Neno la Asubuhi: Mwayachunguza maandiko

mitale na midimu

JF-Expert Member
Aug 26, 2015
10,420
17,701
- Kunatofauti ya Maarifa ya Bibilia (Bible knowledge) na Kujua kiini cha maandiko unayoyasoma.
- Mafarisayo,Masadukayo,waandishi na wanasheria walikuwa wamebobea katika Maarifa ya Maandiko lkn hwaelewi kuwa maandiko hayo yote yanamuelezea wanayempinga (Yesu).
-Lkn pia Shetani ni mbobezi aliyetukuka katika Bible knowledge.


Kama utasoma maandiko, ukawa msemaji mzuri wa maandiko lkn maandiko hayo yakayaacha maisha yako bila kubadilika kumbuka utakuwa katika hadhi zilezile za Maarifa ya Bibilia.
Asubuhi ya Leo tunapaswa Kumuona Mwokozi wa Ulimwengu katika kila kurasa ya maandiko matakatifu, na pia Tumruhusu kupitia maneno hayo abadilishe maisha yetu tupate kutembea katika upya wa Uzima.


Bible Knowledge is not enough. Satan has A in bible knowledge.
Yohana 5:39-40
 
Mwanakoo Ameshinda!
ameen.
Maandiko hayasomwi Kubishaniwa...
Maandiko hayasomwi kudhalilishana...
Maandiko hayasomwi ili kuyashusha viwango yakidhi matakwa ya kisayansi na kiphilosophia...
Maandiko hayasomwi ili uyatumie kama mjeredi wa kumuadhibia usiyempenda...
Maandiko hayasomwi kuburuza watu wasio na ufahamu ili utafune sadaka zao....

Maandiko yanasomwa ili tupate uzoefu mpya wa Maisha. Yule binadamu wa zamani (Carnal mind) ambaye anauadui na Mungu afe, na Kristo ambaye ni kiini cha bibilia yote aishi ndani yetu.

nje ya hapo tutakuwa tunaongea lugha moja na mafarisayo,masadukayo,waalimu na waandishi zaidi ya yote mkuu wa giza.

ubarikiwe mkuu.
 
Duh, Asante Sana Kwa Mada fikirishi. Uwe na Siku njema. Je, mtu akiomba aombewe Utamshaurije? Akasome maandiko amjue Mungu, nadhani itakua ndio njia sahihi.
Kuomba ni kuongea na Mungu kama mtu anavyoongea na rafiki yake.
Kuomba ni kumwambia Mungu akutendee kile alichosema atakutendea. Mungu hujibu vitu alivyosema atafanya. Ili uvijue lazima usome neno.
Binafsi nashauri watu waombe na kusali kutokea kwenye Maandiko zaidi ya kuombewa. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu labda kama akiwa hajiwezi.

Yesu alisema "NANYI MKIWA KATIKA KUSALI.... ". anategemea Tusali sio kusaliwa au kusalishwa.

maoni yangu mkuu.
 
Kuomba ni kuongea na Mungu kama mtu anavyoongea na rafiki yake.
Kuomba ni kumwambia Mungu akutendee kile alichosema atakutendea. Mungu hujibu vitu alivyosema atafanya. Ili uvijue lazima usome neno.
Binafsi nashauri watu waombe na kusali kutokea kwenye Maandiko zaidi ya kuombewa. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu labda kama akiwa hajiwezi.

Yesu alisema "NANYI MKIWA KATIKA KUSALI.... ". anategemea Tusali sio kusaliwa au kusalishwa.

maoni yangu mkuu.
Mkuu uko sawa kabisa kwa mujibu wa Ukristo.Mwanadamu anaalikwa kumtegemea Mungu kimwili na kiroho tena anakumbushwa "nje yangu hamwezi kuzaa(kufanikiwa)".Mwaliko huu ni hakika na unatenda kazi kwa kila aaminiye kwa unyoofu kabisa.Yoh 12:26---
 
Njia ya msalaba, yaongoza nyumbani
ameen...
"Lakin HASHA mimi nisione fahari juu ya kitu chochote ila msalaba, ambao kwa huo ulimwengu umesurubishwa kwangu, na mimi ulimwengu kwa huo " wagalatia 6:14

bila kujali kama huna dini,muislam,Atheist,mkristo,myahudi,budha,freemason au chochote ikiwa Humuoni yesu na alichokifanya Msalabani kwa ajili ya Ulimwengu Kuanzia Mwanzo hadi Ufunuo bado utakuwa unaongea lugha moja na mafarisayo na waandishi wabobezi waneno lkn hawakujua linamzungumzia nani.
 
ameeen
hekima na maarifa vyatoka kwa Mungu.
"Zishikeni basi, mkazitende......Nao watasema, Hakika taifa hili KUBWA ni watu WENYE HEKIMA NA AKILI" Kumbukumbu la Torati 4:6

kwingine kote ni ubatili na kujilisha upepo.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom