NELSON MANDELA mwanasaikolojia ambae hakusoma Saikolojia

LENGISHO

Senior Member
Sep 15, 2017
169
245
Mwaka 1990 Wakati Mandela Officially Anatolewa Gerezani Vijana Walio ANC wakati huo na wale wengine wasiokua ndani ya chama nyoyo zilikua zimewaka moto morale ilikua juu sana .

Katika speech yake ya kwanza akiwa huru wengi wa vijana hao walienda na mapanga na marungu kumsikiliza kiongozi wao kwa ishara wapo tayari kwa battle kulipa machungu ya mateso waliopata kwa wazungu wanahitaji tu order kutoka kwa Kiongozi wao Mandela.

Wakati wote huu CIA waliokua wana tambua Mandela Kama miongoni mwa gaidi mkubwa wakisubiri aseme lolote kwa vijana wake kwa matarajio ya kua anaweza kuamsha hali ya machafuko zaidi kwa maslahi ya kiasiasa.. vijana wale wa wakati huo wakikaa mkao wa kusubiri order na morale ilio juu sana wakiamini hata kiongozi wao ana kisasi cha kulipa baada ya kupoteza miaka 27 akitumikia kifungo .

Nelson Mandela Akasimama mbele yao akawaambia hajapenda anachokiona mbele yake na kama hayo ndio mawazo yao ya yeye atakuja kuwaongoza ivyo basi hayupo tayari kua kiongozi wao .. kama yeye akiwa kiongozi wao basi warudishe mapanga yao nyumbani waijenge nchi kwa pamoja na wazungu kua waafrica walio feel betrayed kuna walio muelewa ila kwa pamoja wote walikubali matokeo na wakaja kumuelewa zaid siku za usoni.

Nikifikiria hasira walio kua nayo hawa waafrica wa kusini wakati ule na ujasiri wa mandela kukataa machafuko ambayo hakua anahitaji kuwashawishi wapigane alitakiwa kutoa order tu maana wenyewe walishajitolea kupigana, najifunza kua huu ndio wito wa kisiasa haswa tunapaswa kua nao, na fujo hizi zinazoendelea huko SA zingeisha kirahisi kama kungekua na viongozi imara..

Viongozi wengi wa siku hizi wanaingia nusunusu hawataki kusimama kwenye ukweli kwa kuhofia tu maslahi yao ya kisiasa, wana wanqnchi wengi wana support hali ya kua na siasa zisizo make anysense wakiamini hivyo ndio siasa ilivyo
FB_IMG_1630748401947.jpg
 
Back
Top Bottom