• Mpendwa mteja, tunakusihi jitahidi kuosha mikono kwa maji safi na sabuni mara kwa mara na kwa siku chache hizi jaribu kutulia nyumbani kuepusha maambukizi ya #CORONAVIRUS

NEC yatoa ufafanuzi juu ya mgombea wa CHADEMA jimbo la Singida Kaskazini, aliyetangaza kujitoa kwenye Uchaguzi

figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined
Oct 17, 2010
Messages
16,639
Points
2,000
figganigga

figganigga

JF-Expert Member
Joined Oct 17, 2010
16,639 2,000
Tume ya Taifa ya Uchaguzi imeeleza kuwa inawashangaa viongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) wanaosema kuwa hawamtambui mgombea wa ubunge aliyesimamishwa kugombea katika jimbo la Singida Kaskazini.

Mkurugenzi wa Uchaguzi wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi, Ramadhan Kailima ameeleza kuwa CHADEMA kupitia Katibu wa Wilaya wa Singida Vijijini wamekamilisha mchakato wa utambulisho wa mgombea wa Ubunge jimbo la Singida Kaskazini, Joseph Njumbe

“Halmashauri ya Wilaya ya singida wagombea 6 wameteuliwa juzi mmojawapo akiwa bwana Joseph Njumbe wa CHADEAMA. Ameteuliwa kwa sababu amekidhi vigezo vya kikatiba, kisheria na kikanuni yeye na chama chake cha Demokrasia na Maendeleo.”

“Kwa hiyo wanapolalamika kwamba huyu hawamjui nawashangaa sana. Nawashangaa sana kwa saababu Kwa mujibu wa ibara ya 67 ibara ndogo ya 1b ya katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inasema Mgombea yeyote wa ubunge lazima awe amependekezwa na chama cha siasa kilichosajiliwa.”

“Kanuni namba 31 kanuni ndogo ya kwanza ya uchaguzi wa Rais na wabunge ya mwaka 2015, inasema mtu akitaka kugombea ubunge atawasilisha barua yake ya utambulisho iliyosainiwa na katibu wa chama au wa wilaya wa chama husika. Barua yake inawasilishwa kwa msimamizi wa uchaguzi.”

“Huyu Bwana David Joseph Njunbe amewasilisha barua hiyo ya utambulisho iliyosainiwa na katibu wa CHADEMA wa Wilaya ya Singida Vijijini, Bwana Amani M mloya,” amesema Kailima.

Mkurugenzi wa Uchaguzi NEC, Kailima Ramadhani amesema kuwa kwa kupitia kanuni na vigezo vya sheria ya uchaguzi, Mgombea huyo wa CHADEMA amekidhi vigezo vyote vilivyohitajika ili kupitishwa kugombea Ubunge katika jimbo hilo.

Aidha, Kailima ameeleza kuwa Joseph Njumbe, pamoja na kuwa ameshakamilisha taratibu za kupitishwa kuwa mgombea wa ubunge kwa tiketi ya CHADEMA, bado ana haki ya kikatiba ya kujiondoa katika kinyang’anyiro hicho pale tu atakapotimiza taratibu zinazotakiwa ili kujiondoa.

Kailima aliongeza kuwa Tume ya Uchaguzi haiangalii

“Sisi hatuangalii muhtasari wa kamati kuu ama hatuangalii katiba iliyosajiliwa na Katibu Mkuu wa chama chochote cha siasa. Tunaangalia barua iliyosainiwa na Katibu wa Chama wa Mkoa ama Katibu wa Chama wa Wilaya na ni kwa mujibu wa sheria, kanuni na maelekezo,” amesema Kailima.

CHADEMA pamoja na vyama vingine vinavyounda Umoja wa Katiba ya Wananchi (UKAWA) vilitangaza kutokushiriki uchaguzi huo mdogo wa wabunge na madiwani unaotarajiwa kufanyika Januari 18, 2018 ikidai kuwa mwenendo wa hali ya kisiasa nchini siyo shwari na kuitaka Tume ya uchaguzi kuahirisha uchaguzi huo.

Jana CHADEMA kupitia Mkuu wake wa Idara ya Mawasiliano, Tumaini Makene ilitoa taarifa kuwa hakijateua mgombea wa ubunge katika Jimbo la Singida Kaskazini na kumtaka Ndugu. Ramadhani Kailima kutambua kwamba mchakato wa uteuzi wa mgombea wa ubunge ndani ya CHADEMA linasimamiwa na Kamati kuu ya Chama hicho.

Chanzo: Mwananchi
======================

 
L

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined
Jul 14, 2015
Messages
10,032
Points
2,000
L

laki si pesa.

JF-Expert Member
Joined Jul 14, 2015
10,032 2,000
CHADEMA chama cha hovyo sana yaani viongozi wa makao makuu hawana mawasiliano na viongozi wa wilaya hiki chama bora kifutwe tu kinatia aibu sana
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
14,114
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
14,114 2,000
Kwanini huyu kailima analazimisha CHADEMA wasimamishe mgombea
kama wenyewe wamesema wanajitoa si awakubalie tu njaa za wanaume wa tanzania zinatia aibu ila Mbowe naye ni shida sana apumzike awaachie chama vijana,anatia mashaka sana kwenye maamuzi yake na timu nzima CHADEMA hamko makini kabisa this time around aisee.
 
MLA PANYA SWANGA

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined
Jul 31, 2015
Messages
4,525
Points
2,000
MLA PANYA SWANGA

MLA PANYA SWANGA

JF-Expert Member
Joined Jul 31, 2015
4,525 2,000
Kwani lazima kusimamisha wao ccm wana homa gani bila chadema. Cdm wamesema hatushiriki hadi kanuni za tume zifuatwe.
Wenye chama ni kamati kuu kama kaonewa aende vyama vingine.
 
W

wa mchangani

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Messages
1,426
Points
2,000
W

wa mchangani

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2017
1,426 2,000
Hawa viongozi wanaoteuliwa na rais na wa ovyo sana,kazi yao ni kuchochea tu,no professionalism, inatia hasira sana
 
W

wa mchangani

JF-Expert Member
Joined
Feb 23, 2017
Messages
1,426
Points
2,000
W

wa mchangani

JF-Expert Member
Joined Feb 23, 2017
1,426 2,000
Kwa hiyo mugabe kateuliwa na rais kuongoza miaka 14 na matamko ya kususia uchaguzi???
Ujumbe umefika ndo maana umejibu ingawa umejibu ki ccm
 
E

excellentone

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
725
Points
500
E

excellentone

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
725 500
kwanini huyu kailima analazimisha chadema wasimamishe mgombea
kama wenyewe wamesema wanajitoa si awakubalie tu
njaa za wanaume wa tanzania zinatia aibu
ila mbowe naye ni shida sana
apumzike awaachie chama vijana,anatia mashaka sana kwenye maamuzi yake na timu nzima
chadema hamko makini kabisa this time around aisee
Una akili dhaifu sana wewe. Nani kakwambia kwenye safu ya maamuzi cdm hamna vijana na huyo mbowe una bifu nae la nini?
 
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Messages
14,114
Points
2,000
nyabhingi

nyabhingi

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2010
14,114 2,000
Una akili dhaifu sana wewe. Nani kakwambia kwenye safu ya maamuzi cdm hamna vijana na huyo mbowe una bifu nae la nini?
mbowe amekifanyia chama mengi na naukubali sana mchango wake
lakini he is done,amechoka kiakili na kimwili,awapasie wengine kijiti..cdm wamekuwa a bunch of cowards these days
the fact
 
E

excellentone

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
725
Points
500
E

excellentone

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
725 500
Miaka yote wasipigwe mapanga, kwa nn leo.. Mnasingizia mapanga wakati mnajua watz washawachoka
Weka panga na mtutu pembeni Kwanza halafu ndo tuongee siasa unataka kutengeza akina ben saa 8, daudi mwangosi, mawazo nk wangapi??? They were real people just like you and l. who cares about their families now
 
E

excellentone

JF-Expert Member
Joined
Aug 28, 2017
Messages
725
Points
500
E

excellentone

JF-Expert Member
Joined Aug 28, 2017
725 500
mbowe amekifanyia chama mengi na naukubali sana mchango wake
lakini he is done,amechoka kiakili na kimwili,awapasie wengine kijiti..cdm wamekuwa a bunch of cowards these days
the fact
Hujui vizuri siasa za Tanzania wewe hatakiwi kiongozi mkakamavu bali asie nunulika
 
barafuyamoto

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2014
Messages
27,194
Points
2,000
barafuyamoto

barafuyamoto

JF-Expert Member
Joined Jul 26, 2014
27,194 2,000
Kwanini huyu kailima analazimisha CHADEMA wasimamishe mgombea
kama wenyewe wamesema wanajitoa si awakubalie tu njaa za wanaume wa tanzania zinatia aibu ila Mbowe naye ni shida sana apumzike awaachie chama vijana,anatia mashaka sana kwenye maamuzi yake na timu nzima CHADEMA hamko makini kabisa this time around aisee.
Umesoma na kuelewa alichosema kailima??
 
M

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined
Nov 29, 2011
Messages
2,981
Points
2,000
M

Malata Junior

JF-Expert Member
Joined Nov 29, 2011
2,981 2,000
Hivi haki ya wananchi wanaoisapot cdm inanyang'anywa na ubabe wa viongozi,, eti kususia uchaguzi...
Mbona ccm wamesusia uchaguzi wa spika wa bunge la Afrika Mashariki na kusababisha mgombea wenu kupata kura 0?
 
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2011
Messages
30,326
Points
2,000
jingalao

jingalao

JF-Expert Member
Joined Oct 12, 2011
30,326 2,000
Kwanini huyu kailima analazimisha CHADEMA wasimamishe mgombea
kama wenyewe wamesema wanajitoa si awakubalie tu njaa za wanaume wa tanzania zinatia aibu ila Mbowe naye ni shida sana apumzike awaachie chama vijana,anatia mashaka sana kwenye maamuzi yake na timu nzima CHADEMA hamko makini kabisa this time around aisee.
kuna sehemu amemkatalia kujitoa?
 

Forum statistics

Threads 1,403,857
Members 531,397
Posts 34,436,601
Top