NENDA MDOGO WANGU... nishari tamuu sana

NENDA MDOGO WANGU... nishari tamuu sana

lisaa mautamu

New Member
Joined
Aug 25, 2018
Posts
1
Reaction score
63
#NENDA_CHUO , #NENDA_MDOGO_WANGU

Nakupongeza kwa kufaulu kwenda Chuo Kikuu , aya nenda Mdogo wangu.

Wanafunzi 40,000 watapata mkopo , na wewe utapata mdogo wangu nenda.

Najua hujawahi kumiliki hata elfu 20 ya kwako mdogo wangu.

Pesa uliyokuwa unapata ni ile mia 5 ya *Shikamoo baba /shikamoo mama , naomba nauli ya kwenda shule* .Najua mdogo wangu.

Nenda nenda mdogo wangu.

Ukifika chuo kikuu utamiliki akaunti benki kwa Mara ya kwanza mdogo wangu nenda .

Kwa Mara ya kwanza utamiliki laki saba za kwako nenda mdogo wangu.

Kutoka kwenye miatano ya shikamoo Baba naomba nauli ya shule mpaka laki saba nenda mdogo wangu.

Ukipata laki saba utakosa cha kuifanyia nenda mdogo wangu.

Ukikosa cha kuifanyia utanunua Simu kama zote , PC kama zote , utawatumia pesa nyumbani bila hata kuombwa , utaenda club kama zote ila mwisho utarudi nyumbani Itigi.Nenda Mdogo wangu.

Nenda nenda mdogo wangu .

Mdogo wangu , hujawahi kufanya *Birthday Party* ila utafanya Chuo Mdogo wangu.

Utachukua laki tatu siyo nyingi mtatumia kwa Siku moja ya sherehe yako mdogo wangu .Kwani wewe ndo hupendi kuburudika mdogo wangu? Nenda mdogo wangu lakini ukimaliza Chuo hufanyi tena Birthday party mdogo wangu.

Nenda Chuo , nenda Mdogo wangu.

Kwani wewe hupendi kwenda Club ukalewe , wewe hupendi kuzijua beach kama zote za mjini. Nenda Mdogo wangu ila ukimaliza Chuo utakosa nauli ya kukurudisha nyumbani kwenu Itigi mdogo wangu.

Nenda chuo Nenda Chuo Mdogo wangu.

Najua hapo shuleni ulikuwa unawaona wanawake unatamani kuwaona kila kitu , mpaka unaenda na kioo shuleni ili ukawachungulie , *aya nenda chuo nenda Chuo Mdogo wangu*.Kona hii utakutana na Mchekoslovakia , kona ila utakutana na mnyarwanda , pale Mzungu mtanzania , hautohtaji vioo tena , hata ukipanda juu ya mti na yeye akiwa chini utaona unachokitaka ila nenda Ukimwi upo kama wote Mdogo wangu.

Nyumbani kwenu wewe ndiye umebahatika kufika Chuo kikuu mdogo wangu, umefka Chuo kwa lift ya Mjomba /Shangazi /Bamdogo kwasababu kwenu hamjiwezi Mdogo wangu. Soma miaka mitatu urudi tena kukaa kwa mjomba au shemeji yako Mdogo wangu.Nenda Chuo Nenda Mdogo wangu.

Nenda Chuo , Nenda Mdogo wangu.

Ni Elimu ambayo utaamua uingie darasani au usiingie , uandike au usiandike na ukiandika ukifanya mtihani utachana daftari mdogo wangu.Nenda

Ni pale ambapo Dada zako waliotumia Pesa vibaya utawakuta kwenye madanguro , utachagua aidha kuwa mteja wao au kufumba macho yote yapite na wewe ubaki imara.Nenda Ndogo wangu nenda .
Nenda Chuo , nenda Mdogo wangu.

Ni Chuo pale ambapo hutaweza kujifulia wala kujifatia Chakula , bali Pesa itafanya yote kwa ajili yako nenda Chuo Nenda, ila ukimaliza Chuo utayaweza nenda .

Nenda Mdogo wangu nenda .

Nenda Chuo, sehemu utakayohisi kwamba *Ukimalilza Chuo unaenda kwenye ile Ofsi ya ndoto yako, utakayohisi kuwa ukohtimu unamiliki maisha ya ndoto yako* , lakini usopoweka mipango vizuri ukimaliza utamoliki stress badala ya kazi na ofsi yako itakuwa ni bar kwenye gongo na Chang'aa. , nenda chuo Mdogo wangu nenda.

Nenda Mdogo nenda.

Ukiishiwa Pesa ujitahidi tu kuweka Voucher na uwe na Namba ya Waziri Wa mikopo .Kazi yako iwe kumtumia SMS *Pesa yetu mbona hamjaweka*?
Nenda Chuo Nenda Mdogo wangu.

Ninayo mengi ya kukusihi mdogo wangu ila tutaendelea kukumbushana , Ondoka na haya kwa leo *Kila anayefurahia maisha leo , alipata tabu sana Jana na kila anayepata tabu sana leo atafurahia maisha kesho*[emoji123]
 
Sawa dada naenda
 
AENDE TU MDOGO WETU HUKO ATAWAKUTA WOTE WA CERTIFICATE NA DEGREE WANAFANANA.....KILA MTU NI MTANASHATI WALA MASIKINI HUTOMJUA..KILA MTU ATAJINADI YEYE NI WAMJINI KUMBE KATOKEA MBWINDE.....AENDE MDOGO WETU HUKO KILA MTU ANAJUA ENGLISH KILUGHA WANAKIKANA...MDOGO WETU UKIFIKA USISAHAU KUWA BAADA UE KUNA STRESS ZA SUP NA DIS........USISAHAU KUKIPAIZA CHUO CHAKO HATA UKISOMA EDUCATION USEME ENGINEERING UKISWAGISHA NA KIBOMBO....HAKIKISHA HATA UKIFULIA USILE MANDONDO HADHARAN KALIE CHUMBANI.......MWISHO KRB KITAA NDIO KWAKO HUKO NI UGENINI NA USIMSAHAU BABY WAKO WA KITAA MPAUKAJI MANA HUKO UTAWAKUTA WAPYAA WAMAKAROLIGHT....HAKIKISHA WAKATI UKISOMA ILI KUITIMIZA PLANI A BASI PIA UIWAZE PLAN B ITAKAYOKUSAIDIA KITAA.
 
Chuo raha sanaaaa
Ukimaliza chuo unakuja kusota na kujutia ulivyolitumia boom vibaya
 
hahahahaha wataenda shika million watajiona maboss mjini hahaaha .... wadogo zangu chuo ni bata endapo unajitambua na unajua kupangilia vizuri mambo ako kama vile.. mda wa kusoma,mda wa kutembea , muda wa kuingia class.. ila kama hujitambui utaishia kuona huo msemo una maana gani utaishia disco na supp za maana..... karibuni chuo
 
Back
Top Bottom