Neno "Huyu anakubalika" lipigwe marufuku katika kampeni za uchaguzi-2015. | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Neno "Huyu anakubalika" lipigwe marufuku katika kampeni za uchaguzi-2015.

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Tango73, Feb 26, 2012.

 1. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #1
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  HIli neno "huyu anakubalika" ni neno la kitapeli ambalo lengo lake ni kumtaka mtu ampigie kura au ampende mtu ambaye hana sifa za kutawala au kuwa mbunge. Utakuta mtu anakuambia au uvumi unaenea mitaani kuwa , mtu "huyu anakubalika", lakini hata mara moja huambiwi sifa za mtu huyo katika Jamii na mafanikio yake.

  Watanzania tusipokuwa makini na usemi huu wa kishetani wa" mtu huyu anakubalika" tutazidi kupata matapeli wa kisiasa wa kuendesha nchi hii na ambao watatucheleweshea maendeleo. Mkoa wa Ruvuma unaongoza hapa tanzania kwa kutumia usemi usemi huu wa "Huyu anakubalika kichama" bila kutaja sifa za mgombeaji.

  Mgombeaji wa uraisi au mbunge lazima achambuliwe ki undani sifa zake zote za kijamii na elimu. Hata kama aliwahi kuvuta bange au kubaka msichana , lazima zianikwe ili watu wamfahamu kwa undani maisha yake ya kiadilifu. Utakuta mtu anagombea uraisi au Ubunge, lakini ofisini kwake , kalala na mke wa mtu, kazaa nje ya ndoa, kaiba kiwanja na kujenga nyumba katika viwanja vya kuchezea watoto na haja retire Imprest nne, wewe unategemea nini kama mtu huyu akiukwaa ubunge au Uraisi?

  Sasa madhala ya neno , mtu huyu anakubalika yanapoficha maovu ya mgombea Ubunge au Uraisi yanapojitokeza.

  Jamani watanzania tukue na kukomaa kiakiri na kuachana na maneno ya kitapeli ya kisiasa ya enzi za Ujamaa na kujitegemea.
   
 2. Tango73

  Tango73 JF-Expert Member

  #2
  Feb 26, 2012
  Joined: Dec 14, 2008
  Messages: 1,678
  Likes Received: 34
  Trophy Points: 135
  wagombea uraisi na wabunge lazima wajue jinsi ya kutafutia watu kazi na kuboresha elimu -2015. wilaya ya Igunga inaongoza kwa kutapeliwa na usemi huu wa mtu huyu anakubalika kichama! wananchi lazima wamchague mtu ambaye ana sifa za kuwatafutia kazi na siyo mtu wa kuvaa suruali za balito na mashati ya juliana.
   
Loading...