Necta ya ndalichako iheshimu wadau wake

Papaa Kinyani

JF-Expert Member
Feb 25, 2013
1,459
697
NECTA YA NDALICHAKO IHESHIMU WADAU WAKE
Ndugu wadau wa JF, hii taasisi ya Necta haina heshima hata kidogo kwa wadau wake. Kauli zake kwa watahiniwa, wasimamizi na wasahihishaji ni chafu sana.

Wadau wa Necta ni watahiniwa ambao wametapakaa nchi nzima. Hivyo Necta yenyewe ina jukumu la kuwasiliana nao ili utendaji wa kazi zake uwe mzuri. Ikiwa wateja wake wanafeli mara kwa mara, Necta inajukumu la kutafiti ili kujua ni kwa nini. Hii ndio maana ya kuwa na madaktari wa taaluma katika kituo hicho. Madaktari hao kazi zao ni kutoa ufumbuzi wa matatizo na sio tu kuwa wanatoa huduma katika kituo.

Ukiona Daktari ana matusi na dharau na shughuli zake ni uwasilishaji wa kazi za kila siku, hicho ni kipimo kuwa elimu yake ni kanjanja.

Necta ina mazoea ya kutoa majibu mepesi kwa kupuuza wanafunzi na wazazi wao huku wakijiridhisha kuwa wanafanya kazi vizuri. Majibu yanayotolewa dhidi ya kufeli kwa wanafunzi na Necta ni eti:

  • Wanafunzi wa siku hizi hawasomi
  • Wazazi hawajui kuwasaidia watoto wao
  • Wanafunzi wanakesha kwenye mitandao mibaya

Kama hiyo haitoshi, mdau mmoja wa Elimu, alisema wanafunzi kufeli ni kwa sababu shule hazina maabara. Sasa, je, masomo ya Kiswahili na Civics yanahitaji maabara?

Necta inatakiwa kufanya tafiti ili kujua ni vipi mitihani inawatatiza wanafunzi na kufanya mawasiliano ya kitaaluma ya kutatua matatizo hayo. Tunataka tafiti za kielimu zinazoonyesha masomo na maeneo magumu na ufumbuzi wake kila mwaka.

Necta ina madaktari/wataalamu ambao hawafanyi kazi za msingi za utafiti, hivyo hawana msaada kwa Taifa. Hawafai kuongoza taasisi nyeti kama Necta. Wanatakiwa waondoke mara moja wakafanye shughuli zisizohitaji taaluma.
 
Back
Top Bottom