NEC: Uchaguzi mdogo Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini kufanyika Januari 13, 2018. Je, Kitila kumrithi Nyalandu?

Mimi sipotezi muda wangu, si kusikiliza vikampeni wala kupiga kura namkubali raisi wangu
 
Nitashangaa sana kama Chadema watakubali kushiriki uchaguzi huu.

Namshauri Nyalandu atunze heshima yake ajiweke pembeni na ubatili huu.

Tunawapa onyo Chadema, mkishiriki uchaguzi huu Freeman Mbowe jiandae kutujuwa invisibles, tutakung'owa hata kwa mapanga kwenye hiyo nafasi yako.

Wewe Mbowe utakuwa ni sehemu ya wasaliti wa Taifa hili.

Movement iliyopo sasa tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Freeman Mbowe ukienda kinyume na hili tutakushikisha adabu.

Tunakuamini, usinaswe na huu mtego wa maccm.
True aisee... kuna mtu kasema hapo yani kweli ccm waruhusu Nyalandu arudi bungeni?! Ni ngumu kuamini... labda useme wamrudishe strategically tu, kwamba wenyewe watashinda majimbo mengine yote (including longido na kinondoni offcourse) na kata nyingine zote zilizobaki alafu wamwache Nyalandu ashinde ili wawe wanasema kama sisi wezi mbona Nyalandu kashinda...lakini hata hivyo upinzani itakuwa bado imepoteza...
 
Ushindi wa mezani mnaoshauri kuupa CCM siku zote ni point 3 na goal 3 bilaaa!!!...ingieni uwanjani CHADEMA testini Nyalandu muangalie upepo!!..You gotta nothing
to loose :D

Inamaana waende kupigania ubunge wa Nyalandu tu? Kwa hiyo chadema wakilipata tu hilo jimbo la nyalandu na kupoteza hayo majimbo mengine na kata zote ndio watajua upepe upo kwao?! Sio kwamba wanatakiwa kupigania kurudisha majimbo yote ya upinzani na kupata kata angalau 3/4?

Nyalandu akishinda ni kwasababu ccm watakua wamemwacha kama karata ya kutumia baadaye...
Upinzani wasiende kwenye huo uchaguzi kama hawana uhakika wa kurudisha majimbo yote ya upinzani na kushinda kata angalau 3/4
 
Focus kubwa kwa singida ipo kwenye jimbo la Nyalandu hata kama kuna kata zinashiriki pia..
 
Ingekuwa mm ndo Mwenyekiti wa Chadema nisingempa apeperushe bendera ya chama hope kuna mgombea wa 2015 aliyepambana na Nyalandu ningemkabidhi apeperushe benderaaa hawa watu wanaohamaham siyo wa kuaminiwa kabisa........

Ni kweli unachozungumza lakini ni lazima pia utambue kuwa Kumpa nafasi mtu kama Nyarandu ni kuitangaza Chadema kwenye hilo jimbo ambapo ni wazi kuwa Nyalandu ataungwa mkono kwa wingi wa kura.
Na bila shaka yoyote CCM hawawezi kushinda jimbo hilo labda kwa wizi na ufisadi wa kura na uvunjaji wa sheria za uchaguzi na ukiukwaji wa maadili ya uongozi hasa wasimamizi wa uchaguzi kukosa maadili mema na uadilifu kwa viapo vyao.

Jambo la Msingi ni viongozi wa Chadema kuonyesha dhamira ya kweli ya kujenga chama badala ya usanii wa kulalamika kuibiwa kura bila kwenda mahakamani na kuthibitisha wizi huo.
Na ikithibitisha kuwa Kuna mkurugenzi au msimamizi wa uchaguzi aliyetangaza mtu aliyeshindwa badala ya mshindi basi iwe ni sababu ya kuweka shinikizo kubwa huyo mkurugenzi afukuzwe kazi kwa kukosa uadilifu na kulisababishia taifa hasara kwa maslahi binafsi.

Wizi wa kura ni wizi kama wizi wa madini, maliasili n.k. Kwa kua wote ni matokeo ya kukosa uadilifu.

Mtu anayeiba kura bila kujali kuliingiza taifa kwenye hasara hana tofauti na wahujumu uchumi.

Pia wapinzani wabadili mbinu za kulinda kura.
Walinde kisayansi sio kila mwaka kukaa mita 200 matokeo yake ni kupigwa mabomu huku wakiibiwa kura kila siku.

CCM nao waache woga wa kushindwa.
Wakubali tu kuwa miaka inavyokwenda ndivyo wanavyopoteza nguvu kwani Chadema kina vijana wengi na pia watoto wanapenda chadema.
 
Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani(2018).

Katika majimbo hayo matatu ni jimbo moja pekee ambalo tayari limepata mgombea .Lazaro Nyalandu atagombea jimbo hilo kupitia CHADEMA.

Je atakutana na nani kutoka CUF, NCCR, ACT na CCM? Je atashinda? Vipi akishindwa ataomba kurudi CCM na kusema CHADEMA haina nia ya kushika dola?

=======

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetangaza ratiba ya uchaguzi mdogo katika majimbo ya Singida Kaskazini, Longido na Songea Mjini na kata sita za Tanzania Bara ambao utafanyika Januari 13 mwakani.

Akitoa taarifa kwa umma jijini Dar es Salaam leo Jumamosi, Makamu Mwenyekiti wa NEC, Jaji mkuu mstaafu wa Zanzibar, Hamid Mahmoud Hamid amesema tume imetangaza uchaguzi huo baada ya kupokea barua kutoka kwa Spika ya kwamba nafasi ziko wazi.

Jimbo la Singida Kaskazini liko kutokana na kujivua uanachama wa CCM aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo, Lazaro Nyalandu, Songea Mjini baada ya kifo cha Leonidas Gama na Longido baada ya Mahakama kufuta matokeo ya uchaguzi yaliyokuwa yamempa ushindi Onesmo Ole Nangole.

Akizungumzia uchaguzi wa kata sita amesema waziri mwenye na serikali za mitaa kwa kuzingatia masharti ya kifungu cha 13(1) cha Sheria ya Uchaguzi ya Serikali za Mitaa, Sura ya 292, aliitaarifu Tume kuwepo nafasi wazi za madiwani katika kata hizo Tanzania Bara

Alizitaja kata zinazohusika katika uchaguzi huo kuwa ni Kimandolu(Arusha), Kihesa (Iringa), Bukumbi (Uyui), Kurui (Kisarawe), Keza (Ngara) na Kwagunda (Korogwe).

Amesema utoaji fomu za uteuzi katika majimbo hayo na kata hizo sita utakuwa ni kati ya Desemba 12 hadi 18, 2017 wakati katika jimbo la Songea Mjini utoaji fumo utakuwa kati ya Desemba 14 hadi 20 mwaka huu.

Alifafanua kuwa kwa upande wa kampeni za uchaguzi huo katika majimbo ya Singida Kaskazini na Longido na kata zote sita zitaanza Desemba 19 na kumalizika Januari 12.

Katika jimbo la Songea Mjini, amesema kuwa kampeni za zitaanza tarehe 21 Desemba, 2017 na kumalizika tarehe 12 Januari, 2018 wakati siku ya uchaguzi katika majimbo yote matatu na kata zote sita itakuwa tarehe 13 Januari, 2017.

Jaji Hamid alivikumbusha vyama vya siasa na wadau wote wa uchaguzi wazingatie sheria, kanuni, taratibu, miongozo na maelekezo yote wakati wa kipindi cha uchaguzi mdogo wa majimbo hayo na kata sita.

Chanzo: Mwananchi
Jimbo tayari limekwisha mpata mwenyewe KM kilichobaki ni taratibu za NEC.
 
CHADEMA msishiriki

Naunga mkono hoja, hakuna haja ya kushiriki uchaguzi ambao cdm wanageuzwa vilema wa kudumu na kuporwa ushindi. Wawaache ccm washiriki na vyama vyake rafiki. Kisha watakapoona hakuna ushindani wa vyama wataanza ushindani wa kikabila na kikanda.
 
acha fikra potofu CHADEMA wanashindwa kihalali kabisa
 
Mie nasubiri tu kauli ya Chadema kwamba kufuatia kupigwa visu, mapanga, marungu na mitutu ya bunduki kwenye uchaguzi wa Madiwani. wafuasi wa Chadema watakaohudhuria mikutano ya kampeni kwenye majimbo hayo wabebe aina yoyote ile ya silaha ili kujilinda na mashambulizi ya hawa wahuni na wauaji.
 
Nitashangaa sana kama Chadema watakubali kushiriki uchaguzi huu.

Namshauri Nyalandu atunze heshima yake ajiweke pembeni na ubatili huu.

Tunawapa onyo Chadema, mkishiriki uchaguzi huu Freeman Mbowe jiandae kutujuwa invisibles, tutakung'owa hata kwa mapanga kwenye hiyo nafasi yako.

Wewe Mbowe utakuwa ni sehemu ya wasaliti wa Taifa hili.

Movement iliyopo sasa tunataka katiba mpya na tume huru ya uchaguzi.

Freeman Mbowe ukienda kinyume na hili tutakushikisha adabu.

Tunakuamini, usinaswe na huu mtego wa maccm.

SASA mkuu wasiposhiriki hawa maCcm siNdio yatafurahi zaidi,,na kwa utawala wa huyu mtu sidhani km ili la tume huru litawezekani, ,, me naona Chadema washiriki lakini wajiandae kama wanaenda kwenye vita vya jihad sio uchaguzi
 
..CCM wamekuja na utaratibu mpya kwamba wagombea wao lazima wawe wakazi wa eneo wanalogombea.

..Je, Prof.Kitila ametimiza kigezo hicho kipya?
Hili akiulizwa polepole nina uhakika hatajibu haa adhikiri uchi
 
Mie nasubiri tu kauli ya Chadema kwamba kufuatia kupigwa visu, mapanga, marungu na mitutu ya bunduki kwenye uchaguzi wa Madiwani. wafuasi wa Chadema watakaohudhuria mikutano ya kampeni kwenye majimbo hayo wabebe aina yoyote ile ya silaha ili kujilinda na mashambulizi ya hawa wahuni na wauaji.

Ilo ndio linalotakiwa, na wao wajiandae km wanaenda vitani
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hapo hakuna kupita mpinzani hata ukipata kura zote hutangazwi au zitaongezwa zingine Mara tatu zaidi uonekane umeshindwa.Fikiria uchaguzi wa madiwani Kuna vituo vilikuwa na wapiga kura 104 lkn mgombea wa ccm anapata kura 350.Akili mukichwa
Halafu wanasema walifanya siasa za kisayansi kwenye uchaguzi wa kisayansi, kura ziliundergo osmosis na assimalation kisha zikadifuse, hahaha
 
Back
Top Bottom