Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,253
- 44,595
Salaam,
Najua wapo baadhi yetu humu ambao kwa namna fulani suala la kuwekwa kizuizini kwa Max limewatisha na kuwakwaza sana. Yawezekana wamo ambao wazo la wao kujulikana na watawala na labda mabosi wao maofisini n.k si jambo ambalo wanalitarajia au kuliombea. Najua tupo wanachama wa kila namna humo na kutoka katika mazingira mbalimbali. Kuna ambao wanajali kujulikana na wengine hawajali.
Wale wanaojali sana wanafanya hivi hasa labda kwa sababu kubwa mbili; kwanza yawezekana waliwahi kutoa habari kutoka maofisi yao ambazo bila ya wao zisingepatikana na kwamba wakijulikana kuna weza kuwepo na retaliation na wengine inawezekana kutokana na maoni yao ya hapa na pale wanaweza kuhofia kujulikana kuwa ni 'wao' walitoa maoni yale - yawe mazuri au mabaya kutegemeana na mtu anayeyasoma.
Naomba niseme kadhaa ambayo yamesemwa na wengine tayari.
Kwanza, suala la serikali kutaka kujua nani amesema nini JF halijaanza leo. Halijaanza na utawala wa Magufuli na sidhani kama linaweza kuisha na Magufuli. Na ni jambo ambalo halijasumbua hapa bali limesumbua na sehemu nyingi sana. Mfano mzuri wa kesi ya Snowden yule Mmarekani aliyetumia mitandao kufichua kashfa mbalimbali za ndani ya Marekani hadi nje alipoamua kumwaga hadharani nyaraka za mawasiliano ya Kibalozi. Serikali ya Marekani ilihangaika sana kutaka kujua ni nani aliyekuwa chanzo cha taarifa zile. Hivyo, ni kweli kuna taarifa na habari ambazo zinatolewa ambazo zinaweza kuhesabiwa kuwa ni nzito na za moto sana hasa kwa yale yanayotajwa na hivyo kutaka kujua nani amezitoa.
Baadhi ya taarifa hizo inawezekana ni ziko kwa watu wachache sana kiasi kwamba kujulikana kwake ni wazi kuna "leak" mahali fulani. Niwakumbushe watu kuwa miaka kadhaa huko nyuma kuna habari zilizowahi kuwekwa hapa kuhusiana na PPF, Posta, na ATCL na zilisumbua sana wakubwa kwenye taasisi hizo kiasi cha kusababisha ili kujilinda kuwaondoa watu fulani fulani; na ninakumbuka kuna mahali ilibidi watu fulani waondolewe kwa kuhisiwa tu - bila ushahidi wowote kisa mtu alionekana ametembelea mtandao wa JF ofisini! Matokeo yake ili kujilinda wakaondoa waliokuwemo na wasiokuwemo katika kufanya retaliation zao hizo.
Kuna habari kama tatu hivi au nne hapa karibuni ambazo zinahusisha taasisi kadhaa - za umma na za binafsi - ambazo hazijawapendeza sana wakubwa wa kwenye taasisi hizo. Kwanza, ni kwa sababu taasisi hizo ziliwekwa kwenye mwanga mbaya sana kwa vile wakubwa wake ni watu ambao wanaamini wako kwenye mwanga mzuri sana kiasi cha kuwalazimisha kujitokeza kukanusha habari zilizoko kwenye mtandao huu - mwenye macho na asome na kuelewa. Habari hizi, hazijamgusa moja kwa moja Rais Magufuli lakini hofu ya baadhi ya watu - kutumbuliwa - sababu ya habari hizo imewafanya watu wawe kwenye hali ya kujihami (defensive).
Zimetumika njia nyingi za kujaribu kuwatambua watu walioleta habari hizo hapa na kwa vile ni vigumu kwa watu hao kujulikana basi hili limetokea na ninaamini litatokea mbele kwa sababu nitakayoileza hapa chini. Tatizo ni kuwa watu wanaotaka kujua nani kasema nini hawajasoma 'disclaimer' iliyopo chini kwenye ukurasa wa mwanzo wa mtandao huu.
Kutokana na hilo naomba kusema mambo machache kwa ufupi kwa viongozi wahusika, polisi, Bunge, Rais n.k.
1. Ni lazima watu wajiulize kwanini watu wako radhi na tayari kwenda kwenye mtandao kutoa madudu au manung'uniko ya mambo yanayotokea kwenye maofisi yao. Kwanini watu walikuwa tayari kufichua ufisadi wa PPF, Postal, na ATCL (kununua ile Airbus 320) badala ya kwenda kwenye vyombo vya umma kuwaambia - kama Polisi, TAKUKURU au Ikulu kwenyewe? Jibu ni rahisi sana - hawaamini kama taasisi hizo zinaweza kuwalinda na kuwahakikishia usalama wao!
2. Kwanini mtu anaamua kutumia jina la kiuandishi ili kufichua uovu au kujadili mambo ambayo yanatokea kwenye taasisi yake au mahali fulani anapopajua; jibu ni rahisi - kwa sababu hajihisi yuko salama kulindwa akitoa taarifa hizo au akijulikana anatoa taarifa hizo!
3. Kwanini baadhi ya watu tangu kusikia kukamatwa kwa Max wanahisi kuwa nchi inaelekea kwenye majaribio dhaifu ya kuzima uhuru wa mawazo na maoni? NI kwa sababu hawajihisi salama kuzungumza kwa uhuru ule ule.
Kila chanzo kina matokeo.
Binafsi naamini Serikali na watendaji wa taasisi mbalimbali watakuwa salama sana na hawatokuwa na watu wanaoenda kwenye mitandao ya kijamii au nje ya taasisi hizo kuibua maovu endapo TU:
1. Sheria ya Kumlinda Mfichua Maovu (Whistle Blower Protection Act) itapitishwa na Bunge ili kuhakikisha kuwa mtu anayefichua uovu kwenye taasisi yake halipiziwi kisasi kama kufukuzwa kazi, kupunguzwa cheo, kuhamishwa, kucheleweshwa kupanda vyeo n.k ili kumkomoa. Kwa kadiri ya kwamba wafanyakazi waadilifu hawalindwi, hakuna mwadilifu atakayekuwa tayari kujulikana.
2. Mifumo ya Ndani ya Taasisi Kuimarishwa - kama taasisi zenyewe hazina mifumo mizuri ya kushughulikia maadili na kubaini vitendo viovu na kuvishughlikia haraka ni wazi kuna watu wataona ni bora wamwambie mtu wa nje. Taasisi yoyote ya umma inayojaribu kufanya kazi kama genge la kihalifu ijue kuwa itakuta wapo watu ambao wana maadili yao na hawako tayari kuwa sehemu ya uhalifu huo na hawa - kwa kuogopa visasi - watafichua maovu hata kwa kutumia majina bandia.
3. Mitandao ya Kijamii kama JF ni silaha nzito sana ambayo Serikali inaweza kuitumia ili kujenga uadilifu kwani watu wataogopa kuonekana. Hii JF inanikumbusha - na labda itawakumbusha wengine - juu ya kile kipindi cha "Mikingamo" cha enzi zile. Hii ndio Mikingamo ya siku hizi; watu wako tayari kufichua maovu katika jamii kwa sababu hawayapendi na Serikali siyo tu inapaswa kulinda mitandao kama hii bali pia kushukuru na kuhakikisha kuwa inafanya kazi kwa uhuru wote.
4. Sasa nafahamu kuna wakati inawezekana ni vizuri kupata ushirikiano wa mitandao kama hii ili kukabiliana na uovu fulani. Kwa mfano, mtu akija JF na kusema kuwa anapanga "kumuua kiongozi au mtu fulani" tishio hilo si la kupuuzia na Serikali ina maslahi ya kutaka kujua mtu huyo ni nani na yuko wapi. Mitandao kama hii inaweza kutoa ushirikiano kwa kadiri inavyowezekana. Hata hivyo, ili kufikia huko ni lazima uwepo utaratibu mzuri ambao utahusisha mahakama (judicial review) ili kuondoa mtu mmoja watu wachache kutumia 'kisingizio cha usalama wa taifa" kuanza kufuatilia watu. Hii ndio sababu ya kupinga ile sheria ya Cybercrime -kwani it was too vast and overeaching.
Ni maslahi ya serikali basi ili iweze kuweka sawa (balance) uhuru wa maoni na vyombo vya habari na mahitaji ya kiusalama ya taifa. Lakini haipaswi kuwa tu "nani kanisema vibaya nataka nimjue". Hiyo ni hoja ya kipuuzi.
Kwa wana JF wengi naomba msiwe na wasiwasi, madai wanayoyataka hawa ndugu zetu ni very specific, na yanahusiana na habari fulani mahsusi. Tatizo ni kuwa siyo jukumu la kina Max, au sisi wengine kuwafanyia kazi wao, baadhi ya mambo kama haya wangeweza kuyashughulikia wao wenyewe tena kwa urahisi tu na hasa kwa kuwa waadilifu, wawazi, na wawajibikaji. Ingeweza kutuepushia usumbufu sisi wengine. Lakini zaidi ni kuwa hakuna namna ambayo wasimamizi (moderators) au super moderators wanaweza kujua utambulisho halisi wa mtu hasa kwa mfano kama wanaishi nyumba moja, jengo moja au ofisi moja n.k Hakuna namna, na zaidi kwa vile wao hawamuoni mtu anapojisaini JF wala kumpiga picha au video kumuonesha akijisaini saa, mahali na muda fulani.
Tuna mambo mengi muhimu ya kitaifa na yanayosumbua vichwa vyetu kuliko kujaribu kuridhisha udadisi wa mtu au watu fulani.
Kutokana na tukio hili na kama nilivyosema jana kuwa halivumiliki, tuna reserve kutumia ICBM option au kutumia nuclear option.
Tulizeni mioyo, na hili litapita - wenye kupinga serikali na kumpinga Magufuli wataendelea na wale wengine ambao tunaamini tofauti tutaendelea. Ndio uzuri wa demokrasia na maana halisi ya Uhuru wa mawazo.
MMM