NEC kuvuruga uchaguzi, watoa takwimu za uongo

NEC kuvuruga uchaguzi, watoa takwimu za uongo

Shobi

JF-Expert Member
Joined
May 31, 2015
Posts
3,401
Reaction score
4,391
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwanvuli wa Ukawa, Juma Duni Haji alipokuwa akizungumza na waandishi mjini hapa. Mgombea huyo alisema kuwa takwimu zilizotolewa na NEC hazina ukweli wowote na kuna kila sababu ya kutolewa ufafanuzi takwimu hizo wamezipataje.

Amesema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi inaonesha watu ambao wanastahili kupiga kura ni milioni 23.7 na vituo vyote vya kupigia kura vitakuwa ni 72,000 na kila kituo kitakuwa na watu 450. Amesema katika kufanya ujanja ujanja NEC inaonekana kuwa na wapiga kura hewa milioni tisa ambapo kuna
vituo hewa 20,000 kwa ni vituo halisi vinatakiwa kuwa 53,000 na siyo 72,000.

Mbali na hilo Haji alifafanua kuwa kwa hesabu ya kuwa na vituo 72,000 kama hesabu ya Tume inavyoelekeza ni wazi wapiga kura wanatakiwa kuwa milioni 32 na siyo milioni 23 tena. Kutokana na hali hiyo Duni amemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva kuhakikisha anatoa mchanganuo mzuri wa mahesabu ya wapiga kura vituo utoa. "Kamwe hatuwezi kukubali tume kwa kushirikiana na serikali kutafuta ushindi wa goli la mkoni kama ilivyozoeleka kwa chama hicho.

"Hata hivyo natahadharisha serikali ikilazimisha kutaka inachokitaka wao, bila kusikiliza watu wanataka nini, ni wazi kuwa kunaweza kutokea machafuko kwani watanzania kwa sasa wamechoka na wanataka mabadiliko," alisisitiza Duni.

Akizungumzia kuhusu safari zake, amesema mpaka sasa kafanya mikutano katika majimbo 130 ambayo mengi yao yapo vijiji na watanzania wanamalalamiko yanayofanana. Amesema wananchi wamechoshwa na manyanyaso kwani wamekuwa wakimbizi katika nchi yao na mbaya zaidi wananyanyaswa na wazawa wenzao na wala siyo wageni.

Amesema watanzania wamechoshwa na mipango isiyokwisha ambayo uchangishwa kwa lazima bila kuona mabadiliko yoyote ya ambayo wanatakiwa kuyapata. Almesema watanzania wengi wanakumbwa na huduma mbovu ya afya, elimu, miundombinu, ukosefu wa walimu mashuleni pamoja na shule nyingi kukosa madawati.

Mbali na hilo alieleza kuwa amebaini kwamba wanachi wengi hawana uhuru kwa kufanya kile wanachokitaka kutokana na watawala wengi kuwatisha wananchi. "Inasikitisha jinsi askari wanyama pori wanavyowashambulia wananchi hususani wale wanaoishi karibu na hifadhi jambo ambalo linaanyima
haki wananchi kufanya maamuzi," amesema Duni.

Chanzo: Mwanahalisi
 
mmh kuachia madaraka jamani sio kazi rahisi,na huku wanajua wamemjeruhi mzee wa mvi na ameshasema hana marafiki tena CCM unategemea nini?ila mwaka huu piga uwa tunataka uchaguzi ulio huru na mshindi apatikane kwa kura sio visingizio vyenu,yaani tuko tayari kwa lolote mwaka huu hatutakubali ng'o
 
hili la takwimu za wapiga kura million 23 linatia shaka na ni vzur UKAWA ikalishupalia!
 
mbivu na mbichi zitajulikana 25 oct, i so tired na utawala wa CCM
 
Mwanzo walikuwa wame estimate vituo 40,000 hili ongezeko nila kutilia shaka mbona kubwa sana kutoka 40,000 hadi 72,000 lazima kuna kitu.

Hebu soma hapa.

Jaji mstaafu Lubuva asema vituo vya kupigia kura vitaongezeka kutoka 20,000 na kuwa zaidi ya 40,000 ili Watanzania wasishindwe kupiga kura, Bosi wa ZEC asema changamoto inayowakabili ni wanasiasa kutoamini matokeo wanayotangaza.

Bagamoyo. Mwenyekiti wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), Jaji mstaafu Damian Lubuva amesema vituo vya kupigia kura katika Uchaguzi Mkuu wa 2015 vitaongezeka mara mbili zaidi ya vile vilivyotumika katika uchaguzi uliopita.

Jaji Lubuva alisema hatua hiyo ni mojawapo ya njia za kukabiliana na changamoto ya Watanzania wengi kutokushiriki katika uchaguzi kutokana na umbali wa vituo.

Alitoa kauli hiyo jana wakati akifungua mafunzo ya wiki mbili kwa watumishi 20 (15 Bara na watano Zanzibar), mjini Bagamoyo yenye lengo la kuwaongezea uwezo wa kukabiliana na changamoto ambazo hujitokeza nyakati za uchaguzi mkuu.

"Mchakato wa daftari kwa sasa umefikia kwenye hatua nzuri, tunajiandaa kupata vifaa lakini idadi ya vituo itakuwa zaidi ya 40,000 ukilinganisha na takriban 20,000 vya mwaka 2010. Hii itasaidia kushawishi Watanzania kujitokeza kwenda kupiga kura," alisema Jaji Lubuva na kuongeza:

"Changamoto nyingine ni elimu ndogo kwa wapigakura wanaohama eneo moja kwenda jingine bila kufuata utaratibu, matokeo yake wanakosa haki ya kupiga kura."

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC), Salim Jecha Salim alisema imani ndogo ya matokeo miongoni mwa wanasiasa imekuwa ni moja kati ya changamoto kubwa inayowasumbua katika nafasi zao.

"Hiyo ni changamoto ambayo imekuwa ikijitokeza mara kwa mara katika chaguzi, wengi wamekuwa hawana imani kabisa na matokeo tunayokuwa tunatoa katika kipindi cha uchaguzi, hivyo tunachokifanya ni kuwaelimisha Watanzania," alisema Salim.
 
Dalili za kushindwa UKAWA washaanza kulialia mapema na bado mtalia sana tu baada ya october 25 maana hamtakiamini mtakachokipata
 
yaani hapo ndo kuna kazii....naomba vitajwee na kila kimoja kijulikane kiko wapi,,,,ukawa watuchangishe hata hela za mawakala jamen
 
Mmepanic Vibaya sasa mna tumia ujuzi wenu wa mda mrefu wa Kuzusha na kuelezea huo uzushi kuwa ukweli..... Mtamuota Magufuli Mwaka huu.!!!!😃😃😃
 
Amesema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi inaonesha watu ambao wanastahili kupiga kura ni milioni 23.7 na vituo vyote vya kupigia kura vitakuwa ni 72,000 na kila kituo kitakuwa na watu 450. Amesema katika kufanya ujanja ujanja NEC inaonekana kuwa na wapiga kura hewa milioni tisa ambapo kuna
vituo hewa 20,000 kwa ni vituo halisi vinatakiwa kuwa 53,000 na siyo 72,000.

Akili ya Duni Haji ni duni.Tume ilisema kila kituo kitakuwa na watu wasiozidi 450.Vingine vitakuwa na idadi chini ya hiyo kutegemea na mazingira ya eneo.Asichoelewa hapo ni nini? Vijijini maporini kituo chaweza kuwa hata na watu 50.
Duni haji uwezo wake mdogo mno.Tume haijasema kila kituo watakuwa 450 Kamili.

UKAWA kuna wanasiasa uchwara mno ndio maana siwapi kura.Watu ambao hata masikio yao tu hayafanyi kazi.
Na waandishi wa habari msiripoti tu kama maroboti tumieni akili pia.
 
Dalili za kushindwa UKAWA washaanza kulialia mapema na bado mtalia sana tu baada ya october 25 maana hamtakiamini mtakachokipata

Hapo ndipo unapokuja umuhimu wa Elimu ili kukuongezea uwezo wa kupambanua mambo
 
Hivi mnafahamu hata watendaji wa NEC karibu asilimia kubwa wamehamishwa wameletwa wengine wanaosemekana ni watu wa Usalama. Ukienda pale unaweza ukajikuta mtu unayemfahamu wa zamani ni Lubuva peke yake
 
Mmepanic Vibaya sasa mna tumia ujuzi wenu wa mda mrefu wa Kuzusha na kuelezea huo uzushi kuwa ukweli..... Mtamuota Magufuli Mwaka huu.!!!!
Wanazusha au ni maneno ya tume na hesabu ya darasa la pili tu?
 
Mmepanic Vibaya sasa mna tumia ujuzi wenu wa mda mrefu wa Kuzusha na kuelezea huo uzushi kuwa ukweli..... Mtamuota Magufuli Mwaka huu.!!!!😃😃😃
Ccm mlizoea vya kunyonga.
 
Akili ya Duni Haji ni duni.Tume ilisema kila kituo kitakuwa na watu wasiozidi 450.Vingine vitakuwa na idadi chini ya hiyo kutegemea na mazingira ya eneo.Asichoelewa hapo ni nini? Vijijini maporini kituo chaweza kuwa hata na watu 50.
Duni haji uwezo wake mdogo mno.Tume haijasema kila kituo watakuwa 450 Kamili.

UKAWA kuna wanasiasa uchwara mno ndio maana siwapi kura.Watu ambao hata masikio yao tu hayafanyi kazi.
Na waandishi wa habari msiripoti tu kama maroboti tumieni akili pia.

Unapoongelea statistics (nyepesi) kama hizi unatoa average na range. Hawazidi 450 sawa, je, wastani wa kila kituo ni wangapi? Kimahesabu tulitakiwa kuambiwa kuwa wastani wa wapiga kura kila kituo ni "kadhaa" na kila kituo kitakuwa na watu kati ya "xxx" na "yyy"...hapo ndipo hesabu zingekwenda vizuri. Ila ukitaja maximum peke yake unakuwa unatoa takwimu za kibabaishaji. Kama amesema hawatazidi 450 kila kituo, una hakika gani kama idadi kila kituo siyo 450?

Acha kujifanya unajua kwa sababu ya ushabiki tu.
 
Vyama vya upinzani wapewe daftari la wapiga kura na majina ya vituo wakahakiki hao wapiga kura wenyewe hatutaki mikanganyiko na malalamiko wakati wa kupiga kura. NEC fanyeni haraka, hatutaki kujadili mambo yenye majibu rahisi, Hakikisheni kila chama kinasema mambo wanayotaka yafanyike mapema, myafanyie kazi,uchaguzi upite salama na haraka, ili watu waendelee na maisha yao. Mkifanya makosa mahakama ya kimataifa uholanzi inawasubiri,, msije kumalizia maisha yenu jela wengine wakila maisha yao na watoto wao.
 
Unapoongelea statistics (nyepesi) kama hizi unatoa average na range.

Na wewe naona una undugu na Duni haji na akili zenu mnafanana

Kinachoongelewa sio vihesabu koko vya takwimu ulivyokariri darasani ni vitu halisia.Hayo ya kutoa average na range vihesabu vya kitoto havitumiki hapo.Cha msingi huwezi kihesabu ukaambiwa kituo hakitazidi watu 450 na kuna vituo 72,000.Ukaibuka kama mwehu ukachukua 72,000 kugawa kwa 450 kama alivyofanya duni haji.Akiomba kujua list ya vituo angeonekana na akili lakini kufikia CONCLUSSION KUWA TUME IMETOA TAKWIMU ZA UONGO NA WEWE MTAALAMU KOKO WA TAKWIMU UKAUKAUNGA MKONO.iNAONYESHA WAZI KUWA UKAWA HAKUNA WANASIASA WALA WATAALAMU WA TAKWIMU.Hebu fikiria wewe ndie unateuliwa kuwa mshauri wa Takwimu wa Duni Haji si balaa tupu.
 
Lubuva amesema daftari la wapiga kura rasmi litafika vituo siku 8 kabla ya upigaji kura...

Je UKAWA watajuaje VITUO hewa ambayo ndiyo oxygen ya magamba!??????????????
 
Akili ya Duni Haji ni duni.Tume ilisema kila kituo kitakuwa na watu wasiozidi 450.Vingine vitakuwa na idadi chini ya hiyo kutegemea na mazingira ya eneo.Asichoelewa hapo ni nini? Vijijini maporini kituo chaweza kuwa hata na watu 50.
Duni haji uwezo wake mdogo mno.Tume haijasema kila kituo watakuwa 450 Kamili.

UKAWA kuna wanasiasa uchwara mno ndio maana siwapi kura.Watu ambao hata masikio yao tu hayafanyi kazi.
Na waandishi wa habari msiripoti tu kama maroboti tumieni akili pia.

Sasa Duni ndio msomi wao,taabu kwelikweli
 
Back
Top Bottom