Neema kwa watumishi hii hapa!

tpaul

JF-Expert Member
Feb 3, 2008
21,818
18,241
Serikali imekiri kiwango cha kodi ambacho imekuwa ikitoza kwa wafanyakazi ni kikubwa kuliko nchi zingine Afrika mashariki na hivyo imeanza kufanya mpango wa kubadilisha viwango hivyo ili viweze kuendana na vile vya nchi zingine za jumuiya hiyo.

Hayo yamesemwa na waziri mkuu Mh Mezengo Pinda katika kipindi cha maswali ya papo kwa papo alipokuwa akijibu swali la Mh David Kafulila mbunge wa Kigoma kusini kwa tiketi ya NCCR mageuzi aliyetaka kujua ni lini serikali itapunguza kodi kwa wafanyakazi wake

Aidha Mh Pinda ameonyeshwa kukerwa na kitendo cha aliyekuwa naibu katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo Chadema Mh Zito Kabwe cha kujitokeza hadharani na kudai kuwa mshahara wake ni milioni 30 jambo alilosema kuwa ni uwongo wenye nia ya kumchafuali jina lake.

Hata hivyo kipindi hicho cha maswali ya papo kwa papo kwa waziri mkuu kiliingia dosari baada ya Mh Moses Machali mbunge wa Kasulu mjini kujikuta anajibizana na Mh Spika pale alipokataa kufuta kauli aliyoitoa dhidi ya wabunge wenzake.

Katika hatua nyingine wabunge wameendelea kuchangia muswada wa sheria ya kura ya maoni wa 2013 huku baadhi ya wabunge wakitumia muda wao mwingi kupigana vijembe kufundishana badala ya kutoa mawazo ambayo yataboresha mswada huo ambao ni muhimu katika kusaidia kupatikana kwa katiba mpya.:dance:
 
Back
Top Bottom