Joyce!!! Leo ni siku ambayo hutakaa kuisahau maishani mwako. Nasema hivi kwa sababu jana tu ndo umetoka Tabora kumwona rafikiyo wa karibu sana, namanisha mmeo. Leo tena tena kupitia hapa JF tunajuzwa habari ya msiba wa babako, Pole sana dadangu... Kuna mambo mawili nataka yakufariji; 1. Mungu anaweza kuonekana zaidi wakati wa furaha na aman na wakati wa shida asionekane kabisa. Hapa nina maana kwamba Mungu yupo pamoja nasi kila wakati ila tunapokuwa na furaha na amani yeye huwa pembeni yetu na ndiyo maana unamuona, lakini tunapokuwa na woga au kupita ktk shida na majaribu yeye hutuchukuwa na kutufunika na uwepo wake na ndiyo maana hatumuoni. So, hupaswi kuogopa chochote kwani yeye atakuvusha kwenye bonde la uvuli (Zaburi 23:1-6). 2. Joyce, kila jambo linalotokea hapa dunian liwe zuri au baya, iwe furaha au huzuni fahamu kuwa Mungu karuhu. Mungu ndiye ajuaye sababu. Umesikia habari ya Ayubu, ndo maana tumeagizwa kushukuru kwa kila jambo... 3. Mwisho, ucmtafute mtu yeyote juu wakati huu ila MUNGU pekee. MANGU NA AKUSAIDIE