ANDREAS SON
Senior Member
- Sep 10, 2014
- 108
- 46
Ivi lengo la kugawanya majimbo kwa kuchelewa ninini na utaratibu wa kugawanyaji na utangazaji majimbo umefatwa? Hasa kwa kuzingatia muda.
Nsimbo ni jimbo la mkoa gani
Jimbo la mafinga mjini lipo mkoa wa njombe!!?
Hao wabunge 26 waliongezeka ni wa majimbo ya kuchaguliwa tu, bado wa viti maalumu watakaongezeka kutokana kuongezeka kwa wabunge wa majimbo.
Hivyo at the end of the day unaweza kukuta Jumla ya Wabunge waliongezeka ni 36 (Wabunge wa majimbo 26 + proportional ya wabunge wa viti maalum 10(?))
Halafu bado sijaona majimbo ya Zanzibar? Ina maana NEC haina mamlaka na majimbo ya Zanzibar?! Kweli Mzee Judge Warioba aliona mbali, huu muungano sio kabisa.
Jambo la kushangaza eti kuna Mtanzania anafikiri kwamba Magufuri atabadilisha hii system iliyomlea! Watanzania akili zetu ni fupi sawa na urefu wa pua zetu (SIC).
Tume imepotoka. Mafinga bado iko mkoa wa Iringa. Mkoa wa Njombe uko kilometa chache sana karibu na Makambako. Kumbuka hata mji mdogo wa Nyololo uko mkoa wa Iringa, sembuse Mafinga ambayo iko jirani na Ifunda/Tosamaganga kuelejea Iringa Mjini.
Hivi wabunge 300 hawatoshi? sijui kama watu wanajua mbunge mmoja tuu ana cost almost 500m kwa mwaka sasa sijui wanaongeza wa nini hawa wakati hata walimu hakuna...zero kabisa wanaofanya maamuzi haya.
Kwa mujibu wa Ibara ya 75(4) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano waTanzania ya mwaka 1977, Tume ya Taifa ya Uchaguzi ina jukumu lakuchunguza mgawanyo wa Jamhuri ya Muungano katika Majimbo yaUchaguzi;
Tume inaweza kutekeleza jukumu hilo mara kwa mara auangalau kila baada ya miaka kumi.
Yafuatayo ndio majimbo mapya....Umaweza kupakua taarifa nzima kwenye kiambatanisho
MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA ONGEZEKO LA
HALMASHAURI
Majimbo 20 yanayoanzishwa kutokana na kuanzishwa kwa
Halmashauri mpya ni:
1. Handeni Mjini
2. Nanyamba
3. Makambako
4. Butiama
5. Tarime Mjini
6. Tunduma
7. Nsimbo
8. Kavuu
9. Geita Mjini
10. Mafinga Mjini
11. Kahama Mjini
12. Ushetu
13. Nzega Mjini
14. Kondoa Mjini
15. Newala Mjini
16. Mbulu Mjini
17. Bunda Mjini
18. Ndanda
19. Madaba
20 Mbinga Mjini
MAJIMBO YALIYOANZISHWA KWA KIGEZO CHA IDADI YA WATU
Majimbo 6 yanayoanzishwa kutokana na idadi ya watu ni:
1. Mbagala Dar es salaam
2. kibamba Dar es salaam
3. Vwawa Mbeya
4. Manonga - Tabora
5. Mlimba - Morogoro
6. Ulyankulu - Tabora
Wanafidia kwenye kuja kufuta viti maalumu. Kwa style hii wanayaongeza kijanja kana kwamba hata vikifutwa viti maalumu idadi irudi/ibaki kuwa ile ile