Need Original? Fake or Genuine?

Yona F. Maro

R I P
Nov 2, 2006
4,201
219
Kuna habari mtu ukizipata huwa unashituka sana lakini unaanza kuzizoea kwa sababu kila siku unapata habari hizo kila siku na hata wakati mwingine wewe mwenyewe unakuwa sehemu ya habari hiyo kama umeshuhudia baadhi ya matuki haya .

Unaonaje unapoenda dukani kununua kitu muuzaji anakuuliza kama unataka Original au feki ? hii inatumika zaidi katika bidhaa kama simu , tv , vifaa vya computer au vitu vinavyohusiana na vifaa hivi vya mawasiliano .

Kama ni vitu kama cartridge , toner hivi muuzaji atakuuliza kama unataka original , feki au refill hapo ni kama unajua lakini kama hujui muuzaji atakupa feki au refill ambazo ni bei rahisi na anakuambia ikileta shida wewe rudisha duka hili hili tutakupa ingine .

Ukitaka hiyo original bei yake ni ghali na mara nyingi hawakupi warranty kwa sababu wana uhakika ni nzuri utatumia mpaka muda wake uishe hizi sana zinatumika katika hivi vitu kama cartdge na toner .

Kwa kukusaidia kama unaenda kunua vitu kama toner , kwanza angalia box yake mara nyingi hizi feki blue yake sio ya kungaa kama zilivyozingine ,halafu nyingi hazina lebo maalumu .

Mfano sasa hivi inajulikana REDDOT ndio wasambazaji wakubwa wa toner na cartridge za HP , utaona muhuri maalumu uko kama alama ya fedha lakini box la hiyo bidhaa yako ukiona hivyo ujue ni mali halali ya HP inayosambazwa na REDDOT .

Kwa toner haswa za printer kitaka ujue kama ni feki au la , ukifungua angalia hiyo karatasi yake ya nailoni , ni fupi haina nafasi ya kuweza kuzungusha hiyo cartridge kwa ndani , kabla ya kutumia toner unashauriwa utingishe .

Kwa sababu ni feki inakuwa imefunguliwa drum yake ukitingisha wino utamwagika hovyo kwahiyo hawakupi nafasi ya kutingisha wino huo inakuwa imebanwa , ukiona hivyo ujue umeliwa rudisha dukani haraka usikurupuke uanze kutumia .

………………………………………………………………………………..

Unaonaje unapoenda dukani kununua vitu kama printer hivi mfano HP DESKJET 1280 unakuta haina wino mwenye duka anakuambia subiri kidogo wino uje tutakuwekea .

Anafanya kitu kirahisi tu anaenda mtaa wa pili dukani kama PRANPEN hivi kununua hizi wino halafu anakuja kuweka katika printer yako na katika risiti inaandikwa kila kiti umenunua katika duka lile .

Au unaenda kununua printer unashangaa haina baadhi ya lebo za HP ukimwambia yule muuzaji anamwita Juma haraka analeta Lebo na kuipachika hapo inaonekana kama ni Bidhaa halali ya HP na ina andikwa Made In China , Malaysia au Indonesia .

Hizi printer ukitumia kwa muda wa miezi 3 hivi zinavujisha sana wino , na mara nyingi ukiprint vitu kama picha au karatasi nyingi maandishi hayatoki vizuri kwa ufupi zinakuwa na matatizo katika print header , unalizimika uwe unazifungua na kusafisha kila mara .

Na mwisho wa siku ukichukua Serial Number yake ukienda katika tovuti ya HP hawatambui Serial Number hizo , kwahiyo Msaada wa kiufundi ni ndoto wewe kupata .

Utatakiwa ueleze umeitoa wapi ili huyo aliyeuza achukuliwe hatua za kisheria haraka iwezekanavyo .

………………………………………………………………………………..

Umewahi kufika dukani unaona tangazo pale WE ONLY INSTALL GENUINE SOFTWARE , sasa umenunua Computer ambayo ni CLONE ( Ya kuunga Unga ) ambayo bei yake ni pungufu ya dola 350 .

Ukiangalia katika karatasi zao za bei unaambiwa CD ya windows ni dola 120 bei hutofautiana kama ni prof au home edi au vista lakini sio chini ya dola 100 lakini hapo hiyo clone yenye windows xp sp2 inauzwa dola 350 tukipiga mahesabu ya kitu kimoja kimoja katika hiyo computer kwa mfano


HARD DISK DRIVE 80 GB 50 USD
MAINBOARD PINLESS 80 INTEL USD
CPU 3.0 AND ABOVE 85 USD
RAM 512 MB 35 USD
CDRW COMBO 30 USD
CASE / MOUSE /KEYBOARD 30 USD
COOLING FAN 10 USD
WINDOWS XP PROF 150 USD FEKI MPAKA ALFU 10
JUMLA UNAPATA 320 USD BILA WINDOWS XP UKIWEKEWA HIVYO JUMLA NI 470

Ukipiga mahesabu utaona kuna kitu kinaendelea hapo katika maduka haya ya vifaa vya computer na computer zenyewe kwa hakika wadau wanatakiwa waingilie kati pamoja na serikali ili wasiendeleze mambo haya mbali zaidi kwa faida za taifa .

ORIGINAL ZIKOJE .

1 – unaponunua inakuwa na operating system yake pamoja na vikoromwezo vingine , au kama haina watakwambia wenye duka na kwa hakika bei yake itakuwa chini zaidi kwa sababu ya bei ya cd original ya computer husika .

2 – lazima inakuwa na cd ya configuration za monitor , drivers na applications pamoja na ya operationg system kwa sababu inaweza kukurupt .

3 – kuna kuwa na lebal katika case ya computer husika yenye product key na aina ya operating system pamoja na mtengenezaji wa computer hiyo kama ni Dell au HP .

4 – kuna Service Tag na Express Service Code , unapotaka msaada kutoka dell au hp hua wanataka hizi service tag ili kuhakiki bidhaa zao na wakupe msaada wa uhakika zaidi kama hizi namba hamna ujue kuna walakini .

5 – inatakiwa iwe na lebal kutoka intel kama ni Pentium au kama ni AMD lazima kutakuwa na lebal inayoonysha aina ya CPU .

Kwa msaada zaidi kama hiyo ni bidhaa ya hp mfano tembelea tovuti yao www.hp.com nenda katika products unaandika aina ya computer yako kisha unapata maelezo ya ziada kuhusu computer yako .

Maelezo haya ya ziada ni ilipotengenezwa iliwekwa nini na nini , kuna watu wanamtindo wa kubadili HDD na kuweka za hali ya chini kama western Digital wakati katika tovuti imeandikwa SeaGate , hata RAM na vitu vingine vingi kwa faida zao wenyewe .

Kama chochote kimebadilishwa lazima mwenye duka au muuzaji atoe taarifa kabla ya wewe kuamua kukagua mwenyewe vitu vinavyotakiwa kuwepo katika computer husika .

Mwisho kama unaona shida sana unaweza kudownload www.belarc.com programu hii unaweza kuingiza katika computer yako na itakupa taarifa zaidi kuhusu computer hiyo bila kufungua ndani .

Sasa kama ina utata aina ya maiboard haitaandikwa , au serial number za mainboard hazitaandikwa .

Mwisho wa siku ni wewe mwenyewe mwenye hela ndio mwamuzi wa mwisho katika manunuzi ya vitu vyako , kama unataka ubora na ufanisi katika kazi zako ni vizuri ununue bidhaa ambazo ni halali kwa bei halali na kwa watu halali .
 
Back
Top Bottom