NEC yatoa ufafanuzi juu ya mgombea wa CHADEMA jimbo la Singida Kaskazini, aliyetangaza kujitoa kwenye Uchaguzi

Weka panga na mtutu pembeni Kwanza halafu ndo tuongee siasa unataka kutengeza akina ben saa 8, daudi mwangosi, mawazo nk wangapi??? They were real people just like you and l. who cares about their families now
Futeni basi na chama watanzania wajue hakuna upinzani,,, au mnamalizia ruzuku mpk 2020. Shame
 
Miaka yote wasipigwe mapanga, kwa nn leo.. Mnasingizia mapanga wakati mnajua watz washawachoka
Watanzania hawawezi kuwachoka CHADEMA kwa sababu hawahusiki na nchi kutokuwa na maji wala umeme, mahitaji ya msingi kabisa kwa binadamu.
 
Hivi haki ya wananchi wanaoisapot cdm inanyang'anywa na ubabe wa viongozi,, eti kususia uchaguzi...
No. Wanataka Chama tawala kipate ushindi kwa urahisi. Kwani kuna tatizo tena hapo mkuu? Kama hamtaki kupingwa kwa hoja, mtakubalije kupingwa kwenye uchaguzi?
 
Hivi haki ya wananchi wanaoisapot cdm inanyang'anywa na ubabe wa viongozi,, eti kususia uchaguzi...
Mjinga haki gani ya wananchi unayoililia? Unataka watu wateswe wapigwe ndio haki hiyo? Acha CCM wajichukulie hicho kiti, mbona mnazungumzia Singida tu, Longido vipi mbona yuko kimya huyo mkurugenzi wa NEC?
 
Kwa hiyo mugabe kateuliwa na rais kuongoza miaka 14 na matamko ya kususia uchaguzi???
Ukiongelea Mugabe sisi, tunajua ni Sizonje au mshambadilisha kufananisha na Mugabe? Duh mnahatari sana, lakini mwisho utafika hakuna jiwe litakalo salia juu ya jiwe.
 
Miaka yote wasipigwe mapanga, kwa nn leo.. Mnasingizia mapanga wakati mnajua watz washawachoka
Sasa kama wametuchoka jitangazeni, shida ya nini? NEC - CCM, POLISI - CCM, WAKURUGENZI- CCM, WATENDAJI WA KATA - CCM, MSAJILI - CCM sasa mnataka UKAWA waweke mgombea hapo kweli, atapitishwa akishinda?
 
Kwanini huyu kailima analazimisha CHADEMA wasimamishe mgombea
kama wenyewe wamesema wanajitoa si awakubalie tu njaa za wanaume wa tanzania zinatia aibu ila Mbowe naye ni shida sana apumzike awaachie chama vijana,anatia mashaka sana kwenye maamuzi yake na timu nzima CHADEMA hamko makini kabisa this time around aisee.
Ameagizwa alazimishe wagombea baada ya kuona hawatoshi.
 
Kwanini huyu kailima analazimisha CHADEMA wasimamishe mgombea
kama wenyewe wamesema wanajitoa si awakubalie tu njaa za wanaume wa tanzania zinatia aibu ila Mbowe naye ni shida sana apumzike awaachie chama vijana,anatia mashaka sana kwenye maamuzi yake na timu nzima CHADEMA hamko makini kabisa this time around aisee.
Kama umesoma vizuri mwisho anasema mgombea ana haki ya kujitoa ila kuna taratibu lazima zifuatwe.

Na nahisi Joseph Jumbe ameshafuata taratibu za kujitoa maana nimeona barua za kujitoa zimesambaa kwenye mitandao mkuu.
 
Futeni basi na chama watanzania wajue hakuna upinzani,,, au mnamalizia ruzuku mpk 2020. Shame
Chadema wapuuzi wanakomalia taratibu za chama chao badala ya sheria inavyosema.Mkurugenzi wa uchaguzi yuko sahihi kwa mujibu wa sheria huyo mgombea wa Chadema ni mgombea halali kabisa kisheria
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeeleza kuwa inawashangaa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaosema kuwa hawamtambui mgombea wa ubunge aliyesimamishwa kugombea katika jimbo la Singida Kaskazini.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima ameeleza kuwa CHADEMA kupitia Katibu wa Wilaya wa Singida Vijijini wamekamilisha mchakato wa utambulisho wa mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini, Joseph Njumbe

“Halmashauri ya Wilaya ya singida wagombea 6 wameteuliwa juzi mmojawapo akiwa bwana Joseph Njumbe wa CHADEAMA. Ameteuliwa kwa sababu amekidhi vigezo vya kikatiba, kisheria na kikanuni yeye na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo.”

“Kwa hiyo wanapolalamika kwamba huyu hawamjui nawashangaa sana. Nawashangaa sana kwa saababu Kwa mujibu wa ibara ya 67 ibara ndogo ya 1b ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Mgombea yeyote wa ubunge lazima awe amependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa.”

“Kanuni namba 31 kanuni ndogo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2015, inasema mtu akitaka kugombea ubunge atawasilisha barua yake ya utambulisho iliyosainiwa na katibu wa chama au wa wilaya wa chama husika. Barua yake inawasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi.”

“Huyu Bwana David Joseph Njunbe amewasilisha barua hiyo ya utambulisho iliyosainiwa na katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Singida Vijijini, Bwana Amani M mloya,” amesema Kailima.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Kailima Ramadhani amesema kuwa kwa kupitia kanuni na vigezo vya sheria ya uchaguzi, Mgombea huyo wa CHADEMA amekidhi vigezo vyote vilivyohitajika ili kupitishwa kugombea Ubunge katika jimbo hilo.

Aidha, Kailima ameeleza kuwa Joseph Njumbe, pamoja na kuwa ameshakamilisha taratibu za kupitishwa kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, bado ana haki ya kikatiba ya kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho pale tu atakapotimiza taratibu zinazotakiwa ili kujiondoa.

Kailima aliongeza kuwa Tume ya Uchaguzi haiangalii

“Sisi hatuangalii muhtasari wa kamati kuu ama hatuangalii katiba iliyosajiliwa na Katibu Mkuu wa chama chochote cha siasa. Tunaangalia barua iliyosainiwa na Katibu wa Chama wa Mkoa ama Katibu wa Chama wa Wilaya na ni kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo,” amesema Kailima.

CHADEMA pamoja na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vilitangaza kutokushiriki uchaguzi huo mdogo wa wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Januari 18, 2018 ikidai kuwa mwenendo wa hali ya kisiasa nchini siyo shwari na kuitaka Tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi huo.

Jana CHADEMA kupitia Mkuu wake wa Idara ya Mawasiliano, Tumaini Makene ilitoa taarifa kuwa hakijateua mgombea wa ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini na kumtaka Ndugu. Ramadhani Kailima kutambua kwamba mchakato wa uteuzi wa mgombea wa ubunge ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati kuu ya Chama hicho.

Chanzo: Mwananchi
Mngekuwa hamjapanga kuiba mngematalia na kusema amekosea kujaza fomu au katibu mkuu taifa hajasaini fomu yaani figisufigisu kibao ili asigombee. Ila kwa vile CHADEMA wamesema hawashiriki mnalazimisha kumpitisha mgombea ili ionekane Chadema wanashiriki. Kapilima nawe ni bomu ambalo kuna cku utaipata hata kama si wewe familia yako tutalala nao mbele. Tunajua yana mwisho. Wahenga walisema hakuna marefu yasiyokuwa na mwisho. Tutaanza kudeal na familia zenu pmj na kuwa mnalindwa na wanyarwanda tutawapata tu. Njia iliyopo ni kudeal na familia zenu
 
Kama umesoma vizuri mwisho anasema mgombea ana haki ya kujitoa ila kuna taratibu lazima zifuatwe.

Na nahisi Joseph Jumbe ameshafuata taratibu za kujitoa maana nimeona barua za kujitoa zimesambaa kwenye mitandao mkuu.
Sheria inasema wazi akitaka kujitoe ana kwenda kula kiapo mbele ya hakimu na barua ya kiapo ina sainiwa na hakimu, kwa hiyo kama hana kiapo cha hakimu basi hajajitoa......
Chadema ni chama cha ajabu sana hasa ukiangalia comments za mashabiki wao yani ni wazi hawasomi habari...
 
Na sisi wapiga kura tunawashangaa NEC. Wanadhani kuwa ccm ni bora kuliko maisha ya watu? Ama siasa ni bora kuliko maisha ya watu?
Shame on them!
 
Kwani lazima kusimamisha wao ccm wana homa gani bila chadema. Cdm wamesema hatushiriki hadi kanuni za tume zifuatwe.
Wenye chama ni kamati kuu kama kaonewa aende vyama vingine.
CHADEMA haishiriki kwa kuwa hawana fedha ya kugharamia mchakato wa uchaguzi. Kama fedha ya ruzuku haiwezi kujenga hata ofisi ya makao makuu, kitakuwa na fedha yakushiriki uchaguzi? Uongozi ukibanwa sana kuhusu matumizi ya ruzuku utakuja na dai kwamba imetumika kumtibia Mh Lissu baada ya Serikali kumtelekeza.

Pia uongozi wa CHADEMA umekwisha kutambua kuwa kutumia shambulio la Mh Lissu, hata Mkoani kwake siyo mtaji wa kisiasa baada ya kufanya hivyo na kupoteza kata ya marudio huko jimboni.

PICHA YA RAIS HAINA MLINZI (body guard)
 
Back
Top Bottom