NECTA ya Ndalichako iheshimu wadau wake

NECTA ya Ndalichako iheshimu wadau wake

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Joined
Feb 25, 2013
Posts
1,457
Reaction score
699
NECTA YA NDALICHAKO IHESHIMU WADAU WAKE
Ndugu wadau wa JF, hii taasisi ya Necta haina heshima hata kidogo kwa wadau wake. Kauli zake kwa watahiniwa, wasimamizi na wasahihishaji ni chafu sana.

Wadau wa Necta ni watahiniwa ambao wametapakaa nchi nzima. Hivyo Necta yenyewe ina jukumu la kuwasiliana nao ili utendaji wa kazi zake uwe mzuri. Ikiwa wateja wake wanafeli mara kwa mara, Necta inajukumu la kutafiti ili kujua ni kwa nini. Hii ndio maana ya kuwa na madaktari wa taaluma katika kituo hicho. Madaktari hao kazi zao ni kutoa ufumbuzi wa matatizo na sio tu kuwa wanatoa huduma katika kituo.

Ukiona Daktari ana matusi na dharau na shughuli zake ni uwasilishaji wa kazi za kila siku, hicho ni kipimo kuwa elimu yake ni kanjanja.

Necta ina mazoea ya kutoa majibu mepesi kwa kupuuza wanafunzi na wazazi wao huku wakijiridhisha kuwa wanafanya kazi vizuri. Majibu yanayotolewa dhidi ya kufeli kwa wanafunzi na Necta ni eti:

  • Wanafunzi wa siku hizi hawasomi
  • Wazazi hawajui kuwasaidia watoto wao
  • Wanafunzi wanakesha kwenye mitandao mibaya

Kama hiyo haitoshi, mdau mmoja wa Elimu, alisema wanafunzi kufeli ni kwa sababu shule hazina maabara. Sasa, je, masomo ya Kiswahili na Civics yanahitaji maabara?

Necta inatakiwa kufanya tafiti ili kujua ni vipi mitihani inawatatiza wanafunzi na kufanya mawasiliano ya kitaaluma ya kutatua matatizo hayo. Tunataka tafiti za kielimu zinazoonyesha masomo na maeneo magumu na ufumbuzi wake kila mwaka.

Necta ina madaktari/wataalamu ambao hawafanyi kazi za msingi za utafiti, hivyo hawana msaada kwa Taifa. Hawafai kuongoza taasisi nyeti kama Necta. Wanatakiwa waondoke mara moja wakafanye shughuli zisizohitaji taaluma.
 
Inaelekea hizo ni hasira za kuwa na ndugu aliyepata ZERO. Mwamko wa kusimamia elimu umekufa kuanzia ngazi ya Familia hadi kwa wenye dhamana kuu ya kusimamia. Tafuta muda angalia kipindi cha SKONGA kinachirushawa na EATV hasa kipengele cha Questions and Answers uone wanafunzi tulionao.
 
Ni kweli mkuu mwambie aangalie aone hao wanafunzi wa secondari walivyo vilanza..!
 
Unataka kuuaminisha kwamba kufeli kwa wanafunzi kunatoka na majibu ya NECTA Kwa waliofeli?
 
Mtoa maada inaelekea, ama hujui kazi za NECTA, ama unapuuza kwa kuwa una mtoto aliyefanya mtihani mwaka jana. Kazi ya Necta, pamoja na mambo mengine ni kutathmini ubora wa Elimu itolewayo nchini kwa njia ya mitihani kwa ngazi mbali mbali za elimu. Kazi ya kusimamia ubora wa Elimu ni ya vyombo vingine vya wizara ya Elimu. Kama NECTA watatunga mitihani nje ya mihutasari inayofundishiwa watastahili lawama; lakini kama wanatunga maswali sawasawa na mihtasari, lawama kwao za nini?! Kazi yao ni kuonesha hali halisi, basi. Usilete siasa hapa!
 
Mtoa mada hujui hata majukumu ya Necta,au ni hasira za wadogo zako kupiga zero,jipangeni find out alternatives,dogo langu nilikuwa nalisimamia mwenyewe limepiga 2,endeleeni kulalamika tu wakati nyie wenyewe hamuwajibiki.
 
Je wewe Kizaizai wanafunzi wote nchini wakipata zero utafurahi? Wewe ukoje? Au elimu yako duni?
 
hakuna sababu ya kuomba utungwe Mtihani rahisi ili watoto wafaulu, sisi sote tunajukumu la kusimamia kwa karibu elimu ya watoto wetu kama tuna nia ya dhati ya kuboresha elimu lakini tukisubiri Wizara tutarajie haya tunayoyaona kwani waheshimiwa wanawapeleka watoto wao nje ya nchi
 
Eti Ndalichako naye anaweza kuja hadharani na kuisema radio fulani na kusikilizwa!
 
Ni kweli mkuu mwambie aangalie aone hao wanafunzi wa secondari walivyo vilanza..!

pamoja na hayo, mwambie aangalie na jinsi wanavyotumia muda mwingi katika kujifunza jinsi ya kuonyesha shoo kwenye hicho kipindi. lakini inavyokuja Q&A Section wanafunzi wengi wanajificha.
 
Wizara imejsahau kuwa kumebadlka mbinu ya ufundshaj wanafunz kwa hyo necta inaenda na mabadllo hayo. tatzo ni kwa wirara kutotoa mafunzo kwa walmu walong co ha2po kwny teacher centred approach, now 2po kwny learner centred app. ili m/funz kjtegemea.
 
UKLAUM, JUA PA KUANZIA. Content based syllabu imepitwa na wakat now 2po kwny paradigm of shift. NECTA ina2nga mitihan kupima uelewa wa mwanafunz na co alcho kalili/kufundswa. mie km mwl ctakiw kumlsha mwanafunz bal ajtafutie na ajtegemee ktk akiri
 
NECTA YA NDALICHAKO IHESHIMU WADAU WAKE
Ndugu wadau wa JF, hii taasisi ya Necta haina heshima hata kidogo kwa wadau wake. Kauli zake kwa watahiniwa, wasimamizi na wasahihishaji ni chafu sana.

Wadau wa Necta ni watahiniwa ambao wametapakaa nchi nzima. Hivyo Necta yenyewe ina jukumu la kuwasiliana nao ili utendaji wa kazi zake uwe mzuri. Ikiwa wateja wake wanafeli mara kwa mara, Necta inajukumu la kutafiti ili kujua ni kwa nini. Hii ndio maana ya kuwa na madaktari wa taaluma katika kituo hicho. Madaktari hao kazi zao ni kutoa ufumbuzi wa matatizo na sio tu kuwa wanatoa huduma katika kituo.

Ukiona Daktari ana matusi na dharau na shughuli zake ni uwasilishaji wa kazi za kila siku, hicho ni kipimo kuwa elimu yake ni kanjanja.

Necta ina mazoea ya kutoa majibu mepesi kwa kupuuza wanafunzi na wazazi wao huku wakijiridhisha kuwa wanafanya kazi vizuri. Majibu yanayotolewa dhidi ya kufeli kwa wanafunzi na Necta ni eti:

  • Wanafunzi wa siku hizi hawasomi
  • Wazazi hawajui kuwasaidia watoto wao
  • Wanafunzi wanakesha kwenye mitandao mibaya

Kama hiyo haitoshi, mdau mmoja wa Elimu, alisema wanafunzi kufeli ni kwa sababu shule hazina maabara. Sasa, je, masomo ya Kiswahili na Civics yanahitaji maabara?

Necta inatakiwa kufanya tafiti ili kujua ni vipi mitihani inawatatiza wanafunzi na kufanya mawasiliano ya kitaaluma ya kutatua matatizo hayo. Tunataka tafiti za kielimu zinazoonyesha masomo na maeneo magumu na ufumbuzi wake kila mwaka.

Necta ina madaktari/wataalamu ambao hawafanyi kazi za msingi za utafiti, hivyo hawana msaada kwa Taifa. Hawafai kuongoza taasisi nyeti kama Necta. Wanatakiwa waondoke mara moja wakafanye shughuli zisizohitaji taaluma.

Nikifanikiwa kuoanisha tittle na content nitarudi kuchangia!

Je wewe Kizaizai wanafunzi wote nchini wakipata zero utafurahi? Wewe ukoje? Au elimu yako duni?

Kama watoto hawaandaliwi vizuri lazima watapata sifuri. Sasa NECTA ina andaa watoto au inatahini kujua kama watoto wameandaliwa? Mwenzetu ulisoma wapi sijui.
 
Mtoa mada hujui hata majukumu ya Necta,au ni hasira za wadogo zako kupiga zero,jipangeni find out alternatives,dogo langu nilikuwa nalisimamia mwenyewe limepiga 2,endeleeni kulalamika tu wakati nyie wenyewe hamuwajibiki.

Moja ya majukum ya NECTA ambayo hufanywa kwa makusudi ni si uzalendo hata kidogo ni kutokuwa na mfumo sahihi wa GRADING unaojulikana kwa wadau wote nchini. Ndarichako na timu yake aeleze kwanini grading zinakuwa tofauti?
Siku moja nilikuwa ninaongea na Mwalimu mmoja ambaye huwa anahudhuria sana kusahihisha mitihani alisema kuwa wasahihishaji wanapomaliza kusahihisha matokeo yote yanakuwa yako tayari kwani wao wenyewe ndio huingiza data kwenye hiyo system ya NECTA ambayo haina grading. kwanini grading isiwekwe hapo hapo kwenye hiyo system? kwa nini kuwe na timu ya kutunuku? enzi za ujima hii tume ya kutunuku ndiko ingetumika na sii sasa hivi enzi za digital. hakuna sababu ya matokeo kucheleweshwa na wakati ukiingiza marks 56 inajulikana ni C moja kwa moja. Dhambi wanayoichuma kwa kuwanyonga watoto kimaisha ni kubwa mno.
 
Back
Top Bottom