Neno kwa Wanachama wa JF: Tulizeni Mioyo

Kuna habari kama tatu hivi au nne hapa karibuni ambazo zinahusisha taasisi kadhaa - za umma na za binafsi - ambazo hazijawapendeza sana wakubwa wa kwenye taasisi hizo. Kwanza, ni kwa sababu taasisi hizo ziliwekwa kwenye mwanga mbaya sana kwa vile wakubwa wake ni watu ambao wanaamini wako kwenye mwanga mzuri sana kiasi cha kuwalazimisha kujitokeza kukanusha habari zilizoko kwenye mtandao huu - mwenye macho na asome na kuelewa. Habari hizi, hazijamgusa moja kwa moja Rais Magufuli lakini hofu ya baadhi ya watu - kutumbuliwa - sababu ya habari hizo imewafanya watu wawe kwenye hali ya kujihami (defensive). MMM

Hapa nilipo BOLD! Kweli MMM umeamua kuwa devil's advocate! Huwezi kuona zaidi ya urefu wa pua yako. You must be suffering from selective amnesia!

Ngoja nikukumbushe, hivi nani aliyesema kwamba anatamani MALAIKA washuke mbinguni waje kuifungia mitandao yote ya kijamii? Ni hao wakuu wa Taasisi 4 za umma ambao taarifa zao zime-leaked JF? au ni huyo ambaye taarifa zilizo leak JF hazimuhusu?

To put it simple kwa wale wenye ostrich brain (no offense intended). Hivi nani mwenye mamlaka ya kuamulisha vyombo vya dola kufanya upekuzi kwenye mitandao ya kijamii na kuwaweka watu ndani? Ni wakuu hao wa Taasisi 4 ambao taarifa zao zime leak JF au ni huyo ambaye habari zilizo-leak JF hazimuhusu?!

Usitufanye mazuzu bwana we can put two and two together.
 
Asante kwa maneno yenye kutia moyo ila kiukweli nimejikuta tu nakuwa mzito kuachangia mada tangu hii issue ianze hasa site ya siasa,
Nimeamini ukimchunga sana mfanyakazi wako hata hyo kazi hatofanya kwa uhuru
 
Uliemsimika kwa maslahi ya kigango ... endelea kuonja joto ya jiwe ...

Salaam,

Najua wapo baadhi yetu humu ambao kwa namna fulani suala la kuwekwa kizuizini kwa Max limewatisha na kuwakwaza sana. Yawezekana wamo ambao wazo la wao kujulikana na watawala na labda mabosi wao maofisini n.k si jambo ambalo wanalitarajia au kuliombea. Najua tupo wanachama wa kila namna humo na kutoka katika mazingira mbalimbali. Kuna ambao wanajali kujulikana na wengine hawajali.

Wale wanaojali sana wanafanya hivi hasa labda kwa sababu kubwa mbili; kwanza yawezekana waliwahi kutoa habari kutoka maofisi yao ambazo bila ya wao zisingepatikana na kwamba wakijulikana kuna weza kuwepo na retaliation na wengine inawezekana kutokana na maoni yao ya hapa na pale wanaweza kuhofia kujulikana kuwa ni 'wao' walitoa maoni yale - yawe mazuri au mabaya kutegemeana na mtu anayeyasoma.

Naomba niseme kadhaa ambayo yamesemwa na wengine tayari.

Kwanza, suala la serikali kutaka kujua nani amesema nini JF halijaanza leo. Halijaanza na utawala wa Magufuli na sidhani kama linaweza kuisha na Magufuli. Na ni jambo ambalo halijasumbua hapa bali limesumbua na sehemu nyingi sana. Mfano mzuri wa kesi ya Snowden yule Mmarekani aliyetumia mitandao kufichua kashfa mbalimbali za ndani ya Marekani hadi nje alipoamua kumwaga hadharani nyaraka za mawasiliano ya Kibalozi. Serikali ya Marekani ilihangaika sana kutaka kujua ni nani aliyekuwa chanzo cha taarifa zile. Hivyo, ni kweli kuna taarifa na habari ambazo zinatolewa ambazo zinaweza kuhesabiwa kuwa ni nzito na za moto sana hasa kwa yale yanayotajwa na hivyo kutaka kujua nani amezitoa.

Baadhi ya taarifa hizo inawezekana ni ziko kwa watu wachache sana kiasi kwamba kujulikana kwake ni wazi kuna "leak" mahali fulani. Niwakumbushe watu kuwa miaka kadhaa huko nyuma kuna habari zilizowahi kuwekwa hapa kuhusiana na PPF, Posta, na ATCL na zilisumbua sana wakubwa kwenye taasisi hizo kiasi cha kusababisha ili kujilinda kuwaondoa watu fulani fulani; na ninakumbuka kuna mahali ilibidi watu fulani waondolewe kwa kuhisiwa tu - bila ushahidi wowote kisa mtu alionekana ametembelea mtandao wa JF ofisini! Matokeo yake ili kujilinda wakaondoa waliokuwemo na wasiokuwemo katika kufanya retaliation zao hizo.

Kuna habari kama tatu hivi au nne hapa karibuni ambazo zinahusisha taasisi kadhaa - za umma na za binafsi - ambazo hazijawapendeza sana wakubwa wa kwenye taasisi hizo. Kwanza, ni kwa sababu taasisi hizo ziliwekwa kwenye mwanga mbaya sana kwa vile wakubwa wake ni watu ambao wanaamini wako kwenye mwanga mzuri sana kiasi cha kuwalazimisha kujitokeza kukanusha habari zilizoko kwenye mtandao huu - mwenye macho na asome na kuelewa. Habari hizi, hazijamgusa moja kwa moja Rais Magufuli lakini hofu ya baadhi ya watu - kutumbuliwa - sababu ya habari hizo imewafanya watu wawe kwenye hali ya kujihami (defensive).

Zimetumika njia nyingi za kujaribu kuwatambua watu walioleta habari hizo hapa na kwa vile ni vigumu kwa watu hao kujulikana basi hili limetokea na ninaamini litatokea mbele kwa sababu nitakayoileza hapa chini. Tatizo ni kuwa watu wanaotaka kujua nani kasema nini hawajasoma 'disclaimer' iliyopo chini kwenye ukurasa wa mwanzo wa mtandao huu.

Kutokana na hilo naomba kusema mambo machache kwa ufupi kwa viongozi wahusika, polisi, Bunge, Rais n.k.

1. Ni lazima watu wajiulize kwanini watu wako radhi na tayari kwenda kwenye mtandao kutoa madudu au manung'uniko ya mambo yanayotokea kwenye maofisi yao. Kwanini watu walikuwa tayari kufichua ufisadi wa PPF, Postal, na ATCL (kununua ile Airbus 320) badala ya kwenda kwenye vyombo vya umma kuwaambia - kama Polisi, TAKUKURU au Ikulu kwenyewe? Jibu ni rahisi sana - hawaamini kama taasisi hizo zinaweza kuwalinda na kuwahakikishia usalama wao!

2. Kwanini mtu anaamua kutumia jina la kiuandishi ili kufichua uovu au kujadili mambo ambayo yanatokea kwenye taasisi yake au mahali fulani anapopajua; jibu ni rahisi - kwa sababu hajihisi yuko salama kulindwa akitoa taarifa hizo au akijulikana anatoa taarifa hizo!

3. Kwanini baadhi ya watu tangu kusikia kukamatwa kwa Max wanahisi kuwa nchi inaelekea kwenye majaribio dhaifu ya kuzima uhuru wa mawazo na maoni? NI kwa sababu hawajihisi salama kuzungumza kwa uhuru ule ule.

Kila chanzo kina matokeo.

Binafsi naamini Serikali na watendaji wa taasisi mbalimbali watakuwa salama sana na hawatokuwa na watu wanaoenda kwenye mitandao ya kijamii au nje ya taasisi hizo kuibua maovu endapo TU:

1. Sheria ya Kumlinda Mfichua Maovu (Whistle Blower Protection Act) itapitishwa na Bunge ili kuhakikisha kuwa mtu anayefichua uovu kwenye taasisi yake halipiziwi kisasi kama kufukuzwa kazi, kupunguzwa cheo, kuhamishwa, kucheleweshwa kupanda vyeo n.k ili kumkomoa. Kwa kadiri ya kwamba wafanyakazi waadilifu hawalindwi, hakuna mwadilifu atakayekuwa tayari kujulikana.

2. Mifumo ya Ndani ya Taasisi Kuimarishwa - kama taasisi zenyewe hazina mifumo mizuri ya kushughulikia maadili na kubaini vitendo viovu na kuvishughlikia haraka ni wazi kuna watu wataona ni bora wamwambie mtu wa nje. Taasisi yoyote ya umma inayojaribu kufanya kazi kama genge la kihalifu ijue kuwa itakuta wapo watu ambao wana maadili yao na hawako tayari kuwa sehemu ya uhalifu huo na hawa - kwa kuogopa visasi - watafichua maovu hata kwa kutumia majina bandia.

3. Mitandao ya Kijamii kama JF ni silaha nzito sana ambayo Serikali inaweza kuitumia ili kujenga uadilifu kwani watu wataogopa kuonekana. Hii JF inanikumbusha - na labda itawakumbusha wengine - juu ya kile kipindi cha "Mikingamo" cha enzi zile. Hii ndio Mikingamo ya siku hizi; watu wako tayari kufichua maovu katika jamii kwa sababu hawayapendi na Serikali siyo tu inapaswa kulinda mitandao kama hii bali pia kushukuru na kuhakikisha kuwa inafanya kazi kwa uhuru wote.

4. Sasa nafahamu kuna wakati inawezekana ni vizuri kupata ushirikiano wa mitandao kama hii ili kukabiliana na uovu fulani. Kwa mfano, mtu akija JF na kusema kuwa anapanga "kumuua kiongozi au mtu fulani" tishio hilo si la kupuuzia na Serikali ina maslahi ya kutaka kujua mtu huyo ni nani na yuko wapi. Mitandao kama hii inaweza kutoa ushirikiano kwa kadiri inavyowezekana. Hata hivyo, ili kufikia huko ni lazima uwepo utaratibu mzuri ambao utahusisha mahakama (judicial review) ili kuondoa mtu mmoja watu wachache kutumia 'kisingizio cha usalama wa taifa" kuanza kufuatilia watu. Hii ndio sababu ya kupinga ile sheria ya Cybercrime -kwani it was too vast and overeaching.
Ni maslahi ya serikali basi ili iweze kuweka sawa (balance) uhuru wa maoni na vyombo vya habari na mahitaji ya kiusalama ya taifa. Lakini haipaswi kuwa tu "nani kanisema vibaya nataka nimjue". Hiyo ni hoja ya kipuuzi.

Kwa wana JF wengi naomba msiwe na wasiwasi, madai wanayoyataka hawa ndugu zetu ni very specific, na yanahusiana na habari fulani mahsusi. Tatizo ni kuwa siyo jukumu la kina Max, au sisi wengine kuwafanyia kazi wao, baadhi ya mambo kama haya wangeweza kuyashughulikia wao wenyewe tena kwa urahisi tu na hasa kwa kuwa waadilifu, wawazi, na wawajibikaji. Ingeweza kutuepushia usumbufu sisi wengine. Lakini zaidi ni kuwa hakuna namna ambayo wasimamizi (moderators) au super moderators wanaweza kujua utambulisho halisi wa mtu hasa kwa mfano kama wanaishi nyumba moja, jengo moja au ofisi moja n.k Hakuna namna, na zaidi kwa vile wao hawamuoni mtu anapojisaini JF wala kumpiga picha au video kumuonesha akijisaini saa, mahali na muda fulani.

Tuna mambo mengi muhimu ya kitaifa na yanayosumbua vichwa vyetu kuliko kujaribu kuridhisha udadisi wa mtu au watu fulani.

Kutokana na tukio hili na kama nilivyosema jana kuwa halivumiliki, tuna reserve kutumia ICBM option au kutumia nuclear option.

Tulizeni mioyo, na hili litapita - wenye kupinga serikali na kumpinga Magufuli wataendelea na wale wengine ambao tunaamini tofauti tutaendelea. Ndio uzuri wa demokrasia na maana halisi ya Uhuru wa mawazo.

MMM
 
Yaani hapo umenikuna.
Hata hili la msako mpaka Ofisi za Jamii Media ilifaa ipate Judicial Review! Uhalali wa Madai ya Jina-in line with Law of the Land(Katiba ) Pamoja na mapungufu yake bado inafaa tuiheshimu Katiba iliyopo.

Hatuwezi kujenga Tanzania ya Viwanda kwa staili hii hata siku mmoja.
 
Huo ndo ukweli, wasafishe kikombe ndani na nje kitakuwa safi. Huwezi kuwazuia watu wasiseme.
 
Well said. Serikali yangu pendwa hapa ni sehemu sahihi pa nyie kupata habari ziwe nzuri au mbaya. Mh rais jukwaa hili linastahili tuzo kwani linaogopeka mno kwa kifichua maovu. lilinde kwa nguvu zote likusaidie kufikia malengo yako ya utawala.
 
Mkuu Mwanakijiji. Mimi sina shaka kabisa kuhusu kinachoendelea na jeshi la polisi. Kwa sababu naamini kabisa jeshi la polisi halina wataalamu wowote wa mambo ya digital. Cryptography technology na cloud computing sidhani kama wana utaaramu huo. Ndo maana unasikia wamechukuwa nyaraka kama leseni ya biashara na Registration certificate vitu ambavyo siyo vya msingi kwa kile wanachokitaka. Hapo utaona kuna mtu mwelewa hapo? Wanachotaka kukifanya labda ni kumbambikia kesi kuwa Max kuwa alikuwa halipi kodi. Polisi wanajua kushika bunduki tu haya mambo ya digital wako nyuma mno
 
Sasa tunakwenda vizuri na tumerudi kwenye uhalisia, hapo ndipo pa kuanzia tuanze kutatua matatizo yetu wenyewe na siyo kukimbilia kwa Wazungu, tunaweza hili linawezekana kabisa kwamba JF na wadau wake wakakae na Serikali chini kujadiliana na kufikia muafaka jinsi ya kutatua hili, hivi ndivyo inavyopaswa kuwa lkn watu wakikimbilia kwa Wazungu na kwenye vyombo vya Habari vya nje wanachokifanya ni kuzidi kuharibu badala ya kujenga kwani Serikali nayo haiwezi kusalimu kirahisi na hapo labda kutakuwa hakuna mshindi!

Lakini hili nina imani kabisa linaongeleka na baada ya hapo siajabu JF ikaibuka kwa nguvu zaidi na Imani kubwa ktk pande zote mbili za Serikali na jamii na hivyo kuwa win-win situation!

Hapo kwenye red, hilo linawezekana if you have a sensible kind of leadership, unfortunately what we have now is the leadership making decisions based on emotions
 
Basi pelekeni kwa Wazungu labda watawasaidia!
 
Baba kusekwa ndani na kuacha familia yako nje hujui wanaishije na kingine kibaya zaidi ni kupoteza ujira na mkate wa kila siku sio kitu cha mchezo.

Ni lazima uingie upepo flani hivi na woga kiasi.

Soon hili jukwaa utawaona baadhi ya watu wapo wenyewe kama akina lizaboni,le mutuz,tata madiba,faiza, et all.

Wengine tutakuwa kimnya tu kwani mtukufu sizonje kashusha malaika wake weusi kudhibiti,kushughulikia na kufungia wanaomkosoa. Kwani yeye anapenda kusikia nyimbo za sifa na kutukuza matendo yake tu. Anataka kusikika yeye peke yake tu.
Wewe umeandika bila kumuelewa mleta mada

Hili halihusiani na Magu
Mbona hamuelewi!!
 
Wakuu nadhani sasa mtaelewa always nasema jiachieni tu hamna wa kukamatwa na Max Melo ataachiwa tu hata iweje hii ni forums hulu na hii ni sehemu ambayo ipo free and safe.....hakuna details zitatolewa humu ndani maana kwanza kisheria hairuhusiwi kabisaaaa.....hizo data watafute wenyewe huko na sio humu ndani.....
 
Baba kusekwa ndani na kuacha familia yako nje hujui wanaishije na kingine kibaya zaidi ni kupoteza ujira na mkate wa kila siku sio kitu cha mchezo.

Ni lazima uingie upepo flani hivi na woga kiasi.

Soon hili jukwaa utawaona baadhi ya watu wapo wenyewe kama akina lizaboni,le mutuz,tata madiba,faiza, et all.

Wengine tutakuwa kimnya tu kwani mtukufu sizonje kashusha malaika wake weusi kudhibiti,kushughulikia na kufungia wanaomkosoa. Kwani yeye anapenda kusikia nyimbo za sifa na kutukuza matendo yake tu. Anataka kusikika yeye peke yake tu.

Wewe unaonekana mgeni humu huna hata miaka 5 nadhani ungeijua hii Forums ilipopotia usingesema hivyo wameanza kuizima kuanzia miaka hiyo sio leo wala jana Max ameshapitia sana tu kwenye hizo kashi kashi sio mara ya kwanzaa na hawezi toa details zozote zile...
 
Back
Top Bottom