Neno la faraja

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
10,757
18,594
Najua sote tuna mategemeo ya kuishi maisha bora, tunajituma ama kujitoa kwa kila namna, kwa nafasi zetu na viwango vyetu vya elimu na mafunzo ya aina mbali mbali.

Furaha yetu imezidi kutukimbia na kutuacha wapweke na waliokata tamaa, tumefika mahali tukajikuta yote tuliyoyawaza kuwa tukiyapata leo basi tutaishi kwa raha na matumaini makubwa sana.

Tafakari yafuatayo:-

1. Wasio na ajira, wanatamani.sana kupata ajira ili walau wapate ujira wa kuwawezesha kujikimu. Walioajiriwa wanalalamika ujira mdogo na haukidhi mahitaji na wengine wakitamani kuacha kazi.

2. Tunawatamani sana matajiri walio na majumba makubwa na magari ya thamani kubwa, lakini hatujui kuwa hawahawa matajiri baadhi yao hawana raha kutokana na madeni ya mabilioni wanayodaiwa.

3. Tumejikuta hatuna raha sababu ya migogoro ya ndoa zetu na mahusiano lakini wengine ndio wapo.katika furaha ya ndoa na mahusiano.

4. Wengine wana magonjwa yasiyopona kama UKIMWI, wanatamani sana ingewezekana warudi zamani ambapo hawakuwa na magonjwa hayo lakini haitawezekana kimwili bali kiroho tu.

5. Tumeteketeza mamilioni ya fedha katika starehe tukidhani tunayafaidi maisha, lakini leo hii tumerudi kuwa vibarua na watu walipoteza matumaini ya kupata tena.

6. Tumeweka matumaini kwa wanasiasa tukiamini kuwa sera na maono yao yatatupa furaha na ustawi mwema maishani.

Faraja ni kuwa:-
* Hakuna jipya hapa duniani, tupo leo lakini miaka 50 ijayo wengi mnaousoma uzi huu ikiwemo mimi inawezekana tusiwepo tena duniani, basi ya nini kujisumbua na kuumia kwa haya yapitayo?

Sishauri tusihangaikie maisha haya ya kupita, ila tusiuache utu wetu kwa kuangalia manufaa ya maisha yetu binafsi.

Maisha ni Furaha na amani moyoni mwako, haijalishi we ni masikini, fukara, usiye na ajira, mgonjwa ama uliye na afya nje.

MUNGU yupo na kamwe tusijaribu kudhani kuwa sisi tupo kwa ajili ya maslahi yetu binafsi, Tupo kama jamii( race) ya uzao wa mwanadamu, tuwapende na kuwajali wenzetu, tuwe na kiasi katika malengo yetu.

#Mungu Awape Ustawi Mwema na Tumaini liliokuu na Upendo Udumu baina yetu.#
 
Back
Top Bottom