Mkurya romantic
Member
- Jul 21, 2022
- 41
- 61
Watu wengi huficha makosa kwa kutumia neno bahati mbaya.Kitu kinachopelekea kufanya kosa lilelile,hii yote ni kuamini kwamba mikosi ndiyo huwaingiza matatizoni lakini katika hali ya kawaida,kila matatizo yanayotutokea yana chanzo,baadala ya kutumia muda na akili nyingi kuhesabu bahati mbaya zako,tumia muda wako kuhesabu vyanzo vya matatizo yako unayopitia.
Usitumie muda kuhesabu matatizo bali jifunze kujua chanzo cha matatizo kwani ukitumia neno bahati mbaya unaficha chanzo cha tatizo na kujiona hujakosea,tuache kujipendelea yanapotufika kwani tusipojua chanzo cha tatizo tutaishia kujiona tuna mikosi kumbe makosa yetu tukiyabaini wapi tunakosea kesho hatutapita palepale tulipopita jana.Lakini tusipobaini tupita palepale.
Wanasaikolojia wengi Duniani husema mtu aliyepitia matatizo mengi ni mtu imara kuliko ambaye hajayapitia matatizo mengi ”.Hivyo matatizo huweza kuwa mtaji.
Kumbe basi, matatizo ukiyatumia chanya hukupa uzoefu wa kuhimiri kwani ukikabiliana na changamoto unakuja kuwa imara na wale waliozoea mteremko wanakuwa dhaifu wanapokumbana na matatizo.
Sasa yatumie matatizo yako kama darasa la kukupa ujuzi.Kutatua tatizo wakati fulani husaidia kukufanya upate nguvu kutatua tatizo lingine unalokumbana nao.
Hivyo matatizo hatutakiwi kuyaogopa na kujiongopea pasipo kukubali ukweli halisi wa jambo, kwani ukweli ndiyo hukupa mwelekeo halisi na asili ya tatizo lilivyo bila kuweka hisia za utetezi.Kwahiyo tatizo hutupa maandalizi ya kufanikiwa kama tutarekebisa makosa yetu.
“Kila mtu ana matatizo yake, matatizo yako ni ya kwako,unahitajika kuyatua ili upate ujuzi na kujua tatizo lilitokeaje, usitangulize tu neno Bahati Mbaya au Siyo Riziki ”.Kwani hutajifunza wala matatizo yako hayatakusaidia kupata ujuzi.