NECTA na matokeo: Kwanini mnaonesha majina? | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NECTA na matokeo: Kwanini mnaonesha majina?

Discussion in 'Jukwaa la Elimu (Education Forum)' started by JAYJAY, Oct 7, 2011.

 1. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #1
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,486
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  mara nyingi nimekuwa nikijiuliza kwa nini baraza la mitihani la Taifa linaonesha majina ya watahiniwa wakati wa kutoa matokeo. mimi kwa mtazamo wangu naona matokeo ya mtahiniwa ni siri kati yake na baraza (au mwalimu na mwanafunzi) au pia mtu/watu ambao mtahiniwa ameridhia au anawajibika kwake/kwao. kwenye vyuo, zamani kabla ya kuenea kwa huduma za mawasiliano ya internet walikuwa wanaweka matokeo ya wanafunzi kwa karatasi zenye kuonesha namba tu za watahiniwa na matokeo yao, ambapo kwa sasa mwanafuzi anakuwa na account yake kwa internet ambapo huweza kuangalia matokeo yake popote pale alipo kwenye huduma hiyo. baraza la mitihani linaweka matokeo kwenye website yake ambayo yana majina ya watahiniwa, nadhani wangebadilisha utaratibu na kuweka namba tu ya mtahiniwa na matokeo yake, na hiki kitu walikifanya kama miaka 3 iliyopita (sina uhakika), sasa sijui kwa nini wamerudia tena huu mfumo wa kuanika majina ya watahiniwa, anayefahamu anaweza kunielewesha. hii inachochea watu kufatilia hata matokeo ya watu yasiyowahusu kwenye mitandao kisa tu wanaishi mtaa mmoja au sababu nyingine za kijinga, na pia inasababisha mateso ya kisaikolojia na aibu kwa familia hasa kwa wale wanafunzi wenye matokeo mabaya. wangesambaza vitabu vyenye majina na matokeo huko mashuleni kisha kwenye website waweke namba na matokeo tu, mwanafunzi mwenye wasiwasi na matokeo yake anaweza kuwasiliana na shule yake kwa uthibitisho.
   
 2. rfjt

  rfjt Senior Member

  #2
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 29, 2011
  Messages: 184
  Likes Received: 13
  Trophy Points: 35
  utaratibu wa sasa ni sawa kwani umeturahisishia sisi wazazi na walezi kufuatilia matokeo ya watoto wetu kwa urahisi. Awali tulikuwa tunadaganywa kwa kupewa namba za uongo na hivyo kutojua matokeo. Njia nzuri ya kuondokana na aibu ni kujitahidi katika masomo.
  Utaratibu huu wa sasa ni mzuri na uendelee.
   
 3. B

  Bajabiri JF-Expert Member

  #3
  Oct 7, 2011
  Joined: Jan 1, 2011
  Messages: 9,755
  Likes Received: 27
  Trophy Points: 0
  Kuna watu hapa nilipo wanafanya mtihan wa taifa,,,,,lakin ukimuuliza wewe INDEX NO:YAKO NGAPI HAKUMBUKI,,,,JE WAKIWEKA NAMBA KWENYE MATOKEO,,,,UNADHAN ITAKUWAJE????na wapo ambao wanajikuta wanaandika namba si zao,,,so mfumo wa majina uko palepale,hata wakitoa kwa namba still utaona tu
   
 4. C

  CHUAKACHARA JF-Expert Member

  #4
  Oct 7, 2011
  Joined: Jun 3, 2011
  Messages: 12,200
  Likes Received: 3,810
  Trophy Points: 280

  Umesema jambo la msingi sana. Matokeo ni siri ya mtu, ni sawa na ugonjwa wa mtu huwa ni siri kubwa. Baraza la mitihani liangalie na mlifanyie kazi. One's exam results is not for public consumption at all. Mimi nitakwenda mahakamani kuomba baraza la mitihani lipewe order ya kutotoa majina ya watu kwenye internet. Namba zinatosha kwa mhusika kujua matokeo basi.
   
 5. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #5
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,486
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  kwani wazazi wa wanafunzi zamani walikuwa wanafuatilia vipi? mzazi asiyefuatilia maendeleo ya mtoto wake ndiye anayeweza kudanganywa tuu!
   
 6. JAYJAY

  JAYJAY JF-Expert Member

  #6
  Oct 7, 2011
  Joined: Oct 31, 2008
  Messages: 2,486
  Likes Received: 822
  Trophy Points: 280
  ndio maana nikatoa ushauri kuwa vitabu vyenye majina na matokeo vipelekwe mashuleni huku kwenye mtandao ibaki namba tu! huyo anayesahau namba atapaswa kwenda au kuwasiliana na shule yake!
   
 7. t

  torres0909 Member

  #7
  Oct 7, 2011
  Joined: Feb 22, 2011
  Messages: 42
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 15
  Dawa ni kusoma tu, kwanini ufiche.
   
 8. Mrimi

  Mrimi JF-Expert Member

  #8
  Oct 7, 2011
  Joined: Jul 18, 2011
  Messages: 1,673
  Likes Received: 75
  Trophy Points: 145
  Biafsi sioni tatizo lolote kuweka wazi majina. Mbona kuna wazazi wengine hufanya party kwa ajili ya kuwapongeza wanao wanapokuwa wamefanya vizuri, mkialikwa mbona tunakwenda, hatusemi ni siri yake? Hii ni self defense kwa wanafunzi wavivu darasani.Sina hakina ni miaka ni miaka mitatu gani unayosema,lakini nachoelewa ni kwamba tangu kuanzia mwishoni mwa miaka ya 90 majina yalikuwa yakichapishwa kwnye magazeti bila malalamiko yoyote. Tunasahau magazeti yanavyonunuliwa baada ya matokeo kutoka. OK, fine kama unaona matokeo ni udhalilishaji basi,huna haja ya kununua magazeti yale wala kuingia kwenye website ya NECTA.Mimi naona ni msaada kwa wanafunzi zaidi ya hivyo tunavyofikiria. Unamfikiriaje mtoto wa masikini aliyemaliza shule Newala halafu akarudi kwao Biharamulo,kipi rahisi kati ya kununua gazeti au kwenda internet cafe kwa Tsh 500 au kusafiri kuendea matokeo yake Mtwara kisha kurudi tena Kagera kujiandaa kwa hatua nyingine inayofuata??? Jiongeze!!!!!!!!!!!!!!!!!!!
   
 9. U

  Ulimakafu JF-Expert Member

  #9
  Oct 7, 2011
  Joined: Mar 18, 2011
  Messages: 17,966
  Likes Received: 723
  Trophy Points: 280
  Naona ni sawa kurahisisha,kwa chuo watumie namba.
   
 10. R

  Rajo Member

  #10
  Oct 7, 2011
  Joined: Sep 26, 2011
  Messages: 21
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Umenena mwn,kw hao wanaotaka namba pekee wafanye bdii km hawatak aibu pia watoto wa cku hz wanapenda starehe kulko kusoma so matokeo na majina ndo mpango mzima cz unaleta maendeleo makubwa sn ktk elimu.
   
 11. OMGHAKA

  OMGHAKA Member

  #11
  Oct 7, 2011
  Joined: Aug 15, 2011
  Messages: 99
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Hivi hebu fikiria matokeo yako umejenga vibanda (kibanda= A) 7 au 9 na jina lako linatokea wenzako wote wanaona, utajisikia vipi? Kuandika Jina ni motisha pia kuwafanya msome kwa bidii, huku wavivu wakiadhibiwa kwa kupokea funguo hadharani.
   
Loading...