Neno la Asubuhi: Mwayachunguza maandiko

Neno la Asubuhi: Mwayachunguza maandiko

Neno hili sio la Asubuhi tu bali la siku! Ahsante kwa kutupa chakula cha siku
Mababu zetu wa IMANI walikula Mana wakaishi jangwani, na Sisi kwa CHAKULA hiki tutaishi katikati ya dunia hii iliyojaa kila aina ya masumbufu,hofu,manyanyaso,kutokutabirikia na vifo vya kushtukiza.

ameen mkuu
 
Kuomba ni kuongea na Mungu kama mtu anavyoongea na rafiki yake.
Kuomba ni kumwambia Mungu akutendee kile alichosema atakutendea. Mungu hujibu vitu alivyosema atafanya. Ili uvijue lazima usome neno.
Binafsi nashauri watu waombe na kusali kutokea kwenye Maandiko zaidi ya kuombewa. Hayo ndiyo mapenzi ya Mungu labda kama akiwa hajiwezi.

Yesu alisema "NANYI MKIWA KATIKA KUSALI.... ". anategemea Tusali sio kusaliwa au kusalishwa.

maoni yangu mkuu.
Upo sahihi kabisa
 
Mkuu uko sawa kabisa kwa mujibu wa Ukristo.Mwanadamu anaalikwa kumtegemea Mungu kimwili na kiroho tena anakumbushwa "nje yangu hamwezi kuzaa(kufanikiwa)".Mwaliko huu ni hakika na unatenda kazi kwa kila aaminiye kwa unyoofu kabisa.Yoh 12:26---
Ameen.
Kama tunaamini mwanadamu Aliumbwa na Mungu, ni busara ya hali ya juu sana Kuamini Ukombozi wetu kwa njia ya Kristo.
Pale tulipomkataa Mungu na kumchagua Shetani, yeye mwenyewe alikuwa wa kwanza kututafuta wakati sisi tukiwa gizani na tukikabiliwa na kifo.
Kukubali au kukataa mchakato huu wa ukombozi kupo katika uchaguzi wa kila mwanaadamu.

"...Kwa kuwa nimekuwekea mbele yako UZIMA na MAUTI, BARAKA na LAANA, Basi chagua uzima ili uwe hai wewe na uzao wako" Kumbukumbu 38:19
 
- Kunatofauti ya Maarifa ya Bibilia (Bible knowledge) na Kujua kiini cha maandiko unayoyasoma.
- Mafarisayo,Masadukayo,waandishi na wanasheria walikuwa wamebobea katika Maarifa ya Maandiko lkn hwaelewi kuwa maandiko hayo yote yanamuelezea wanayempinga (Yesu).
-Lkn pia Shetani ni mbobezi aliyetukuka katika Bible knowledge.


Kama utasoma maandiko, ukawa msemaji mzuri wa maandiko lkn maandiko hayo yakayaacha maisha yako bila kubadilika kumbuka utakuwa katika hadhi zilezile za Maarifa ya Bibilia.
Asubuhi ya Leo tunapaswa Kumuona Mwokozi wa Ulimwengu katika kila kurasa ya maandiko matakatifu, na pia Tumruhusu kupitia maneno hayo abadilishe maisha yetu tupate kutembea katika upya wa Uzima.


Bible Knowledge is not enough. Satan has A in bible knowledge.
Yohana 5:39-40

Swali dogo, wakati Yesu Kristo akiwa na umri kati ya miaka 13 na 29, alikuwa wapi na anafanya nini? Nimeuliza kwani kwenye Biblia kipindi hiki hakina maelezo.
 
Tungekuwa tunapata mada kama hizi kila asubuhi. Hata wanaotaka tufungiwe JF yetu wangeshindwa na kuanguka.

Uwe na amani ya BWANA mtumishi.
amina mkuu.
neno ni chakula cha moyo chenye dawa na uhai ndani yake.
wengi wangemiminika jf kutafuta dawa, maana siku hizi hatulishwi Manna makanisani katika viwango vyake, wengi wanatulisha miujiza na maneno yao.
Mungu Ilinde JF idumu milele.
 
Swali dogo, wakati Yesu Kristo akiwa na umri kati ya miaka 13 na 29, alikuwa wapi na anafanya nini? Nimeuliza kwani kwenye Biblia kipindi hiki hakina maelezo.
"Kuna mambo mengi aliyoyafanya Yesu; ambayo yakiandikwa moja moja, nadhani hata ulimwengu usingetosha kwa vile vitabu vitakavyoandikwa " Yohana 21:25
.

Sijui alikuwa wapi, ila popote alipokuwa HAKUTENDA DHAMBI Wala kufanya mambo ya Hovyohovyo.
(...bali yeye alijaribiwa sawasawa na sisi katika mambo yote, bila kufanya dhambi :Wabrania 4:15)

ubarikiwe mkuu.
 
Back
Top Bottom