NEC tusaidieni kujibu hoja za wananchi

naulza tu, kama wanadai watu waende nymban,je hay matokeo yanabandkwa nje ya ktuo anawekewa mbuz asome? tutabak tu
 
Inawezekana huu ndiyo uchaguzi wako wa kwanza matokeo yanabandikwa na msimamizi wa kituo wakishirikiana na mawakala wa vyama vya siasa na waangalizi wakiwepo.
 
Kwani Matokeo Yanabandikwa Saa Ngapi Na Wewe Unapiga Kura Saa Ngap?Vituo Vinafungwa Saa 10,kwanini Usiende Nyumbani Ukarudi Saa Muda Huo?Kama Sio Kutafuta Shari Nini?
 
Mita mia kutoka kituoni kwangu ni bar, nitakua nimechili hapo na kalite kabariiiiidi.
 
Kwani Matokeo Yanabandikwa Saa Ngapi Na Wewe Unapiga Kura Saa Ngap?Vituo Vinafungwa Saa 10,kwanini Usiende Nyumbani Ukarudi Saa Muda Huo?Kama Sio Kutafuta Shari Nini?

Hautakiwi urudi kuangalia matokeo, kaa huko huko kwako matokeo yatatangazwa na tume kupitia vyombo vya habari
 
naulza tu, kama wanadai watu waende nymban,je hay matokeo yanabandkwa nje ya ktuo anawekewa mbuz asome? tutabak tu

Tatizo lako ni uelewa mdogo, mbona umekwenda kuhakiki jina lako kwenye ofisi za kata. baada ya kubandika utakwenda kusoma na kwa kuwa umezoea kuambiwa, basi utapewa taarifa.
 
Ikiwa mmetoa agizo kuwa mtuakisha piga kura inabidi akae umbali wa Mita mia moja je hivyo vituo ambavyo vipo ndani ya makazi ya watu inamaana watu wanaoixhi na vituo jilani baada ya kupiga kula watarudi nyumbani au ndo mita mia moja bado zinahusika? Maana umbali wakutoka kituoni mpaka kwenye nyumba zetu izo Mita mia moja mbona hazifiki? Tunaomba majibu tafadhali halaka sana mana siku Nazo zimeish.
 
Inawezekana huu ndiyo uchaguzi wako wa kwanza matokeo yanabandikwa na msimamizi wa kituo wakishirikiana na mawakala wa vyama vya siasa na waangalizi wakiwepo.
hujajibu ndugu, wanabandika ili iweje, ndege wasome?
 
Suala hapa si kuwaamini mawakala,tatizo ni kuwa mawakala wanatishiwa na kukazimishwa kugeuza matokeo.pili kutokuwepo watu umbali wa mita mia moja kutapelekea watu kuja na kura bandia au kujitokeza watu wasio wamitaa hiyo kuja kupiga kura,ndio maana watu wakaambiwa kukaa mita 100 hili endapo itatokea wkala analazimishwa kukubaliana kuhujumu natokeo apige kelele ili wananchi wasogee kusaidia mambo yaende vyema.
 
Mwaka 2010 pale ubungo wasimamizi wa uchaguzi walitaka kulazimisha kuondoka na mabox ya kura na laptop iliyokuwa inatumika kwa ajili ya majumuisho ya kura ili wakachakachue baada ya kuona kwamba mgombea wa ccm amepigwa china. Kama isingekuwa vijana wanamsapoti Mnyika waliokuwa wamebaki hapo kituoni story ya mshindi wa ubunge ingekuwa nyingine. Mimi naamini kama haki itatendeka hakuna hata mmoja atakayeleta fujo. Fujo zitaletwa na ccm kutaka kulazimisha ushindi kama ambavyo imekuwa kawaida yao sehemu nyingi hapa nchini wakati wa uchaguzi. Mwaka huu wanaona wamekamatika kwelikweli na ndio maana wanalazimisha watu kuondoka vituoni ili kama ikiwezekana iwe rais kuiba kura kwa njia wanayoijua wao.

Mkuu Mwaka Huu Kura Zote Zinahesabiwa Vituoni Mabox Yatakuwa Kama Ushihidi Tu....
 
Wana Jamvi,

Baada ya kupiga kura mnashauriwa mrudi nyumbani mkasubiri matokeo huko! Hivi si yanabandikiwa Kituoni? Au Tume itapitisha matokeo nyumbani kwa kila mpiga kura?! Na yakiwa tayari kubandikwa kituoni, tajuaje tayari yamebandikwa na Mie sipo hapo Kituoni?

Nani hasa alitunga hii sheria ya kuondoka kituoni na kwa maslahi ya nani? Wana sheria mpo hapa, kwa nini msiipeleke mahakani Tume ili mahakama itoe ufafanuzi wa Mita 200 kutoka kituoni?

Inanikera sana sheria hii.....
 
Kuna haja safari hii NEC kubadili mwelekeo kwa kuweka eneo la wazi /nje kabisa mabox ya kuwekea kura zilizopigwa karibu na vituo husika ili kila mmoja aone kinachoendelea!


Nigeria imewezakana na kwetu inawezekana. Mpango wa kutumia vyumba vya madarasa na ofisi iwe tu panapojitokeza hali ya mvua tu siku husika ya upigaji kura.






 
Baada ya Rais kutishia kuwakamata watakaobaki vituoni baada ya kupiga kura, wana CCM wameshangilia na wengine kuanza kuwa na matumaini. Kwa nini? Tafakari haya:

- CCM ni wezi wa kura, UKAWA ni walinzi wa kura
-Tuhuma Za siku nyingi kuwa CCM wanaiba kura, zimethibika pasipo shaka

kama rais angekuwa anasema watu watoke ili wassibe kura, ningeelewa.

Tunasogeza moto karibu na petroli.


Kwa sasa ndiyo wimbo wa Lumumba hakuna kulinda kura! Wanahofu nini?
Tatizo liko wapi watu kusubiria matokeo kituoni ?
 
Tume ya uchaguzi imetangaza na kuweka wazi kuwa kura zitabandikwa vituoni.

Tume ya uchaguzi imetangaza na kuweka wazi kuwa ni lazima kila mpiga kura arudi nyumbani.

Maswali kwa Tume ambayo ni huru:-

1. Matokeo ya kura yatatoka saa ngapi kwenye vituo?

2. Matokeo kwenye vituo yatabandikwa saa ngapi?

3. Kama wapiga kura hawapo nani anabandikiwa hayo matangazo (maana wanaobandika tayari wanayajua)?

4. Nani atatangaza kuwa sasa wapiga kura waje kuona matokeo?

5. Watatangaza wapi na kwa njia zipi?

6. Kama wananchi hawaruhusiwi vituo vya kupiga kura mara baada ya kupiga kura, kwa nini matokeo yasibandikwe sehemu nyingine ili wananchi wakayaone hapo?

7. Pale ambapo sheria iko kimya tafsiri ya nini kifanyike inatolewa na nani?
 
Kifungu cha 104(1) cha sheria za uchaguzi,sura ya 343 kinasema;

Mtu yoyote haruhusiwi kufanya mkutano siku ya uchaguzi au ndani ya majengo ambako upigaji kura unaendelea au sehemu yoyote ndani ya mita 200 ya jengo hilo akiwa amevaa au kuonyesha bango,picha au nembo kwa ajili ya kumpigia debe mgombea kwenye uchaguzi huo.

Wataalamu wa sheria naomba tafasiri ya sheria hii?
 
kufanya mkutano-tafsiri pana ya neno mkutano wakati wa uchaguzi ni lipi??!!

Ndani ya mita 200,maana yake nje ya mita 200 ni ruksa au nakosea??!!

Watu kukaa nje ya mita 200 kuna tatizo gani haswa??!! NEC na serikali ya CCM mnataka kupika matokeo,kwa nini iwe nongwa safari hii??!!
 
Kifungu cha 104(1) cha sheria za uchaguzi,sura ya 343 kinasema;

Mtu yoyote haruhusiwi kufanya mkutano siku ya uchaguzi au ndani ya majengo ambako upigaji kura unaendelea au sehemu yoyote ndani ya mita 200 ya jengo hilo akiwa amevaa au kuonyesha bango,picha au nembo kwa ajili ya kumpigia debe mgombea kwenye uchaguzi huo.

Wataalamu wa sheria naomba tafasiri ya sheria hii?

Unataka tafisi gani ya kilugha au?

 
Mimi naamini NEC hawana tatizo na watu kukaa mita 200 kama watataka kusubiri matokeo. Kama mnakumbuka Lubuva alipinga kwa nguvu zote pale Mbowe aliposema watu wakae mita 100 na kama nakumbuka sawa sawa yeye mwenyewe alisema sheria inasema mita 200 na akasoma vile vile ile sheria ya mita 300 ya serikali za mitaa....

Mbowe na yeye juzi amesisitiza sheria inaruhusu mita 200 hivyo aliwaambia wananchi alipokuwa anahutubia mkutano kwamba wasiondoke hata kama Kikwete kasema hivyo kwani hawavunji sheria yeyote kwa kukaa mita 200. Kwa hiyo kama NEC wanakubali mita 200 na UKAWA wanakubali mita 200 tatizo linatoka wapi ? Kama ni tatizo la Kikwete na chama chake, hayo yatakuwa ni matatizo yao binafsi......

Kuhakikisha hili nimewapigia NEC kupitia kituo cha huduma kwa wapiga kura namba 0800782100 nao kwa uwazi kabisa wameniambia kama utataka kukaa kusubiri matokeo then hakikisha unakaa umbali wa mita 200 kutoka kituoni....vile vile wakaniambia unaweza ukaendelea na shughuli zako na baadaye kwenye saa kumi na mbili hivi unaweza kurudi kuangalia matokeo yaliyobandikwa kama utapenda kufanya hivyo.......

Kikwete na CCM yake ndio wenye matatizo na wasipoangalia wanaweza wakiingiza nchi kwenye vurugu kwa kulazimisha vitu ambavyo haviko kisheria......
 
Back
Top Bottom