NEC kuvuruga uchaguzi, watoa takwimu za uongo

NEC kuvuruga uchaguzi, watoa takwimu za uongo

Nasubiri baada ya uchaguzi Tusikie Ngonjera za jinsi CCM ilivyo tuna mamluki Chadema kuua upinzani !!!?😊
 
Akili ya Duni Haji ni duni.Tume ilisema kila kituo kitakuwa na watu wasiozidi 450.Vingine vitakuwa na idadi chini ya hiyo kutegemea na mazingira ya eneo.Asichoelewa hapo ni nini? Vijijini maporini kituo chaweza kuwa hata na watu 50.
Duni haji uwezo wake mdogo mno.Tume haijasema kila kituo watakuwa 450 Kamili.

UKAWA kuna wanasiasa uchwara mno ndio maana siwapi kura.Watu ambao hata masikio yao tu hayafanyi kazi.
Na waandishi wa habari msiripoti tu kama maroboti tumieni akili pia.

wewe ni pumba? kutoka vituo 20,000 kwa miaka mitano tu vifikie 72,000 hao watu wanazaliwa au wanatagwa?
hivo 20,000 vya uchaguzi uliopita tayari walishazidisha .
WEWE
 
Dalili za kushindwa UKAWA washaanza kulialia mapema na bado mtalia sana tu baada ya october 25 maana hamtakiamini mtakachokipata

Ubongo wako mdogo mno.Hujui hata 1+1.Duu! kweli mwaka huu mchagua CCM lazima tuwapime akili.
 
Kauli hiyo ilitolewa jana na Mgombea Mwenza wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa mwanvuli wa Ukawa, Juma Duni Haji alipokuwa akizungumza na waandishi mjini hapa. Mgombea huyo alisema kuwa takwimu zilizotolewa na NEC hazina ukweli wowote na kuna kila sababu ya kutolewa ufafanuzi takwimu hizo wamezipataje.

Amesema kwa mujibu wa tume ya uchaguzi inaonesha watu ambao wanastahili kupiga kura ni milioni 23.7 na vituo vyote vya kupigia kura vitakuwa ni 72,000 na kila kituo kitakuwa na watu 450. Amesema katika kufanya ujanja ujanja NEC inaonekana kuwa na wapiga kura hewa milioni tisa ambapo kuna
vituo hewa 20,000 kwa ni vituo halisi vinatakiwa kuwa 53,000 na siyo 72,000.

Mbali na hilo Haji alifafanua kuwa kwa hesabu ya kuwa na vituo 72,000 kama hesabu ya Tume inavyoelekeza ni wazi wapiga kura wanatakiwa kuwa milioni 32 na siyo milioni 23 tena. Kutokana na hali hiyo Duni amemtaka mwenyekiti wa tume ya uchaguzi Jaji Damian Lubuva kuhakikisha anatoa mchanganuo mzuri wa mahesabu ya wapiga kura vituo utoa. "Kamwe hatuwezi kukubali tume kwa kushirikiana na serikali kutafuta ushindi wa goli la mkoni kama ilivyozoeleka kwa chama hicho.

"Hata hivyo natahadharisha serikali ikilazimisha kutaka inachokitaka wao, bila kusikiliza watu wanataka nini, ni wazi kuwa kunaweza kutokea machafuko kwani watanzania kwa sasa wamechoka na wanataka mabadiliko," alisisitiza Duni.

Akizungumzia kuhusu safari zake, amesema mpaka sasa kafanya mikutano katika majimbo 130 ambayo mengi yao yapo vijiji na watanzania wanamalalamiko yanayofanana. Amesema wananchi wamechoshwa na manyanyaso kwani wamekuwa wakimbizi katika nchi yao na mbaya zaidi wananyanyaswa na wazawa wenzao na wala siyo wageni.

Amesema watanzania wamechoshwa na mipango isiyokwisha ambayo uchangishwa kwa lazima bila kuona mabadiliko yoyote ya ambayo wanatakiwa kuyapata. Almesema watanzania wengi wanakumbwa na huduma mbovu ya afya, elimu, miundombinu, ukosefu wa walimu mashuleni pamoja na shule nyingi kukosa madawati.

Mbali na hilo alieleza kuwa amebaini kwamba wanachi wengi hawana uhuru kwa kufanya kile wanachokitaka kutokana na watawala wengi kuwatisha wananchi. "Inasikitisha jinsi askari wanyama pori wanavyowashambulia wananchi hususani wale wanaoishi karibu na hifadhi jambo ambalo linaanyima
haki wananchi kufanya maamuzi," amesema Duni.

Chanzo: Mwanahalisi

Duni watu hata hawamuelewi anachoongea yule mwingine anatumia dakika 3 tu upinzani mwaka huu kazi mnayo.
 
Ubongo wako mdogo mno.Hujui hata 1+1.Duu! kweli mwaka huu mchagua CCM lazima tuwapime akili.
attachment.php
 
mwaka huu wa uchaguzi vurugu zinaweza kusababishwa na wafuatao. 1.tume ya uchaguzi- kwa kutokutenda haki.2.jeshi la polis- kwa kusababisha vurugu kwa kuegemea upande mmoja badala ya kuwa neautral.3. viongozi wa vyama vya siasa-kwa kutoa kauli za kiuchochezi kwa wananchi dhidi ya utofauti wao...
 
450x72000=32,400,000.

Duh hawa NEC kama hawatumiki watoe mapema hizo majina ya vituo kila kata watu tuhakiki mapema.

Kwanza hawajatupa muda wa kuhakiki majina yetu.
Hawajatupa muda wa kuhakiki daftari la awali.
Hawajatupa muda wa kuhakiki daftari la kudumu.....

Lubuva fungua macho yako, tenda kazi kwa mujibu wa sheria na haki.
 
mmh kuachia madaraka jamani sio kazi rahisi,na huku wanajua wamemjeruhi mzee wa mvi na ameshasema hana marafiki tena CCM unategemea nini?ila mwaka huu piga uwa tunataka uchaguzi ulio huru na mshindi apatikane kwa kura sio visingizio vyenu,yaani tuko tayari kwa lolote mwaka huu hatutakubali ng'o

Walai hatukubali kabisaa ushenzi ushenzi lazima uchaguzi upended haki
 
hacha ujinga YEHODAYA husiwe mtu wa kukurupuka wewe unaongea km nan hz habar wanazipata wana inteligencia wa ukawa lkn pia inasemekana ni watu milluon 23 ambao wanatarajiwa kupiga kura leo wanatangaza milion 33 huon km kuna kura za wiz hapo?
 
Akili ya Duni Haji ni duni.Tume ilisema kila kituo kitakuwa na watu wasiozidi 450.Vingine vitakuwa na idadi chini ya hiyo kutegemea na mazingira ya eneo.Asichoelewa hapo ni nini? Vijijini maporini kituo chaweza kuwa hata na watu 50.
Duni haji uwezo wake mdogo mno.Tume haijasema kila kituo watakuwa 450 Kamili.

UKAWA kuna wanasiasa uchwara mno ndio maana siwapi kura.Watu ambao hata masikio yao tu hayafanyi kazi.
Na waandishi wa habari msiripoti tu kama maroboti tumieni akili pia.

Hivi kwanza nani ana shida ya kura yako wewe ukawa tupo tumetosha
 
+49 159 04181859

👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿👆🏿
Hiyo ni number whatsapp ya "DW" ujerumani,wanafanya utafiti wa nani anakubalika urais Tanzania.

👇🏾👇🏾👇🏾save hiyo namba na tuma Neno LOWASSA.

Wenzetu wa chama cha mapinduzi CCM wanahamasishana kwa wingi kupiga kura kwa njia ya WhatsApp.
Hivyo ukiwa kama mwana UKAWA kura yako ni muhimu sana.
 
Maranyingi mambo yanayoonekana madogo ndiyo huwa yanaleta utata na kutokuelewana.

Hili lipo ndani ya uwezo wa tume, na ni rahisi sana. Wana idadi kamili ya vituo vyote ambavyo watu walijiandikisha. Kwa vituo vilivokuwa na watu zaidi ya idadi wanayotaka wao katika upigaji wa kura ni vema wakachanganua kwa kuonyesha kwa uwazi mgawanyo wawapiga kura. Kama eneo liliandikisha watu 500, basi ionyeshe watu 450 wanapiga kituo kipi na 50 wanaozidi wanakuwa kituo gani; kuiswe na ukakasi wowote kwa lolote lile. Na kwa maeneo ya idadi pungufu pia wachanganue ieleweke kwakila mpiga kura.
 
Jana niliona ndege inashusha vifaa vya kupigia kura......imeleta kama mara 7 iv ..apo kuna goli la mkono kakabidhiwa mkurugenz ase
 
Huwezi kukubali kushindwa kirahisi tunajua lakin achen maneno wana ukawa bado cku 17 tufikie kileleni...kama mnataka kubadiri tena gia angani semen
 
Kikwete na MACCM wake ni wakuwatupa mto kagera hatutakubali hatutakubali ujanja ujanja
 
Akili ya Duni Haji ni duni.Tume ilisema kila kituo kitakuwa na watu wasiozidi 450.Vingine vitakuwa na idadi chini ya hiyo kutegemea na mazingira ya eneo.Asichoelewa hapo ni nini? Vijijini maporini kituo chaweza kuwa hata na watu 50.
Duni haji uwezo wake mdogo mno.Tume haijasema kila kituo watakuwa 450 Kamili.

UKAWA kuna wanasiasa uchwara mno ndio maana siwapi kura.Watu ambao hata masikio yao tu hayafanyi kazi.
Na waandishi wa habari msiripoti tu kama maroboti tumieni akili pia.

Ninaomba taarifa rasmi ya tume yenye mchanganuo kamili, maeneo yaliko vituo na majina yake ili kuthibitisha kuwa wewe akili yako ni kubwa zaidi ya wenzio...!
 
Dalili za kushindwa UKAWA washaanza kulialia mapema na bado mtalia sana tu baada ya october 25 maana hamtakiamini mtakachokipata

Mkuu unajivunia hila ??????!!
Aibu nyingine Tz !!
Naskia wasimamizi uchaguzi ni lazima uwe Gamba !!??? Yoote hayo kupika matokeo !!!???
 
Back
Top Bottom