Neno La Leo: Miaka 50 Ya Uhuru Na Ugali Ni Ule Ule, Kwanini? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno La Leo: Miaka 50 Ya Uhuru Na Ugali Ni Ule Ule, Kwanini?

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by maggid, Jan 9, 2012.

 1. m

  maggid Verified User

  #1
  Jan 9, 2012
  Joined: Dec 3, 2006
  Messages: 1,084
  Likes Received: 397
  Trophy Points: 180
  Ndugu zangu,


  Nimetafakari sana na kujiuliza; kwanini hata katika miaka 50 ya uhuru wetu hatujaweza kubadilisha hata ladha ya ugali tunaokula?


  Ndio, miaka 50 ya Uhuru na ugali ni ule ule. Hatujaongeza ubora wa ugali wala wingi wake kwenye sahani. Kama jana kama leo, tunachemsha maji, tunaweka unga na kisha tunasonga. Ni vile vile, tunasonga ugali kwa mazoea. Hivi, hatuwezi kuukamulia ndimu au limau ugali tunaousonga?

  Ni swali linalokutaka ufikiri kwa bidii. Maana, kama tunaweza kunywa uji wa ndimu au limau kwanini tusiweze kula ugali wa ndimu au limau? Naam, ndimu inaweza kuchangamsha ugali tunaokula.


  Na kama tunaweza kunywa uji wa chenga kwanini tusianze kusonga ugali wa chenga? Na ugali wa chenga ukikamuliwa ndimu au limau unaweza kuwa mtamu haswa.


  Ndugu zangu,

  Tunahitaji mabadiliko.
  Tumekuwa ni watu wa kuogopa mabadiliko. Ni watu tulioridhika na ugali ule ule, miaka nenda miaka rudi. Kwanini? Tumekuwa kama watu wa Taifa la Kusadikika. Maana, mwandishi yule mahiri, Mtanzania mwenzetu Shaaban Robert anaandika; ” Wasadikika wana desturi ya kutafuta fimbo baada ya kuumwa na nyoka. Tumekwisha umwa na nyoka wa matendo yetu mabaya ya zamani.


  Nyoka mwenyewe amekwishakimbia. Hapatikani kwa kujilipiza kisasi, lakini, sumu yake imebakia katika jeraha tulilolipata. Sasa, shauri lililo jema ni kuzuia sumu hii isienee miilini mwetu ikaleta kifo.

  Maovu yana hatari kubwa kukaa kati yetu. Tumedumu nayo kwa muda mrefu. Hayakutuletea faida ila hasara, huzuni na kilio siku zote.”- Shaaban Bin Robert.

  Naam, na Shaaaban Robert naye alitutaka tubadilike, miaka 50 iliyopita!


  Maggid Mjengwa,

  Iringa
  Januari 9, 2012
  Mjengwa Blog::Habari,Picha,Matangazo
   
Loading...