

Nikiwa kama mzazi pia, naguswa sana kila ninapoliona tatizo la matumizi mabaya ya madawa ya kulevya likiongezeka hapa nchini. Idadi ya vijana wetu wanaoangamia kwenye hili inaongezeka.

Jana nilimsikiliza Waziri Nape Nnauye. Kimsingi, naungana na Nape kwenye msogeleo wa tatizo/ Approach. Kwenye matatizo yao, hawa wasanii wetu, kuna umuhimu pia wa kuangalia leo na kesho yao katika kibarua chao kinachowafanya waishi.
Wasanii kwa vile wana jina wapelekwe rehab? Na watoto wetu wasiokuwa na majina Lupango? Kutumia dawa za kulevya ni kosa la kijinai so kama ni kweli sheria ichukue mkondo wake. Baada ya hapo wafikiriwe rehab.
Pale wanapotumbikia kwenye shimo la matumizi mabaya ya madawa ya kulevya, tutafute namna ya kuwatoa shimoni kwa kuwapeleka Rehab, kama alivyoita Waziri Nape. Rehab kifupisho tu cha Rehabilitation kwa maana kupatiwa usaidizi wa kuondokana na tatizo. Hivyo, uwepo wa Rehabilitation Centres.

Anayetumia madawa ya kulevya kimsingi ni mgonjwa. Anahitaji msaada wa jamii atoke kwenye hali hiyo. Serikali nayo ina jukumu la kumsaidia raia kama huyu. Ni rahisi kuwaona baadhi ya wasanii tu kwa vile wana majina makubwa. Lakini, tatizo ni kubwa kwenye miji yetu. Inahitajika jitihada ya pamoja.

Walau, kwa mifano tunaweza kuona jinsi rehab zinavyoweza kuwatoa vijana wetu hawa wakarudi wapya kwenye jamii.

Kwa mfano, nimekuwa mpenzi wa msanii Ray C na tungo zake. Bahati mbaya sijapata kumuona akitumbuiza. Nakumbuka mwaka 2004 nikiwa Moshi Mjini nilisikia kuwa Ray C angetumbuiza kwenye moja ya kumbi maarufu za mji huo.

Nilikwenda ukumbini hapo usiku huo na kukaa mpaka saa saba usiku bila kumwona Ray C, kama ilivyonitokea kwa msaanii mwingine ninayependa tungo zake alipokuja Iringa, Lady Jay Dee.
Niliondoka pale ukumbini Moshi bila kumwona Ray C. Kesho yake nikaambiwa aliingia ukumbini saa nane za usiku. Hilo ni tatizo lingine la wasanii na hapa si mahali pake.

Alhamisi ya Juni 16, 2016, nilisoma gazetini kuwa Ray C alionekana usiku eneo la Manyanya, Kinondoni akiropoka hovyo na kuomba kisu ajiue. Polisi walimkamata na akafikishwa kwenye Rehab Centre.

Nilifarijika, Januari 30, kuona mitandaoni kuwa Ray C ametumbuiza mbele ya Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa kule Dodoma.
Niliangalia video ile, yenye kumuonyesha Ray C, sio tu uwezo na kipaji chake cha muziki, bali kutufundisha, kuwa inawezekana kuwasaidia hawa wasanii wetu, kwa kuwapeleka Rehab.

Kisha wakarudi kwenye jamii na kuendelea na kazi yao ya kuwapatia kipato halali cha kuishi.

Imewezekana kwa Ray C, inawezakana kwa wasanii wengine na wanajamii wengine walio kwenye shimo la madawa ya kulevya.

Neno lile la Waziri Nape, ' Rehab', lituongoze pia katika kutafuta jawabu la tatizo husika.

Ukweli, wasanii hawa ni vijana wetu na tunawapenda kwa kazi zao njema.

- Tusiwaache Bila Sababu, Tuwatafutie Matabibu..

Na Video hii ya Ray C ni uthibitisho wa ukweli huu..

Maggid,

Iringa.

Kwa vile ni wasanii na wana majina makubwa wapelekwe rehab? Watoto wetu wasiokuwa na majina lupango? Kutumia dawa za kulevya ni kosa la jinai. kama ikithibitika ni kweli sheria ichukue mkondo wake bila kuangalia sura au cheo cha mtu. Dawa za kulevya ni janga la kimataifa. Kuacha kundi fulani litumie tu eti kwa vile ni wasanii si sawa.
 
Nguto, asante, huenda hukusoma kipande hiki nilichokiandika...
"Imewezekana kwa Ray C, inawezakana kwa wasanii wengine na wanajamii wengine walio kwenye shimo la madawa ya kulevya."
 
Ok mkuu!!!!
 
maggid
Nimeeleza mahali sote tunaguswa na tatizo. Hakuna asiyetaka kuona lina koma

Tofauti uliyosema ndiyo wengi hawaelewi.
Approach lazima iwe ya weledi, maarifa na endelevu. Siyo harakati

Ukimtuhumu mtu na kushindwa kuthibitisha utakuwa umemharibia maisha

Tuhuma hazifanyi mhusika awe na kosa, ni hadi ushahidi usio na mashaka utakapothibitishwa na chombo cha sheria.

Lakini tuhuma zina madhara kama hazina ithibati, ndipo ninapoona tatizo

Pili, vita inaweza kutumiwa vibaya kwa kukomoana. Kwamba, mtu anasingiziwa anauza madawa kwa tuhuma tu na kwavile ni mapambano basi anawekwa rumande

Tumeona neno 'uchochezi' linavyotumika kuhukumu watu ktaika mazingira tata

Nakumbuka lile sakata la Polisi waliotuhumiwa 'Kumbambikia' mtoto wa Mengi madawa

Najiuliza kuliacha suala hili kama lilivyo, wengi wataonewa bila sababu

Kutoa nguvu na mamlaka tu bila kuzingatia sheria ni makosa

Kwa nchi za wenzetu kumtuhumu mtu bila ushahidi ni 'defamation' na tungelikuwa tunafuata sheria serikali ingeishia kulipa watu fidia za mabilioni

Tufanye mambo kwa weledi ndiyo maana naungana na Nape kwa hili wazi kabisa

Tayari kuna stigma wasanii ndio watumiaji. Hili tu linawakwaza baadhi na litawakwaza wengi maana msanii kutoka Tz akienda popote duniani, ni mtuhumiwa tayari

Mtu anaweza kukamatwa tu kwa kisingizo cha madawa kwasababu ni mapambano
Mtu katoka safari anaweza kamatwa airport kwasababu tu anatuhumiwa

Tunaweza kupigana vita kwa akili kuliko maguvu na hapo ndipo ushindi ulipo

Kwa haya ninayoona, sitegemei jipya.
Bandiko hilo tuliweka siku chache zilizopita

Lengo lilikuwa kuonyesha kuwa hii vita inayopiganwa bila utaratibu tutaishia kubaya

Hivi kweli hakuna taratibu za kushughulikia matatizo sasa hivi ni RC kusimama na kutoa tuhuma tu zisizo na uthibitisho

Angalia defamation inayoendelea halafu ujiulize wewe 'ngurumbili' si unaweza kuitwa ukapigwa picha umebeba mzigo usioujua!

Jamani, lazima tuwe na taratibu za kushughulikia haya mambo

Madawa ni tatizo na ni vita ya kila mmoja, tofauti ni jinsi gani watu wanapambana

Lilianza na wasanii, sasa wanasiasa, halafu ukiwa na kajumba kazuri tayari ni mtuhumiwa. sijui linaelekea wapi

Hili si suala la mchezo kama tutalifanyia utani.
 
Back
Top Bottom