Neno la Kuudhi: Hakuna Haki ya Kikatiba ya Kuonwa "Live"

Nililisema hili wakati ule wa mjadala huu na narudia tu; hakuna haki ya Kikatiba ya watu au watendaji wa umma kuonwa "live" kwenye luninga au kusikilizwa radioni. Katiba haitambui wala kuilinda haki hii.
na ile transparency (uwaz) unadhan nn kama sio haki ya kikatiba ya bunge kuonwa live? Alaf amtak muonwe live kwasabab gan, tht means mnafanya mambo ambayo siyo kwaio mnaogopa kuonekana. yan wananch wa nje hatujui knachoendelea ndan
 
Huko uliko ukishazidi miaka 60 unapelekwa nyumba za wazee na kufugwa na kupewa kila kitu bure, kazi yako kuletewa magazeti na kuangalia Tv bure. Leo unadanganya wazee wenzako. Mzee sa hizi kambini kwa sababu ya kukimbia shida zetu
 
Hili likiendekezwa litatoa njia kwa shughuli nyingine pia kutakiwa kuonyeshwa live. Kwa mfano hukumu zikiendeshwa, matatibu wakitibu au kufanya upasuaji, wahandisi wakitekeleza mirado etc. Ndugu wananchi tufanye kazi, kwa nini tunashinikiza kuwaona wawakilishi wetu wakituwakilisha live muda wa kazi?
 
Nililisema hili wakati ule wa mjadala huu na narudia tu; hakuna haki ya Kikatiba ya watu au watendaji wa umma kuonwa "live" kwenye luninga au kusikilizwa radioni. Katiba haitambui wala kuilinda haki hii.
Mkuu Mzee Mwanakijiji, kwanza naungana na wewe kuwa uko right, hakuna mahali popote katika katiba yetu, haki hiyo imeandikwa!. Katiba yetu ni ni ya mwaka 1977, na tuliipitisha mwaka mmoja tuu baada ya Newspaper Act ya mwaka 1976, hivyo muda huo hatukuwa na TV, redio ilikuwa moja tuu RTD, hivyo kitu kinachotambuliwa vizuri ni gazeti. Sisi Tanzania bado hatuna kitu kinachoitwa "freedom of information act", yaani hatuna haki ya kupata habari, na hizi habari zote tunazopata ni just a favor tuu, tatizo kubwa ni watu wakiishapata favour, na kuizoea hiyo favor, then wanaigeuza hiyo favor is right na kufikia kuidai, hivyo Mkuu Mzee Mwanakijiji, you are very right on this!

Sasa tuko kwenye zama zingine, hizi ni zama za information age, good governance, transparency na human rights, miongoni mwa haki za msingi, ni haki ya kupata habari, hivyo Mtanzania kupata habari sasa sio favour tena, ni haki, na akikosa habari fulani, ana haki kuidai habari hiyo ndio maana mpaka leo tunaipigania ile miswada miwili ya Media Services Bill na the Access to Information Bill, iletwe .

Serikali yetu imezoea vya kunyonga, hivyo hivi vya kuchinja hatuviwezi!, na kitendo cha Watanzania kulishwa nyama iliyochinjwa rasmi, kisha ukawaletea vile vile vya kunyonga, lazima watakataa, ndio maana kuna wengi watakupiga pale unapowaambia ukweli ambao hawapendi kuusikia!, sisi wengine tukisema serikali yetu hii ya CCM ni seikali dhalimu, tutaambia tunamchukia eti kwa vile tuliyemyaka siye!.

Endelea na kazi hii nzuri ya uelimishaji saidizi, tutafika tuu.
Pasco
 
Ukishangaa ya CCM, utastaajabu ya Watanzania... Naona kujipendekeza ndo SI unit ya kupata ulaji!!
Mzee kaza buti!! Ongeza idadi ya posts mwezako Slow slow alikuwa hata radhi kupiga deki studio ili apewe airtime star tv na chanel 10
 
Nililisema hili wakati ule wa mjadala huu na narudia tu; hakuna haki ya Kikatiba ya watu au watendaji wa umma kuonwa "live" kwenye luninga au kusikilizwa radioni. Katiba haitambui wala kuilinda haki hii.
Wewe unapaswa ukapimwe.""
Nini maana ya uhuru wa havbari na vyombo vya habari?? Kwenye utumbuaji wa majipu sehemu inayoonekana ni ya kupata sifa inaonekana.
Lakini kwenye SALATANI YA INI amvapo ni hatari mno na ambapo watanzania wanaona mapungufu na utofauti wa serikali na bunge ndio mnaona hakuna haki a kuonwa live??

Kiukweli nilishasema hivi;
"" IKITOKEA MKASIKIA NA KUDHITISHA KUA NIMEKUBALIANA NA HILI SWALA LA BUNGE KUTOONYESHWA LIVE,, NIKAMATENI NIKAPIMWE AKILI YANGU NA MSISIKIE LOLOTE WAKATI NAJITETEA ITAKUA NDOO ZINALIZIKIA AKILI ZANGU KULUKA CHONDE MNIWAHISHE SEHEMU YOYOTE NIPATE MSAADA WA AKIL""
 
Hili likiendekezwa litatoa njia kwa shughuli nyingine pia kutakiwa kuonwa live. Kwa mfano hukumu zikiendeshwa, matatibu wakitibu au kufanya upasuaji etc. Ndugu wananchi tufanye kazi, kwa nini tunashinikiza kuwaona wawakilishi wetu wakituwakilisha live muda wa kazi?
Madam unaishi dunia gani? Hivi mnadiriki kujitoa ufahamu kiasi hivyo!! Oooh. Ktk dunia hii he utandawazi kuna kipi kisicho live. Je yale majipu yanayotumbuliwa live JPM amevunja katiba? Mpe MM salam kuwa na yeye hatachaguliwa ukuu wa wilaya live.
 
Hili likiendekezwa litatoa njia kwa shughuli nyingine pia kutakiwa kuonyeshwa live. Kwa mfano hukumu zikiendeshwa, matatibu wakitibu au kufanya upasuaji, wahandisi wakitekeleza mirado etc. Ndugu wananchi tufanye kazi, kwa nini tunashinikiza kuwaona wawakilishi wetu wakituwakilisha live muda wa kazi?
Wabunge wanatuwakilisha. Tunataka kuona na kusikia wanatuwakishaje. Wengine uliowataja wameajiriwa na sekta/idara husika. Wabunge tumewaajiri. Tunataka tuuone utendaji wao wa kazi.
Kuonyesha matukio ya bungeni usiku ni kuwachosha wananchi na kusababisha ufanisi wa kazi kushuka. Aidha wapo wanaingia shift za usiku. Je, hao nao mtawasaidiaje ili wafanye kazi zao huku wakipata habari za bunge?
Rusheni matangazo hayo.
 
Back
Top Bottom