Uchaguzi 2020 NEC yatoa ratiba ya mwisho: Lissu atafungia Dar, Magufuli Dodoma

Sera mbadala zipo, Ila masikio yako na hisia zako zimejikita zaidi kwenye mambo yanayokuumiza ww na mgombea wako. Kwa taarifa yako hata Membe na Lipumba wanasema watashinda, hiyo ndio maana ya ushindani. Kuna matusi na ukweli unaoumiza, jitahidi kutenganisha haya mambo mawili.

Nchi hii ina miaka 6 na raia 59m+, mpaka sasa waliokuwa marais ni watano tu, hivyo tukitazama hiyo ratio ya miaka na watu, kuwa rais ni bahati zaidi kuliko uwezo. Hivyo iwapo atashindwa kihalali hakuna mwenye tatizo na hilo, maana hiyo ni kanuni sahihi ya ushindani. Suala la yeye kuwa rais halitegemei matamanio yako, bali kura za wananchi.
Hapo sawa,kumbe kujifariji ni muhimu,maana hata lipumba umesema anasema atashinda hapo nimeelewa logic yako kuwa huwez kujikatia tamaa hata kama ukweli unaujua. Moyoni mwako unajua lisu atashinda ila hatatangazwa.
 
Narudia tena, kwenye ushindani kuna kushinda na kushindwa na yote ni matokeo sahihi. Cha muhimu ushinde au ushindwe kihalali hilo ndio la msingi.
Matokeo yeyote kwenye uchaguzi huu bila kujali nani mshindi, yamewaka wazi kuwa nchi hii haiwezi kutawaliwa na ccm tena, kama chama pekee chenye nguvu kwa ridhaa ya wananchi walio wengi.

Ndani ya hii miaka mitano, Magufuli kwa ulevi na matumizi mabaya ya madaraka, yeye na wapambe wake walitaka tuamini kuwa upinzani umekufa, na ccm inakubalika sana. Na hata kama Magufuli alijiandaa kujiongezea madaraka zaidi ya miaka kumi, basi matumaini hayo yamefutika rasmi kwenye kampeni hizi. Na iwapo ccm haitatumia mbinu chafu ambazo ndio nguzo yake pekee inaweza kupoteza dola, na hata kama itashinda basi ni kwa ushindi mwembamba mno. Kwenye uchaguzi huu tuendelee kuomba wananchi wabaki na ukondoo wao, uliovikwa koti liitwalo amani, kinyume na hapo iwapo wapinzani watasimama mshindi halali atangazwe, basi katiba mpya na tume huru ya uchaguzi lazima ipatikane.
 
Hizo ndoto zako wewe ukweli haupo hivyo,bado tupo ambao tunaimani na magufuli na ana nia njema na taifa hili,hizo stress zako kwa kuwa kuna baadhi ya mambo yako yameguswa usitake kutuambukiza na sie tunao ona ana muelekeo fulani. Taasisi zote zinatambua #RAIS NI MAGUFULI hizo ni burudani tu mnaleta,tanzania bado haiwez kutawaliwa na upinzani never sio kwa kizazi hiki.
 
Hilo la watu kuwa na imani na Magufuli sina tatizo nalo na huo ni ukweli ulio wazi. Ajabu ni pale Magufuli na genge lake wanapotumia madaraka yake kushurutisha kila mtanzania kumkubali yeye na chama chake, kupitia madaraka yake. Amegusa mambo yangu yapi, mimi sio muhalifu na ninafanya kazi yangu ya halali na kulipa kodi. Mimi sio muumini wa kiongozi anayeburuza watu na kuendesha nchi kwa vitisho, kama anavyoendesha familia yake. Kama amezoea kuendesha familia yake kidictator, na kuburuza watu wanaomtetemekea kupitia madaraka yake, sio wote tuna hofu hizo.

Hana maendeleo yoyote aliyoyafanya ya kutaka kila mtu amtetemekee, na kutii kila atakacho kwa utashi wake. Tuna mitazamo yetu na matarajio yetu, na hatuamini katika approach zake za kuleta maendeleo. Tunajua ni rais wetu, ila kwa sasa ni wakati na muda halali wa kisheria na kikatiba kupata kiongozi wa nchi. Anapaswa aheshimu box la kura na wananchi wamchague wamtakaye, kama ni yeye hiyo ni sawa, na iwapo sio yeye aheshimu matokeo fullstop.
 
Mzee Kikwete anasema Hana wasiwasi Rais Magufuli atashinda na Chama cha Mapinduzi kitashinda kitaendelea kuongoza Nchi hii! #sasa we vimba kwenye keyboard kuhisi lisu atashinda kalagabaho,labda akuongezeeni idadi ya watoka nje bungeni.
Kwani Kikwete atapiga kura kwa niaba ya watanzania wote ?
 
Kibaya mnataka mpinzani anayeendana na matamanio yenu. Lisu hataki urais kwa kupindua nchi, kama wananchi wanakubaliana naye watampa kura, ndio maana tunasisitiza uchaguzi huru na matokeo yaheshimiwe. Nipe tofauti ya Lisu na Magufuli kwenye matumizi ya mdomo, ukiweza uje na mrejesho wa hilo hapa.

Ni kweli kabisa kuwa changamoto zinaweza zisiishe, ila changamoto hizo zisiwe hizi za kutengeneza kwa makusudi ili kukibeba chama fulani. Kama tatizo lenu ni Lisu, mbona Slaa hakupata huo urais ili tujue kuwa mtu sahihi tofauti na wa sasa, ndio anaweza kuwa rais? Ukiacha Lisu ambaye ni mwiba kwa mgombea wenu, Lipumba, Mgombea wa NCCR nk wanafikia matamanio yenu, wapeni huo urais ili tuamini mnataka marais wenye staha kuliko Lisu.
Mpaka sasa chadema ina viti vingapi?
 
Hilo la watu kuwa na imani na Magufuli sina tatizo nalo na huo ni ukweli ulio wazi. Ajabu ni pale Magufuli na genge lake wanapotumia madaraka yake kushurutisha kila mtanzania kumkubali yeye na chama chake, kupitia madaraka yake. Amegusa mambo yangu yapi, mimi sio muhalifu na ninafanya kazi yangu ya halali na kulipa kodi. Mimi sio muumini wa kiongozi anayeburuza watu na kuendesha nchi kwa vitisho, kama anavyoendesha familia yake. Kama amezoea kuendesha familia yake kidictator, na kuburuza watu wanaomtetemekea kupitia madaraka yake, sio wote tuna hofu hizo.

Hana maendeleo yoyote aliyoyafanya ya kutaka kila mtu amtetemekee, na kutii kila atakacho kwa utashi wake. Tuna mitazamo yetu na matarajio yetu, na hatuamini katika approach zake za kuleta maendeleo. Tunajua ni rais wetu, ila kwa sasa ni wakati na muda halali wa kisheria na kikatiba kupata kiongozi wa nchi. Anapaswa aheshimu box la kura na wananchi wamchague wamtakaye, kama ni yeye hiyo ni sawa, na iwapo sio yeye aheshimu matokeo fullstop.
Karibu tena
 
Back
Top Bottom