Phillipo Bukililo
JF-Expert Member
- Dec 29, 2015
- 18,487
- 13,612
Uvaaji wa mtu huwa ni kielelezo cha mambo mengi yenye kuhusiana na maisha yake. Unaweza kumgundua mtu kama ni mvivu, mchapakazi, mpenda watu, msiri sana, unaweza kugundua mengi kwa kuutazama muonekano wa kila siku wa mtu fulani. Rais John Magufuli anavaa beji ya ramani ya Afrika juu ya suti yake, upande wa kushoto. Beji ile ina maana kubwa sana, haivaliwi kama mapambo ya mwilini.
Rais Magufuli anaamini katika uafrika wake, anaamini katika asili yake kwanza kabla hajaamua kujivika asili za watu wa mabara mengine. Ile beji nyekundu inasimamia tabia ya uzalendo kwa bara zima. Hata matamshi yake wakati akiongea na wafanyabiashara, wanafanana na ujumbe wa beji anayopenda kuivaa.
Mwalimu Nyerere alilipenda bara hili kwa vitendo, alitamani lote liwe na maisha bora, aliumizwa sana kila mara wazungu walipotudharau kwa sababu ya umasikini wetu. Alipopata muda hakusita kuwapa vidonge vyao wazungu pamoja na taasisi zao zenye hulka ya kupenda kunyenyekewa.
Rais Magufuli anao uzalendo kama wa Mwalimu Nyerere ndio maana ameweza kuanza mapambano ya kuhakikisha hata taasisi zetu za kibenki zinaondokana na tamaduni za kuwathamini wenye fedha wachache ambao kwa asilimia kubwa wanaishi katika majiji na makao makuu ya mikoa.
Beji ya Afrika anayoivaa rais Magufuli, sidhani kama inavaliwa kwa mbwembwe, nadhani kusudio lake ni kufikisha ujumbe kwamba afrika nzima kwake ni kitu cha kwanza na mengine yanafuatia. Kama afrika ni priority ya kwanza maana yake Tanzania nzima kwake ni chaguo la kwanza pia.
Nadhani kwa muda wote atakaokuwa Rais, atasafiri mara chache sana kwenda nje. Kwa Rais Magufuli Afrika kwanza mengine baadae, uzalendo wa alipozaliwa unaanza na mengine yanafuata baadae. Wazungu hawawapendi viongozi wenye fikra za aina hii, wanapenda wale walio tayari kuwapigia magoti na kujikomba.
Naamini beji anayoivaa Rais wetu italingana na matokeo ya utendaji kazi wa serikali ya awamu ya tano. Inatubidi kwa wingi wetu tuielewe maana ya beji ile, ili tuweze kujifunza dhana ya kuitumikia Afrika, kwa kuanzia na nchi yetu.