NEC sasa yagoma kuwalipa mawakala | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

NEC sasa yagoma kuwalipa mawakala

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by Rutashubanyuma, Oct 24, 2010.

 1. Rutashubanyuma

  Rutashubanyuma JF-Expert Member

  #1
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 24, 2010
  Messages: 85,363
  Likes Received: 60,877
  Trophy Points: 280
  Kinyume na makubaliano kati ya vyama vya siasa na NEC katika dakika za lala salama kuelekea uchaguzi NEC wamegoma kuwalipa mawakala na kuwatupia zigo hilo vyama husika.

  Leo kiongozi mmoja wa NCCR MAGEUZI alionekana Channel Ten jioni hii akilia na NEC kwa kukiuka makubaliano yake na vyama vya siasa.

  Zimekuwepo shutuma nyingi dhidi ya NEC kuyachakachua matokeo na kuwanufaisha CCM na hili ni jipu jingine ambalo laweza kupasuka wakati wowote ule.

  Mawakala wa vyama vya siasa ndiyo inasadikiwa ni karata turufu ya kumwokoa JK na CCM kutoka kwenye kibanio cha kudhalilishwa vibaya na Chadema kwenye chaguzi hii.

  Hivyo kutowalipa mawakala yawezekana kabisa kuwa ni njama ya kuwaweka mawakala hao katika hali ya tafurani ambayo endapo vyama vyao vikishindwa kuwalipa CCM ikawalipa na hivyo kuzua utata wa wanawajibika kwa nani na hivyo kuufanya uchaguzi huu kutokuwa wa huru na wa haki.

  Pamoja na Mwenyekiti wa NEC kuahidi chaguzi hii kuwa ya huru na haki yapo matendo mengi ya NEC yanayoashiria kuwa nia hii siyo ya dhati na kutoka moyoni.

  Zimekuwepo kauli za kutofautiana kati ya NEC na wasimamizi wa chaguzi majimboni na hili NEC imeshindwa kuwakemea wasimamizi hao au hata kutoa mwongozo unaoeleweka hususani kwenye eneo la wapigakura kuwa mita 100 kutoka vituo vya kuhesabia kura kuhakikisha haki inatendeka........Msimamizi wa Tarime amedai wapigakura wajiendee majumbani na watajulishwa matokeo jambo ambalo Naibu Mwenyekiti wa NEC tayari alikwisha kutoa mwongozo tofauti kabla ya hapo alipouulizwa swali na mgombea ubunge wa jimbo la Bukoba mjini Bw. Rwakatare..........NEC walisema ni ruhksa kwa wapigakura kuwa mita 100 kutoka vituo vya kupiga kura............
   
 2. Bado Niponipo

  Bado Niponipo JF-Expert Member

  #2
  Oct 24, 2010
  Joined: Aug 15, 2008
  Messages: 680
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 35
  Hii ungeunganisha na ile nyingine mkuu.
   
 3. c

  chanai JF-Expert Member

  #3
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Ni njama tu ili kupunguza nguvu ya CHADEMA. Wanajua CCM imejikusanyia fedha nyingi za kiufisadi na wanaweza kuwalipa mawakala na kuwaonga walalahoi. Kwani hujui NEC ndo CCM?
   
 4. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #4
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  this was not unexpected... lots of money involved by a corrupt system to finish off vichwa ngumu

  lets wait for 2015, inshallah
   
 5. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #5
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  si chadema pekee hata kafu zanzibar na bara, tusisahau kafu ni chama muhimu sana

  CCM is very smart, bilioni 70 kwa miraji, vijisenti kwa uchaguzi na mawakala

  LOL
   
 6. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #6
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,937
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  hatuhitaji watulipe, kama wanataka wawalipe mawakala wa CCM, sisi tutajilipa wenyewe, KURA NI ZETU MALIPO YA NINI? TUTALINDA KURA ZETU KWA GHARAMA ZETU.
   
 7. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #7
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Ndiyo maana tunasema tena, na nimeshauri ktk thread nyingine kuhusu mawakala kutokulipwa. Majibu ni haya.
  MOJA: TUME ISHITAKIWE KWA UMOJA WA ULAYA- EU, NA WAFADHILI AMBAO NDIO WALISHATOA FEDHA ZA UCHAGUZI NA PIA WASHITAKIWE MAHAKAMANI.

  PILI, VYAMA VIANDAE MAANDAMANO YA AMANI HARAKA, WAWASILISHE UKIUKWAJI HUU KWA UMOJA WA ULAYA, UBALOZI WA MAREKANI WAUJUE UNAFIKI NA UOZO HUU NA PIA KESI MAHAKAMANI.

  TUME KWA MBINU HII YA UOVU, INAISAIDIA CCM ISHINDE KWA WIZI NA KUHONGA MAWAKALA.
   
 8. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #8
  Oct 24, 2010
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,275
  Likes Received: 353
  Trophy Points: 180
  Dr alisema jana ulinzi wa kura ni kazi yetu achana na mawakala
   
 9. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #9
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  wewe unaongea hivyo kwasababu haupo kwenye ground.. tumezoea

  bila pesa kura zinaibiwa... hebu niambie wewe ni wakala wa wapi?? au ndio walewale mavuvuzela??

  You have posted something that shows you are not on teh ground

  bila pesa za wakala kura huna

  njaa kali
   
 10. TIMING

  TIMING JF-Expert Member

  #10
  Oct 24, 2010
  Joined: Apr 12, 2008
  Messages: 21,838
  Likes Received: 111
  Trophy Points: 145
  do you trust EU??? unadhani hao richmond, tanzania one, GGM etc wanapata wapi sapoti

  wake up buddy
   
 11. zumbemkuu

  zumbemkuu JF Bronze Member

  #11
  Oct 24, 2010
  Joined: Sep 11, 2010
  Messages: 8,937
  Likes Received: 489
  Trophy Points: 180
  ACID njaa ya watu haipo kwenye uwakala, njaa ya watu ipo kwenye mabadiliko, na hili km huliamini subiri uchaguzi upite. chaguzi ndogo za Tarime pamoja na nguvu kubwa ya CCM bado walishindwa, KUMBUKA TARIME YA JUZI NDO TANZANIA YA LEO.
   
 12. Not_Yet_Uhuru

  Not_Yet_Uhuru JF-Expert Member

  #12
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 11, 2010
  Messages: 1,305
  Likes Received: 7
  Trophy Points: 0
  Guys, the concept behind this ni kuwa, the matter is made kwown to the whole world rather than assuming that here is no impact that can be made. Something is greater than nothing. these people need to be fully exposed.
   
 13. c

  chanai JF-Expert Member

  #13
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 279
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Jamani jambo hili ni la msingi sana hasa maeneo ya vijijini. Unajua Tshs 10,000 kwa watu wa vijijini ni sawa la milioni kwa watu wengine. Nafikiri hoja hii ya NEC kutowalipa mawakala ni njia muhafaka ya kuutengenezea ushinsi CCM. Nina uhakika mawakala wengi wa vijijini kama watashindwa kulipwa ni rahisi sana kushawishiwa kuchakachua matokeo. Kuna haja ya kuliangalia suala hili kwa kina
   
 14. tzjamani

  tzjamani JF-Expert Member

  #14
  Oct 24, 2010
  Joined: Oct 9, 2010
  Messages: 997
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Jamani hela ya mawakala ni muhimu sana. Hilo ni tengo la CCM. wapinzani wakomae na NEC. hela ipatikane else sijui kama kuna means zingine za kupata hizo hela.
   
 15. Msanii

  Msanii JF-Expert Member

  #15
  Oct 24, 2010
  Joined: Jul 4, 2007
  Messages: 6,418
  Likes Received: 347
  Trophy Points: 180
  Kinachowatia hofu NEC ni hii hali anayokumbana nayo bosi wao. lazima walinde mkate wao atii.

   
Loading...