Pangusa machozi yakoo...
Futa mavumbi shangiliaaa...
Amekuja mtetezi wakoo...
Msaada kwa walio na shida...
Huuu wimbo niliusikia kwa mara ya kwanza kwenye Clouds radio jumapili moja Nikawa naukuta unaishia kabisa maneno ya mwisho niliyoyasikia ni ya hiyo Chorus hapo Juu...
Hariss Kapiga akawa anauelezea kidogo ni akina nani na ndipo nilipojua ni hao Neema na wimbo wao huo...
Kwa ambao mnapenda Vibe la ku praise lENYE MANENO ambayo ukiyaimba hata wewe yanakutia nguvu aseee Usiache u weka huu wimbo katika playlist yako,maana ni Bonge moja la mdundiko la ibadani.
Ukijisikia kusahau shida zako na kuruka ruka ndani kwako basi nakushauri Utafute huu wimbo halafu usikilize Utakuja kuniambia
Huu ni MOJA ya wimbo unaotakiwa uuimbe ukiwa na maringo kama yote hasa kwa watu kama sisi tulio MPOKEA YESU...
Katika step zangu kuna huwa nikifikaga Kwenye haya maneno Yaliyobeba Jina la wimbo step inabadilika na laiti mtu angekua akinirekodi angekua anapata raha ya aina yake maana Sio kwa kujichetua huku..
Burudani Moyonii..
Sina wasiwasi yesu yupo (narudiaga hiki kipande mara 50)
Mpokee Yesu nawe leo MOYONI
Akufanye upya moyo wako,uwe na Amani