Neema ya korosho msimu huu, bei yafikia tsh 4010

Msimu huu bei ya korosho imeendelea kupaa hadi kufikia sh. 4010 katika mnada wa jana huko Tunduru. Tukipata fedha hizi tujitahidi kujiwekea akiba kidogo.
Nawasilisha.
Ijumaa Tarehe 10, November 2017, umefanyika muendelezo wa minada ya zao la korosho ambapo taarifa zimeonyesha ule uliofanywa na TANECU umevunja rekodi kwa kufikia bei ya Juu ya hadi Tsh 4128.

Taarifa iliyotolewa na Media Coordinator, Brayson Mshana mapema leo imethibitisha bei hiyo na ile ya MAMCU ambao wao wameuza bei ya juu Tsh 4050.

“Mnada wa Leo wa TANECU uliofanyika kijiji cha mtopwa bei ya juu shiling 4,128/= na bei ya chini shilingi 4,010/= . Jumla ya tani 12 zimeuzwa taarifa zaidi nitawatumia kampuni zilizonunua korosho , MAMCU wao wameuza bei ya juu 4,050/= na bei ya chini Tsh 3,800/=ameandika Mshana kwenye taarifa yake kwa WanaHabari

Sasa baada ya taarifa hizo, BecaLoveTz.Com imeyanasa maandishi yaliyoandikwa na Katibu Tawala wilaya ya Nanyumbu, Salum Palango kwenye Ukurasa wake wa Facebook ambapo amefunguka kuhusu maendeleo yanayoendelea kufikiwa na minada hii na kusema Rekodi ya mnada wa leo ndiyo ambayo inaongoza tangu kuanza kwa minada hii.

>>> “Mnada wa KOROSHO KWA Vyama vinavyohudumiwa na MAMCU kwa maana ya Masasi, NANYUMBU na Mtwara uliofanyika Leo Kijiji cha NAMBELEKETELA KATA ya Ziwani Wilaya ya Mtwara, Bei ya Juu ni Tsh 4,050/= na ya chini ni Tsh 3,800/= Aidha mnada wa KOROSHO wa Vyama vinavyohudumiwa na TANECU KWA maana ya NEWALA na Tandahimba Bei ya Juu ni Tsh 4,128/= na ya chini ni Tsh 4,010/=!” ameandika Palango

Palango ameendelea kuonyesha furaha yake kwa mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya awamu ya tano kwenye upande wa bei ya zao la korosho kwa kuandika kuwa bei hii ya mnada wa nne Leo, imevunja rekodi ya minada yote iliyowahi kufanyika.

“Jumla ya Tani zilizouzwa ni 13,033.6 kwa MAMCU na Tani 10,000 kwa TANECU! ….RECORD ya BEI YA Tsh 4,128 kwa kilo moja ya KOROSHO KWA sasa ndo Bei ya JUU kabisaaa ikiivunja ya [HASHTAG]#MWAMBAO[/HASHTAG] Lindi ya Tsh 4,065 ya Wiki iliyopita! ” SERIKALI YA WATU KWA AJILI YA WATU”
 
55d5f7c7b4fcd09cd6628d70553339fa.jpg
 
Wanaouza kwa wanunuzi ni wakulima wenyewe au kuna watu wananunua na kuuzia hao wanunuzi wakubwa?
 
Mfumo uko hivi, vyama vya ushirika vinakusanya korosho kutoka kwa wakulima alafu wanaenda kuuza kwa matajiri wakubwa. Baada ya mauzo vyama vinaenda kulipa fedha walizopata kwa wakulima.
Kwa hiyo kama Mimi nataka kufanya huo ujasiriamali mpaka niwe na mashamba yangu cyo?
 
HII NDO SHIDA YA WAIZRI MKUU KUJIPENDELEA WAKULIMA WAKUSINI KUPATA BEI NZURI...ILI KUONYESHA HAKUNA KUPENDELEWA BASI BEI INGESHUKA KAMA YA MBBAZI ILI KUONYESHA KUWA HAKUNA UHUSIANO NA KUWA NA WAIZIRI MKUU

Ijumaa Tarehe 10, November 2017, umefanyika muendelezo wa minada ya zao la korosho ambapo taarifa zimeonyesha ule uliofanywa na TANECU umevunja rekodi kwa kufikia bei ya Juu ya hadi Tsh 4128.

Taarifa iliyotolewa na Media Coordinator, Brayson Mshana mapema leo imethibitisha bei hiyo na ile ya MAMCU ambao wao wameuza bei ya juu Tsh 4050.

“Mnada wa Leo wa TANECU uliofanyika kijiji cha mtopwa bei ya juu shiling 4,128/= na bei ya chini shilingi 4,010/= . Jumla ya tani 12 zimeuzwa taarifa zaidi nitawatumia kampuni zilizonunua korosho , MAMCU wao wameuza bei ya juu 4,050/= na bei ya chini Tsh 3,800/=ameandika Mshana kwenye taarifa yake kwa WanaHabari

Sasa baada ya taarifa hizo, BecaLoveTz.Com imeyanasa maandishi yaliyoandikwa na Katibu Tawala wilaya ya Nanyumbu, Salum Palango kwenye Ukurasa wake wa Facebook ambapo amefunguka kuhusu maendeleo yanayoendelea kufikiwa na minada hii na kusema Rekodi ya mnada wa leo ndiyo ambayo inaongoza tangu kuanza kwa minada hii.

>>> “Mnada wa KOROSHO KWA Vyama vinavyohudumiwa na MAMCU kwa maana ya Masasi, NANYUMBU na Mtwara uliofanyika Leo Kijiji cha NAMBELEKETELA KATA ya Ziwani Wilaya ya Mtwara, Bei ya Juu ni Tsh 4,050/= na ya chini ni Tsh 3,800/= Aidha mnada wa KOROSHO wa Vyama vinavyohudumiwa na TANECU KWA maana ya NEWALA na Tandahimba Bei ya Juu ni Tsh 4,128/= na ya chini ni Tsh 4,010/=!” ameandika Palango

Palango ameendelea kuonyesha furaha yake kwa mafanikio yaliyofikiwa na serikali ya awamu ya tano kwenye upande wa bei ya zao la korosho kwa kuandika kuwa bei hii ya mnada wa nne Leo, imevunja rekodi ya minada yote iliyowahi kufanyika.

“Jumla ya Tani zilizouzwa ni 13,033.6 kwa MAMCU na Tani 10,000 kwa TANECU! ….RECORD ya BEI YA Tsh 4,128 kwa kilo moja ya KOROSHO KWA sasa ndo Bei ya JUU kabisaaa ikiivunja ya [HASHTAG]#MWAMBAO[/HASHTAG] Lindi ya Tsh 4,065 ya Wiki iliyopita! ” SERIKALI YA WATU KWA AJILI YA WATU”
 
Kwa hiyo kama Mimi nataka kufanya huo ujasiriamali mpaka niwe na mashamba yangu cyo?
Ndio mkuu ni lazima uwe na shamba lako na sio kununua kwa wakulima alafu wewe unaenda kuuza ili upate cha juu. Serikali imepiga marufuku kwa wanunuzi wadogo ukibainika jela au faini milion 5.
 
Nimekuelewa kiongozi, kwa sasa naamini mtapiga hela kwa kujiamni maana kwa hiyo bei NOAH zitakuwa nyingi sana huko kusini. Hongereni sana
 
Kwa Mwendo huu itabidi tuhamie Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kusini..,
 
Kama watu wa kusini hawataboresha maisha yao kipindi hiki basi tunaweza tukasema fedha hizi ni za laana kwao. Waweke mipango mizuri ya maendeleo ili kuondokana na dhana ya umaskini uliotopea kwa miaka mingi.
 
Nimekuelewa kiongozi, kwa sasa naamini mtapiga hela kwa kujiamni maana kwa hiyo bei NOAH zitakuwa nyingi sana huko kusini. Hongereni sana
Asante sana. Noah zilianza mwaka jana kila kijiji sasa kuna watu 2 au zaidi wanamiliki Noah.
 
Kuna ndugu yangu kapeleka mitsubishi canter anasema kila siku analaza 500000.
 
Msimu huu bei ya korosho imeendelea kupaa hadi kufikia sh. 4010 katika mnada wa jana huko Tunduru. Tukipata fedha hizi tujitahidi kujiwekea akiba kidogo.
Nawasilisha.

Ndugu zangu wa Kusini hasa Wamakuwa na Wayao acheni matumizi ya hovyo ya hizo Pesa mnazozipata na sijui ni kwanini huwa mkipata tu Pesa mnawehuka / mnachizika mno halafu mnaishia kuzitumia hovyo na mkiishiwa mnaanza kutusumbua kwa Simu zenu Sisi Ndugu zenu tuliopo Dar na Mikoa mingine. Mnasemwa sana lakini hambadiliki kiukweli mnatutia mno aibu. Mtoto wenu GENTAMYCINE ambaye upande mmoja ni wa Mara na mwingine wa Mtwara leo nawasema. Bahati mbaya sana tu sikijui vizuri Kimakuwa na Kiyao kama ambavyo nakijua mno Kizanaki na Kinyarwanda ila nilitamani niwaseme kwa Kilugha hapa.
 
Naomba kuuliza tafadhali,
1kg ya korosho isiyobanguliwa, ikibanguliwa italeta Korosho kiasi gani?
 
Kilo 4 hadi 5 (hutegemea ukubwa wa korosho) ya korosho (ghafi) yaani isiyobanguliwa hutoa kilo 1 ya korosho iliyobanguliwa
 
Back
Top Bottom